Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Januari, 2015
Wanawake wa Kiislam na Kikristo Nchini Nigeria Walivyoungana Kupambana na Misimamo Mikali ya Kidini
Mchungaji Esther Ibanga kiongozi wa ki-Islam Khadija Hawaja walianzisha Mradi wa Wanawake Wasio na Mipaka miaka michache iliyopita kama jitihada za kurudisha hali ya usalama na amani katika jamii zao.
Bunge Lililoteuliwa na Jeshi la Thailand Lapiga Kura ya Kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu
Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatra amepigiwa kura ya kutokuwa imani naye kwa 'kosa' la kutekeleza mpango wa kununua mchele unaokosolewa kwa kuliletea hasara na matatizo taifa hilo
Watu 36 Wauawa, Mtandao wa Intaneti Wafungwa Kongo DRC Kufuatia Maandamano ya Kumpinga Rais Kabila
Ghasia na mapigano kati ya Polisi na waandamanaji wanaopinga hatua ya Kabila kurekebisha sheria ya uchaguzi vimesababisha kuuawa kwa watu 36 nchini Kongo DRC katika kipindi cha siku chache.
Wafilipino Walivyomficha Papa Francis Hali Mbaya ya Haki za Kijamii Nchini Humo
Wanaharakati, watoto wa mitaani, na wakazi masikini wa mijini walikuwa baadhi ya watu waliokuwa wamefichwa na serikali wkaati wa ziara ya Papa Francis nchini Ufilipino.
Pamoja na Wapiga Kura Kutilia Shaka Sera Zake, Croatia Yapata Rais Mwanamke
Croatia ipo katika mpasuko mkubwa wa kisiasa. Kolinda Grabar Kitarović ameweza kunyakua kiti cha uRais kufuati ushindi mwembamba alioupata dhidi ya Rais anayemaliza muda wake, Ivo Jospović katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika mwezi Januari, 2015 kwa kupata asilimia 50.74 ya kura zote.