Uganda: Binti awa Mbunge wa Kwanza Mdogo Kuliko wote Afrika

Proscovia Alengot Oromait, akiwa na umri wa miaka 19, amekuwa mwafrika mdogo kabisa wa kwanza kuwa mbunge mara baada ya kushinda uchaguzi mdogo wa Jimbo la Usuk kwa kura 11, 059. Msichana huyu jasiri na asiye na woga amechukua nafasi ya baba yake aliyefariki mapema mwaka huu.

Alengot ni mwanachama wa chama cha NRM (National Resistance Movement) kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni. Wengine waliokuwa wanagombea nafasi hiyo ni pamoja na Charles Ojok Oleny aliyejipatia kura 5,329, Charles Okure kutoka FDC aliyepata kura 2, 725 na Cecilia Anyakoit wa UPC aliyeambulia kura 554.

Honourable Alengot Oromait. Photo used with permission of monitor.co.ug.

Mheshimiwa Alengot Oromait. Picha imetumiwa kwa ruhusa ya monitor.co.ug.

Watu wengi wamejitokeza kumpongeza, wakati wengine wakisema kuwa hataweza kumaliza muhula wake akiwa bungeni kwa sababu ya kuwa na umri mdogo pamoja na kutokuwa na uzoefu wa kutosha. Baadhi ya watu wanaamini kuwa, huu ni mwanzo wa mabadiliko barani Afrika na ni muda wa kuwaondoa viongozi wazee na kuwapa nafasi vijana walipeleke bara la Afrika kwenye mafanikio zaidi.

Pamoja na mambo mengine, Jimbo la mheshimiwa Angelot linakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa maji safi, umeme pamoja na miundo mbinu mibovu ya barabara. Lakini, kwa sasa, watu wa Usuk wameweka matumaini makubwa kwa mbunge huyu aliye na umri wa miaka 19. Ni matumaini kuwa, atakuwa katika nafasi nzuri ya kuliwakilisha jimbo lake na kuliendeleza.

Ramani ya Google ikionesha jimbo la Angelo:

Tazama ramani kubwa zaidi

Baadhi ya raia wa mtandaoni wanatoa maoni yao kama ifuatavyo:

Solar Sister‏ anaamini kuwa, ni wanawake wadogo ambao kwa sasa ndio mihimili ya mabadiliko:

wanawake wadogo wanawezesha mabadiliko! Proscovia Alengot Oromait mwenye umri wa miaka 19 amechaguliwa kuwa mbunge katika bunge la Uganda. http://fb.me/28DoJ2IUr

Joy Doreen Biira amependekeza pawepo na mtu wa kumuelekeza msichana Alomait mambo muhimu ambayo mbunge nayopaswa kujifunza:

@JoyDoreenBiira: Alengot Oromait, msichana wa miaka 19 kwa sasa ni mbunge katika bunge la Uganda….. Vizuri sana. Lakini je yupo yeyote anaweza kumpa “mafunzo ya ziada” kwa mambo muhimu anayopaswa kuyafahamu zaidi?

Akiweka maoni yake kwenye Tovuti ya New Vision, Agambagye Frank anafikiri ni vizuri kuwa amechaguliwa na anaamini hivi ndivyo demokrasia inavyopaswa kuwa:

Ndio maana demokrasia ni nzuri, watu walimchagua

lakodo anashauri kuwa, Mheshimiwa Aromait asimuache rafiki yake wa kiume kwa kuwa tayari ana pesa zaidi na ana nafasi kubwa ya kuwa na rafiki wa kiume tajiri:

Mheshimiwa Prossy , tafadhali, usimsahau rafiki yako wa kiume mwenye umri kama wako wa miaka 19 aliyekuwa akikununulia chapati, na pia aliyekusaidia kufika hapo ulipo, na kumbuka, uwe na moyo shupavu wa kutowaogopa baadhi ya wabunge kama akina Moses Ali wanaovuta pumzi utadhani paa lote la jingo la bunge linataka kuanguka.

Akitoa maoni yake katika habari inayopatika katika tovuti ya Monitor, nkuutu anashauri kuwa mbunge huyu azingatie kwenye masomo kwa kuwa anaweza kupoteza kiti cha ubunge muda wowote, hali itakayomlazimu kutafuta kazi:

nina ushauri kwa mheshimiwa mbunge: Usiogope, kuwa mwenye furaha. Hii inaweza kuwa ni nafasi yako ya kipekee kabisa ya kung’ara! Chaguzi zijazo… nani anajua. Usisahau kazi yako ya kila siku… ninamaanisha masomo yako. Hakuna atakayekupa kazi kwa kuzingatia wasifu kuwa ulikuwa “Mbunge na bila kuzingatia vigezo vya kielimu”. Yeyote anaweza kuwa Mbunge, lakini si kila mmoja amesoma. Hongera sana!

ProWoman anafikiri kuwa, watu wanamchukulia msichana Alengot kama mtoto mdogo. Anaendelea kuwaambia kuwa,wamuache ajitathmini mwenyewe kwa sababu yeye yu mtu mzima:

Proscovia haitaji sana kushauriwa. Jamani mnamchukulia kama vile ni mototo mdogo. Kwa umri wa miaka 19, yeye ni mtu mzima. Mafunzo yalishaanzia nyumbani. Kwa nini kila mtu ana

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.