Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Septemba, 2012
Kenya: Wito wa Mshikamano Baada ya Mashambulizi ya Kigaidi
Siku chache kabla ya ufunguzi wa GV2012 mjini nairobi, Kenya ilikumbwa na milipuko na utekaji nyara huko Mombasa na mjini Garissa. Mlipuko ulitokea katika sehemu ya burudani mnano Juni 24 na kuwauwa watu watatu siku moja baada ya ubalozi wa marekani kuonya mamlaka ya Kenya kuhusu mashambulizi hayo jijini. Umati huo ulikuwa umekusanyika katika kilabu kutazama robo fainali kati ya Uingereza na Italia.
Mbinu za Kugundua Dawa Bandia katika Nchi Zinazoendelea
Watu 700,000 hufa kila mwaka kwa kutumia dawa bandia za malaria na saratani pekee. Shirika la Afya Duniani, WHO linasema katika ripoti yake kuwa, mapato kutoka kwa dawa hizi kila mwaka hukaribia dola bilioni 200.
Mexico: Uandishi Kutoka Gerezani
Enrique Aranda Ochoa writes literature from jail. Convicted of kidnapping in 1997 with a sentence of 50 years in prison, Enrique has used his time in jail to write six novels and earn various literature awards. His latest book, available for purchase in an electronic format, focuses on the mysteries of the Mayans.
India: Waume Kuwalipa Wake Zao kwa Kufanya Kazi za Nyumbani
Wizara ya Maendeleo ya Watoto na Wanawake nchini India inaandaa mswada ambao, kama utapitishwa na bunge, utawalazimisha waume kisheria kuwalipa wake zao wanaoshinda nyumbani mshahara wa mwezi, kwa kufanya shughuli za nyumbani. Wizara ya Maendeleo ya Watoto na Wanawake nchini India inaandaa mswada ambao, kama utapitishwa na bunge, utawalazimisha waume kisheria kuwalipa wake zao wanaoshinda nyumbani mshahara wa mwezi, kwa kufanya shughuli za nyumbani.
Uganda: Binti awa Mbunge wa Kwanza Mdogo Kuliko wote Afrika
Afrika inachipuka na wanawake wa ki-Afrika wanachipuka nayo. Hivi sasa, Malawi na Liberia zinaongozwa na maraisi wanawake. Sasa nchini Uganda mbunge kinda kabisa kuliko wote barani Afrika amechaguliwa - naye ni Proscovia Alengot Oromait umri wa miaka 19 .
Je, Sifa ya ‘Kisiwa cha Amani’ Tanzania Imeanza Kutoweka?
Tanzania imeshuhudia matukio kadhaa mabaya tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2010. Tukio la hivi karibuni ni kifo cha kikatili cha mwandishi wa habari wa Tanzania Daudi Mwangosi, aliyeuawa kwa bomu la machozi huko Iringa, Kusini mwa Tanzania, wakati polisi walipojaribu kukitawanya kikundi cha wafuasi wa chama cha upinzani.
Kocha Mfaransa Ateuliwa Kuongeza Bahati ya Kenya Kwenye Kandanda
Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF, limemchagua Kocha mpya wa timu ya taifa la Kenya ambaye ni Mfaransa, Henri Mchel. Wanakamati hao, wana matumaini kuwa anaweza kuwa 'bahati' ya Kenya katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya 2013 na Kombe la Dunia la 2014.
Italia Yalaumiwa kwa Ukiukaji wa Haki za Wakimbizi wa Kiafrika
Februari 23, Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya huko Strasbourg ilikuja na hukumu ya kihistoria kwamba Italia imevujna Tamko la Ulaya la Haki za Binadamu kwa kuwazuia na kuwarudisha wakimbizi wa ki-Eritrea na Somalia kwenda Libya. Abdoulaye Bah anaripoti.
Afrika: Tuzo la Mbuyu wa Dhahabu
Wasilisha kisa chako upate fursa kushinda Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu: “Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu ilianzishwa mwaka 2008 kuwahamasisha waandishi wa ki-Afarika waliojikita katika vitabu vya watoto na vijana.”...
Paralympiki 2012: Mwanzo mzuri, Habari za Kukumbukwa
Martine Wright, aliyenusurika mlipuko wa mabomu uliotokea London, Rim Ju Song, mshiriki wa kwanza kutokea Korea Kaskazini ambaye, miezi michache iliyipita, hakuweza kuogolea; na Hassiem Achmat, ambaye alinusurika kuuawa na papa aliyemshambulia akiwa baharini. Baadhi tu ya washiriki wakuu wa mashindano ya Paralympiki. Martine Wright, aliyenusurika mlipuko wa mabomu uliotokea London, Rim Ju Song, mshiriki wa kwanza kutokea Korea Kaskazini ambaye, miezi michache iliyipita, hakuweza kuogolea; na Hassiem Achmat, ambaye alinusurika kuuawa na papa aliyemshambulia akiwa baharini. Baadhi tu ya washiriki wakuu wa mashindano ya Paralympiki.