Aliyekuwa Katibu mkuu wa NATO wa masuala ya uhusiano wa kimataifa Kolinda Grabar Kitarović amechaguliwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa nchi ya Croatia, kwa kumshinda Rais aliyemaliza muda wake katika uchaguzi wa kwanza kabisa mara baada ya nchi hii ndogo ya Ulaya ya Kusini kujiunga na Jumuia ya Umoja wa Ulaya mapema mwaka jana.
Grabar Kitarović alipata ushindi katika mazingira ya upinzani mkali kutoka kwa Rais aliyemaliza muda wake, katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika January 2015, akijizolea asilimia 50.74 ya kura zote, kwa mujibu wa taarifa za matokeo ya awali. Ataapishwa rasmi tarehe 18 Februari, 2015.
Kama Rais wa kwanza mwanamke nchini Croatia, na Rais wa nne wa kuchaguliwa tangu nchi hii ijipatie uhuru wake, bila shaka yoyote ataweka historia kwa nchi yake na ukanda wa Jumuia ya Ulaya. Pamoja na ushindi wake wa kihistoria, raia wengi ambao wangalipendelea Rais tofauti na yeye, wanaonesha hofu yao ni kwa namna gani mawazo na mahitaji yao yatatekelezwa na Rais huyu katika kipindi cha uongozi wake.
Grabar Kitarović ambaye ni mwanachama wa chama cha Umoja wa Demokrasia ya Raia wa Crotia, chama kilichosimamia kupatikana kwa uhuru wa nchi hii mwaka 1992, amenuia kurudisha kile alichokiita “Hulka ya Watu wa Crotia”, pamoja na kusisitiza mambo ya “kiutamaduni”. Nchi hii ina mpasuko mkubwa miongoni mwa makundi mawili ya siasa za kati-kushoto na kati-kulia, na alifanikiwa kumshinda mpinzani wake, Josipović kwa tofauti ya elfu kadhaa tu za kura.
Josipović anakuwa Rais wa kwanza tangu Croatia ipate uhuru kwa kushidwa kuchaguliwa kama Rais kwa awamu ya pili ya uongozi tofauti na maRais wengine kama Franjo Tuđman, Rais wa kwanza wa Croatia, pamoja na Stjepan Mesić ambao wote waliongoza kwa vipindi vyote viwili. Kwa mtazamo wa wapiga kura wengi, Josipović alipokuwa Rais, hakuweza kutimiza mambo mengi waliyoyataka watu wa Crotia.
Kuelekea duru ya pili ya uchaguzi
Harakati za uchaguzi zinaonekana kuwa ziligubikwa na udanganyifu na matumizi makubwa ya fedha. Duru ya kwanza ya uchaguzi ilifanyika tarehe 28 December, 2014, ukiwa na wagombea wanne wa uRais: Ivan Vilibor Sinčić, mwanaharakati mdogo wa kisiasa, ambaye aliwashangaza wengi kwa kupata asilimia 16.42 ya kura zote; Milan Kujundžić, mwanasiasa wa mrengo wa kulia alipata asilimia 6.30 ya kura zote; Grabar Kitarović, anayewakilisha mrengo wa kati-kulia wa chama cha Umoja wa Kidemokrasia wa Chrotia, aliyejizolea asilimia 37.88; na Rais aliyekuwa madarakani Josipović, aliyepata asilisia 38.48% ya kura zote. Rais hawezi kutangazwa hadi pale mgombea atakapopata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote.
Kwa kuwa, hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa kupata zaidi ya asilimia 50 nya kura zote (asilimia 47.14 tu ya wapiga kura wote ndio tu waliopiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi), Grabar Kitarović na Josipović ndio walioelekea kwenye duru ya pili ya uchaguzi iliyofanyika January 11.
Wakati wa kampeni, wagombea walieleza mikakati mingi kwa ajili ya nchi yao, ambayo hadi sasa inakabiliwa na changamoto ya mdororo wa uchumi, kukosekana kwa ajira, kushuka kwa pato la taifa na rushwa. Hata hivyo, pamoja na kiasi kikubwa cha fedha kutumiwa kwenye kampeni, madaraka ya uRais kwa hakika ni machache katika serikali ya Crotia, ambapo Rais kimsingi anakuwa kama muwakilishi ndani na nje ya nchi pamoja na kushughulikia mambo ya sherehe kama vile kuwatunuku watu mashuhuri.
Koliko god se mi dijelili na ovim i budućim izborima u postocima, oni loši gospodarski postoci su isti za sve #izboriprh
— Bruno Zupan (@komacore) enero 11, 2015
Bila kujali ni kwa kiasi gani tunatofautiana katika asilimia za kura katika chaguzi hizi au zijazo, asilimia mbaya za kiwango cha uchumi zitaendelea kuwa zilezile kwa kila mmoja wetu.#izboriprh (#electionscroatia)
Mbali na hali hii, wagombea waliwashawishi wapiga kura pia kupitia midahalo iliyorushwa kwenye vituo vya televisheni, midahalo iliyomfanya mpiga kura wa kawaida kutaka kupata sababu za msingi za kwa nini ampigie kura mgombea mmojawapo. Hata hivyo, midahalo hii iliibua twits za kufurahisha kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wa Crotia kupitia viungo habari #izboriprh (#electionscroatia), #izbori2014 (#elections2014), #debataRTL (#debateRTL), na #HRTizbori (#HRTelections).
Između Ive Josipovića i Kolinde Grabar Kitarović mogu izabrati samo nevažeći glasački listić. #izboriprh #izbori2014
— Vencislav Jularic (@VJularic) enero 8, 2015
Kati ya Ivo Josipovića na Kolinda Grabar Kitarović ninaweza tu kuchagua karatasi kura zisizo sahihi. #izboriprh #izbori2014
Nitko ne očekuje španjolsku inkviziciju #izboriprh #izbori2014
— Ivan (@Setka_i) enero 8, 2015
No one expects the Spanish inquisition #izboriprh #izbori2014
Mada za midahalo kama ile ya WWII war crimes and war profiteering wakati na mara baada ya vita vya uhuru wa Crotia, haukuepukika wakati wa mdahalo uliooneshwa katika televisheni kati ya Josipović na Grabar Kitarović, ambaye pia, aliwahi kuwa balozi wa Crotia nchini Marekani.. Historia ina mchango mkubwa sana kwa Crotia– wagombea wanaonekana kuitumia nafasi hii kujikita zaidi kwenye mada za kihistoria wawapo majukwaani badala ya kujadili mambo ya wakati huu na ambayo ni changmoto kwa raia na mbayo moja kwa moja yanahusiana na maisha ya kila siku ya raia.
Nchi iliyogawanyika kupita kiasi
Grabar Kitarović anaungwa mkono na wapiga kura wa mrengo wa kulia pamoja na Raia wa Crotia wanaoishi nje ya nchi, hawa haswa raia wa Crotia wanaoishi Bosnia-Herzegovina. Katika chi hizi mbili, Croatia na Bosnia-Herzegovina, vituo vya kupia kura vilifunguliwa tangu saa 1 asubuhi hadi saa 1 usiku tarehe 11 Januari, lakini hadi kufika saa 1 usiku huko Mostar, Bosnia, mamia ya watu walikuwa bado katika mistari wakisubiri kupiga kura, kwa hiyo, vituo vya kupigia kura vilikuwa wazi hadi kila mmoja alipopiga kura. Wapiga kura walijipanga katika mistari mirefu na pia walisafiri kutokea maeneo mbalimbali ya Bosnia-Herzegovina kwa ajili ya kupiga kura huko Mostar. Watuamiaji wengi wa mitandao ya kijamii nchini Crotia wanakejeli kuwa Grabar Kitarović ni Meya mpya wa Mostar.
Croatia kwa mara kadhaa imekuwa katika mpasuko wa kisiasa, lakini inaonekana kuwa nchi hii imefikia ukomo katika mpasuko huu. Vyombo vya habari kutoka maeneo tofauti vipo tayari kuweka bayana mfululizo wa taifa jipya la Croatia, ambapo wengine wanasema , ni kama vile bomba la unga wa risasi linapokaribia kulipuka.
Pamoja na kuwa Grabar Kitarović alisema kuwa “atajituma ili kuijenga Crotia iliyo bora zaidi” na ambayo haitabagua au kuwatenga raia kutokana na mrengo wao wa kisiasa, baadhi ya raia katika mrengo wa kulia wameendelea kuwa na mashaka. Twiti moja ilijumuisha mawazo ya kiujumla:
Najtuznije je sto ovaj povijesni dogadaj za jednu patrijarhalnu drzavu vjerojatno ni jedna feministkinja ne smatra pobjedom. #izboriprh
— ena (@bluperception) enero 11, 2015
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa tukio hili la kihistoria, katika nchi yenye misingi ya mfumo dume, bila shaka halichukuliwi kama ushindi kwa yeyote awateteao wanawake. #izboriprh
Libela.org, jarida linalojitegemea la masuala ya usawa wa jinsia, jinsia pamoja na demokrasia nchini Crotia, ilihoji kama Grabar ana uwezo wa kuliunganisha taifa ikiwa ni pamoja na Kitarović is capable of uniting the nation and working kutoa kipau mbele kwa haki za binadamu, pamoja na kuwa hakucheza “female card” wakati wa uchaguzi.
Taifa linajengwa na watu, na watu wa Crotia wameshamchagua Kolinda Grabar Kitarović kama Rais wao anayefuata, na kama jinsi inavyopaswa kufanyika katika nchi yenye demokrasia. Wakati ndio utakaosema kiwango cha umahiri wa chaguo la watu katika kuijenga nchi ya Croatia.