Mexico: Uandishi Kutoka Gerezani

Enrique Aranda Ochoa siyo mwandishi wako wa Ki-Mexico wa kawaida: Enrique alikamatwa mwaka 1997 na alituhumiwa kwa utekaji nyara, kiasi cha kumpelekea kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka 50. Hata hivyo, kufungwa kwake jela hakujamzuia mwanasaikologia huyu kuendeleza karama aliyonayo ya uandishi.

Enrique ameshatunukiwa zawadi kadhaa za kitaifa za utungaji wa vitabu na hadi sasa ameshaandika vitabu sita vya simulizi. Kwa sasa amejikita sana katika kuelezea zaidi siri za Mayans katika kitabu chake “El fin de los dias” (Nyakati za Mwisho) [es], ambacho kinauzwa mtandaoni [es] katika mfumo wa kielekroniki.

Mwanablogu Gabriela Gutierrez M. kutoka Animal Político [es] anaelezea kazi za mwandishi huyu akiwa jela:

Ávido por conversar, se le agolpan los temas entre las palabras. Puede comenzar hablando del Sol, por ejemplo, y termina hablando sobre Yoga, disciplina que además enseña en el penal. Una charla con él es equivalente a visitar alguna biblioteca, tras la cual uno termina con una lista de bibliografía pendiente por leer. Su última recomendación fue el cubano Joaquín María Machado de Assis.

Ni mwenye hamu ya kuzungumza, mada zinajitokeza wakati wa mazungumzo yake. Anaweza kuanza kuzungumzia Jua kwa mfano, na anaweza kuhitimisha kwa kuiongelea yoga, maarifa ambayo huwa anayafundisha gerezani. Maongezi yake na mtu mwingine ni sawa tu na kama ungefika katika maktaba na kujisomea, ambapo ungeishia kupata idadi kadhaa ya vitabu kwa ajili ya kujisomea. Pendekezo lake la mwisho lilikuwa ni kuhusu raia wa Cuba Joaquin Maria Machado de Assis.

Image via Shutterstock, copyright Steve Snowden

Picha kupitia Shutterstock, haki zote kwa Steve Snowden

Gabriela anaendeleza makala hii ya blogu yake[es] kwa kuziorodhesha tuzo alizowahi kuzipata Enrique kupitia machapisho yake aliyowahi kuyaandika kutokea gerezani:

Desde la cárcel, Enrique Aranda ha sido tres veces Premio Nacional de Poesía “Salvador Díaz Mirón” (1998, 2001 y 2008), otorgado por Conaculta-INBA. También obtuvo dos veces (2003 y 2008) el Premio Nacional de Cuento José Revueltas, otorgado por las mismas instituciones. El reconocimiento más reciente le fue concedido por el INBA en el concurso “México lee 2011”, que se otorga por fomento a la lectura, por el club de lectura que impulso dentro de la cárcel. Fue el Instituto de Cultura de la Ciudad de México, hoy Secretaría de Cultura, quien le proporcionó los cerca de 800 libros: “Cuando les llamé, primero creyeron que era un funcionario. Cuando les dije que era un preso se emocionaron”, dice. La misión con este proyecto era darles a los internos “el boleto para un tour por el anhelado mundo exterior”.

Akiwa gerezani, Enrique Aranda alishatunukiwa mara tatu Tuzo ya Taifa ya Ushairi “Salvador Diaz Miron” (1998, 2001 and 2008) na Conaculta-INBA. Pia, aliwahi kushinda Tuzo ya Taifa ya Hadithi Fupi, aliyotunukiwa mara mbili na asasi hizo (2003 and 2008). Tuzo ya hivi karibuni aliyotunukiwa ilikuwa ni ile ya INBA katika shindano la “Mexico lee 2011″, inayohamasisha watu kusoma, hii inatokana na yeye kuanzisha klabu ya wasoma vitabu huko gerezani. Ilikuwa ni taasisi ya Utamaduni ya Jiji la Mexico ambayo kwa sasa ndiyo Wizara ya Utamaduni, ambayo ilitoa takribani vitabu 800 [kwa ajili ya klabu hiyo]: “Nilipowaita, kwa mara ya kwanza walifikiri ulikuwa wito rasmi. Nilipowaambia kuwa, mimi ni mfungwa, walishikwa na butwaa”, anasema. Lengo haswa la mradi huu lilikuwa ni kuwapa wafungwa wenzangu “fursa ya kuyafahamu yanayoendelea nje ya gereza, jambo walilolitamani kwa muda mrefu”

Tovuti ya jarida ya Ki-Mexico liitwalo Proceso [es] waliandika makala kuhusiana na kesi yake ambapo walielezea namna mashitaka yake yake ya utekaji yalivyokuwa na upungufu:

Enrique sospechó siempre que su detención se debió a sus actividades políticas en distintos foros públicos, por solidarizarse con causas sociales, como la zapatista, y por participar como activista contra el Tratado de Libre Comercio. El caso también fue denunciado por Amnistía Internacional en su informe de 2003: Juicios injustos: tortura en la administración de justicia (Índice AI: AMR 41/007/2003/); el presidente del PEN Club, Eugene Schoulgin, los visitó en 2006; también Lawyer’s Committee for Human Rights los defiende, y la Comisión de Derechos Humanos del Distrito Federal emitió la recomendación 12/02 por tortura y violación a sus garantías jurídicas.

Wakati wote Enrique anahisi kuwa kushitakiwa kwake kulitokana nay eye kujihusisha na mambo ya siasa kwenye majukwaa huru, na tena alionesha mshikamano mkubwa na makundi ya kijamii kama vile zapatista cause, na pia kujihusisha na uanaharakati dhidi ya NAFTA. Jambo hili pia liliwekwa bayana na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International katika taarifa yake ya mwaka 2003: hukumu zisizo za haki: maumivu katika kusimamia haki (AI Index: AMR 41/007/2003/). Raisi wa klabu ya PEN , Eugene Schoulgin, alimtembelea mwaka 2006; na pia jopo la wanasheria wa haki za binadamu wanamtetea, na Tume ya Haki za Binadamu ya Shirikisho ya Wilaya (Jiji la Mexico) ilitoa mapendekezo 12/02 kufuatia uonevu na ukiukwaji wa taratibu wanazozisimamia.

Enrique Aranda Ochoa anafikiria kuihamishia kesi yake katika mahakama ya Amerika inayoshughulikia maswala ya haki za binadamu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.