Uchaguzi Wa Irani Katika Picha

Uchaguzi wa rais nchini Irani utafanyika tarehe 12 Juni. Ni watu wanne, kati ya watu zaidi ya 400 waliojiandikisha ambao walipewa idhini rasmi na Baraza la Walezi kuwa wagombea. Macho makali ya wanablogu-wapiga picha yamenasa nyakati na taswira katika mitaa ya Irani ambako watu waliwapigia debe wagombea wanaowapenda pamoja na madai yao ya kisiasa.

Maryam Majd alichapisha picha kadhaa kwenye ukurasa wa Feminist School (Shule ya haki za wanawake) kuhusu “uwepo huru wa wanawake katika anga ya uchaguzi.”

Kwenye Feminist School tunasoma kwamba “Tajrish sq. Emamzadeh Saleh (eneo takatifu kaskazini ya Tehran) pamoja na soko maarufu la Tajrish Baazar vilikuwa wapokezi wa wanachama wa kujitolea wa “mseto wa vyama vya wanawake.” Walidai uwepo huru wa wanawake kwenye anga ya uchaguzi. Kauli mbiu yao ilikuwa: “Tunapigia kura haki za wanawake.” Matumaini yao ni kuwa utawala wa Irani utakomesha sheria zote za kibaguzi dhidi ya wanawake.

Saaba Vasefi pia alilinasa kundi hili likiwa kwenye harakati kwenye Feminist School.

Kwenye blogu ya picha ya Zoherpix tunaona jinsi waunga mkono wa Mahmoud Ahmadinejad na wale wa Mir Hussein Mousavi wanavyopepea picha za wagombea wanaowapenda:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.