Wafilipino Walivyomficha Papa Francis Hali Mbaya ya Haki za Kijamii Nchini Humo

Human rights groups were blocked by the police from getting near the pope motorcade. Image from Facebook page of Kathy Yamzon

Makundi ya haki za kijamii yalizuiwa na Polisi kuukaribia msafara wa Papa Francis. Picha kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Kathy Yamzon

Fursa ya kumwona kumwona Papa Francis alipoanza  ziara yake ya ki-Papa nchini Ufilipino haikuwa kwa wazi kwa kila m-Filipino aliyetaka. Kikundi cha wanaharakati kilichokuwa na mabango yanayopinga hali mbaya ya haki za kijamii nchini humo kinasema polisi waliwazuia kufanya maandamano mbele ya msafara wa Papa. Kadhalika, kuna taarifa kwamba maafisa wa polisi waliwakamata na kuwaweka kizuizini baadhi ya watoto wa mtaani wakati wa ziara hiyo ya Papa.

Papa Francis alizuru Ufilipino kuanzia Januari 15 mpaka 19. Ziara hiyo, iliyokuwa na kauli mbiu ya “rehema na huruma,” ilimfikisha Papa Francis katika taifa hilo linaloongoza kwa idadi kubwa ya wa-Katoliki nchini Asia.

Kiasi cha wanaharakati 2,000 walikusanyika jijini Manila ‘kumsalimia’ Papa kwa mabango yaliyokuwa na ujumbe wa masuala kadhaa yanayowaathiri masikini wa taifa hilo, kama vile njaa, ukosefu wa ardhi, na uvunjifu wa haki. Polisi hata hivyo  waliwazuia kuukaribia msafara wa Papa.

Kiongozi wa wanaharakati hao Nato Reyes aliikosoa vikali serikali kwa kuyazuia makundi mbalimbali yaliyotaka kujaribu kumweleza Papa kuhusu “hali halisi” ya mambo nchini Ufilipino. :

Kuanzia Siku ya 1, kumekuwa na jitihada za makusudi kujaribu kudhibiti kile ambacho Papa anatakiwa kukiona na kukisikia. Hilo liko wazi kwa sababu Papa hakuja nchini humu kuona kile kinachoitwa “ukweli, mema na mazuri” pekee. Papa amekuja hapa kusikia matatizo ya watu masikini na wanaotengwa.

Police barred a group of activists from marching near the pope motorcade. Photo from Facebook page of Southern Tagalog Exposure

Polisi wakiwazuia wanaharakati kadhaa kuandamana karibu na msafara wa Papa. Picha kutoka kwenye mtandao wa Facebook wa Southern Tagalog Exposure.

Mudwalk performance artists, who depicted the plight of typhoon Haiyan victims, were barred by the police from handing a letter to church authorities. Photo from Facebook page of the group.

Wasanii wa Mudwalk wakioonesha igizo la waathirika wa dhoruba ya Haiyan. Walizuiwa na polisi kukabidhi barua kwa uongozi wa kanisa. Picha kutoka ukursa wa Facebook wa kikundi hicho.

Members of the police confiscate an activist banner along the pope motorcade. Police said only "greeting streamers" are permitted. Photo from Facebook page of Southern Tagalog Exposure

Polisi wakirarua bendera ya mwanaharakati. Polisi wamesema ‘watu waliokuwa wakimshangilia’ Papa tu ndio tu waliruhusiwa. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Southern Tagalog Exposure.

Some political prisoners were able to hang a banner outside their cell. They urged the pope to look into the worsening human rights situation in the country. Photo from Facebook page of Kathy Yamzon.

Baadhi ya wafungwa wa kisiasa waliweza kuning'iniza mabango nje ya vyumba vyao vya magereza. Walimwomba Papa kutazama hali ya haki za binadamu yanayozidi kuwa mbaya nchini humo. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Kathy Yamzon.

Zaidi ya kuwaingilia waandamanaji, serikali pia inadaiwa ‘kuwakamata” na “kuwaweka kizuizini” watoto wa mtaani siku chache baada ya Papa kuwasili. Jarida maarufu la kila siku la Manila Standard Today, lilihoji busara ya sera hii, likisema inamwelekeo unaokaribiana na sera ya Potemkin-Village.

Serikali imekanusha kuwakamata watoto wa mtaani wakati wa ziara ya Papa.

Wakati huo huo, maafisa wa serikali walitengeneza kwa haraka ukuta wa kijani pembezoni mwa barabara ambazo msafara wa Papa Francis ungepita, kwa lengo la kumzuia Papa na watu wengine waliokuwa kwenye msafara huo kuo mitaa wanayoishi maskini pembezoni mwa kizuizi.

Kizuizi kingine kinachomtenga Papa na watu kilikuwa usalama mkali. Wengi walisema kumwagwa kwa polisi na kuwekwa kwa vizuizi vya chuma jijini humo kulizidi kiwango, na kuwafanya watu washindwe kumwona mgeni huyo maalum wa taifa. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti wa ki-Filipino walifananisha ziara ya hivi majuzi ya Papa nchini Sri Lanka, ambapo alionekana akigusa na kubariki mikono ya waumini waliokuwa wamesimama barabarani kumlaki.

Overkill police deployment? Image from Facebook page of labor center Kilusang Mayo Uno (May First Movement)

Polisi walizidi kiwango? Aquino ni rais wa Ufilipino. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa kituo cha kazi cha Kilusang Mayo Uno (Vuguvugu la Mei Mosi).

Papa Francis! Quirino Ave cor Taft Ave akiwa njiani kwenda kwenye uwanja wa MOA Arena majira ya saa 11 jioni

Papa Francis akipunga mono alipokuwa akipita akiwa kwenye gari la Quirino. Mkesha ulifanyika saa 7:14 leo.

Serikali inasema usalama wa hali ya juu ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya tahadhari. Hata hivyo, wengi wanaendelea kuhoji kwa nini serikali haikuheshimu matakwa ya waumini na kuwaruhusu kumkaribia Papa:

Ni kweli kwamba hali hiyo ilikuwa ya lazima kwa usalama lakini ninadhani Papa angependa kuwafikia watu waliokuwa wamefichwa na mamia ya wana usalama.

Nonoy Oplas alikosoa vikali “mfumo wa kiusalama wa kijeshi” unaotumiwa na serikali:

Kumwona barabarani ni jambo la fahari zaidi ambalo watu wangejisikia kuweza kumwona Papa. Na mfumo unakera wa usalama ulijaribu kufanya iwe vigumu kwa watu kumwona Papa kwa karibu kadri inavyowezekana.

Wengi wanatarajia kwamba Serikali itafikiria upya utaratibu wake wa kiusalama katika siku zilizobaki, ili kuwaruhusu watu zaidi kumwona Papa Francis, kabla hajaondoka Januari 19.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.