Italia Yalaumiwa kwa Ukiukaji wa Haki za Wakimbizi wa Kiafrika

Siku ya Februari 23 2012, Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu, mjini Strasbourg, ilifikia uamuzi wa kihistoria. Mahakama hii iliamua kwamba nchi ya Italia ilikiuka sheria za Mkataba wa Ulaya wa Haki za Binadamu ilipowakamata wakimbizi Waeritrea na Wasomali na kuwarudisha Libya.

African Refugees by Vito Manzari on Flickr (CC BY 2.0).

Wakimbizi Waafrika, picha ya Vito Manzari, Flickr (CC BY 2.0).

Blogu ya Unione Diritti Umani inaeleza [it] yaliyotokea:

Il caso Hirsi e altri contro Italia riguarda la prima operazione di respingimento effettuata il 6 maggio 2009, a 35 miglia a sud di Lampedusa, in acque internazionali. Le autorità italiane hanno intercettato una barca con a bordo circa 200 somali ed eritrei, tra cui bambini e donne in stato di gravidanza. Questi migranti sono stati presi a bordo da una imbarcazione italiana, respinti a Tripoli e riconsegnati, contro la loro volontà, alle autorità libiche. Senza essere identificati, ascoltati né preventivamente informati sulla loro reale destinazione. I migranti erano, infatti, convinti di essere diretti verso le coste italiane. 11 cittadini somali e 13 cittadini eritrei, rintracciati e assistiti in Libia dal Consiglio italiano per i rifugiati dopo il loro respingimento, hanno presentato un ricorso contro l’Italia alla Corte Europea, attraverso gli avvocati Anton Giulio Lana e Andrea Saccucci, dell’Unione forense per la tutela dei diritti umani.

Kesi ya Hirsi na wengine dhidi ya nchi ya Italia inahusu operesheni ya kwanza dhidi ya uhamiaji haramu iliyotekelezwa tarehe 6, mwezi wa Mei, 2009 katika ukanda wa bahari ya kimataifa, maili 35 kusini kutoka Lampedusa kwa upande wa kusini. Serikali ya Italia ilisimamisha mashua iliyokuwa ikibeba Wasomali na Waeritrea 200, watoto na wanawake waja wazito wakiwa miongoni mwao. Wahamiaji wakahamishwa kwenye meli ya ki-Italia, na kurejeshwa Tripoli kisha wakakabidhiwa kwa serikali ya Libya kwa nguvu. Hawakutambulishwa, na hakuna aliyewasikiliza wala kuwajulisha walikokuwa wakielekea. Wahamiaji hao hawakutambuliwa, hakuna aliyewasikiliza au kuwajulisha kabla kuhusu walikokuwa wanaelekea. Na kwa kweli, wahamiaji hao waliamini kwamba walikuwa wakielekea kwenye pwani ya Italia. Baada ya operesheni hii, raia wa-Somali 11 na wengine 13 wa Eritrea waliopatikana na kusaidiwa nchini Libya na Baraza la kushughulikia Wakimbizi nchini Italia, walipeleka malalamiko yao dhidi ya Italia mbele ya Mahakama ya Ulaya. Walipata msaidizi kutoka kwa Anton Giulio Lana na Andrea Saccucci wanaotoka katika Chama cha Wanasheria wa Ulinzi wa Haki za Binadamu.

GiulioL [it] alitoa maelezo kuhusu operesheni iliyotokea mara walipowasili Tripoli [it] kwenye blogu ya ilmalpaese:

Sul molo di Tripoli li aspettava la polizia libica, con i camion container pronti a caricarli, come carri bestiame, per poi smistarli nelle varie prigioni del paese. A bordo di quelle motovedette c’era un fotogiornalista, Enrico Dagnino, che ha raccontato la violenza di quell’operazione. Poi fu censura.

Polisi wa Libya walikuwa wakiwangojea kwenye magati, wakiwa na malori yenye kontena, tayari kuwachukua kama mifugo kwenye magari ya kubebea mifugo na kuwawasilisha kwenye magereza kadhaa kote nchini. Maelezo ya mpiga picha na mpashaji habari, Enrico Dagnino, aliyekuwa kwenye mashua ya doria, yalionyesha kwa undani vurugu zilizotokea wakati wa operesheni hii. Baadaye, maelezo kuhusu yaliyotokea yakadhibitiwa.

Henry Oliver anavyoeleza katika blogu ya UK Human Rights, matokeo ya kitendo hiki ni kwamba kanuni zinazosimamia suala la watu wanaotoroka sehemu za hatari hazikutekelezwa:

 Kuwarudisha wale wakimbizi kulivunja Kifungu cha 3 (kinachozuia utesaji na matendo ya kinyama), Kifungu cha 4 katika Ibara ya 4 (kuwafukuza wageni kwa pamoja), na Kifungu cha 13 (haki ya mkimbizi kupata ufumbuzi fanisi). Askari wa doria waliowarudisha wahamiaji nchini Libya waliivunja kanuni inayopiga marufuku kitendo cha kuwarudisha wakimbizi kwenye hatari.

An immigrant's t-shirt saying "I am an immigrant using soap and water" to avoid abuse. By Cristiano Corsini on Flickr (CC BY-NC-SA 2.0).

Tisheti ya mhamiaji isemayo “Miye ni mhamiaji mwenye kutumia sabuni na maji,” lengo lake likiwa kuepukana na dhuluma. Na Cristiano Corsini katika Flickr (CC BY-NC-SA 2.0).

Serikali ya zamani ya Italia, iliyoundwa na chama cha Silvio Berlusconi, Popolo della libertà (Watu wa Uhuru), na chama cha Umberto Bossi cha msimamo mkali wa mrengo wa kulia kiitwacho Northen League, ilijiandaa kisheria na kuchukua hatua dhidi ya uhamiaji nchini Italia. Hatua hizi zimekemewa mara kadhaa na mashirika ya kiraia pamoja na Kanisa Katoliki. Nchi ya Italia pia imelaumiwa mara kadhaa kwa ajili ya sera yake dhidi ya uhamiaji [it] isiyolingana na maafikiano ya Kiulaya.

Blogu ya Gabriele Del Grande, fortresseurope.blogspot.com [it], huchapisha taarifa kuhusu shughuli za ‘Ngome ya Ulaya’ kwa ajili ya utetezi wa haki za wahamiaji. Chama hiki kimetoa ripoti nyingi, shuhuda, na filamu kuhusu wanavyotendewa wakimbizi nchini Italia na katika nchi zingine za Ulaya.

Hapa, anaongea juu ya maisha ya gerezani [it] nchini Libya katika enzi za utawala wa zamani:

Siamo a Misratah, 210 km a est di Tripoli, in Libia. E i detenuti sono tutti richiedenti asilo politico eritrei, arrestati al largo di Lampedusa o nei quartieri degli immigrati a Tripoli. Vittime collaterali della cooperazione italo libica contro l’immigrazione. Sono più di 600 persone, tra cui 58 donne e diversi bambini e neonati. Sono in carcere da più di due anni, ma nessuno di loro è stato processato. Dormono in camere senza finestre di 4 metri per 5, fino a 20 persone, buttati per terra su stuoini e materassini di gommapiuma. Di giorno si riuniscono nel cortile di 20 metri per 20 su cui si affacciano le camere, sotto lo sguardo vigile della polizia. Sono ragazzi tra i 20 e i 30 anni. La loro colpa? Aver tentato di raggiungere l’Europa per chiedere asilo.

Tuko mjini Misratah, umbali wa kilomita 210 mashariki ya Tripoli, nchini Libya. Mahabusu wote hapa watafuta hifadhi, Waeritrea waliokamatwa kwenye bahari karibu na Lampedusa, au katika mitaa ya wahamiaji, mjini Tripoli. Wahanga wa ushirikiano kati ya Italia na Libya dhidi ya uhamiaji. Zaidi ya watu 600, 58 wao wakiwa wanawake, na wengine wengi wakiwa watoto, hata watoto wachanga. Wamekuwa gerezani kwa muda wa zaidi ya miaka miwili, lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyeshtakiwa. Kati yao, watu ishirini hivi hulala kwenye mikeka au magodoro katika vyumba visivyo na madirisha na vyenye vipimo vya mita 4 kwa mita 5. Wao hushinda mchana chini ya ulinzi wa polisi kwenye behewa lenye vipimo vya mita 20 kwa 20. Vyumba vyao viko kando ya behewa hili. Wote wana umri kati ya miaka 20 na 30. Na ni uhalifu upi walioutenda? Walijaribu kufika Ulaya ili watafute hifadhi.

Blogu ya observatoirecitoyen.over-blog.org inafunua [fr] kuwa:

Le principe de non refoulement, inscrit dans la Convention des Nations unies sur le statut des réfugiés de 1951, interdit de renvoyer une personne vers un pays où sa vie ou sa liberté peut être menacée. …

Quelque 602 migrants ont été interceptés en mer et immédiatement refoulés de mai à juillet 2009, principalement vers la Libye, un pays où “toute personne détenue risque d'être soumise à des mauvais traitements sérieux” ou d'être renvoyée vers un pays où existent de tels risques, note le CPT (Comité de prévention de la torture).

Certes, reconnaît-il, “les Etats ont le droit souverain de protéger leurs frontières et de contrôler l'immigration”, mais l'Italie doit revoir ses procédures pour s'assurer que tous les migrants interceptés reçoivent d'abord des soins et puissent déposer une demande d'asile.

Kanuni inayopiga marufuku kitendo cha kuwarudisha wakimbizi kwenye hatari, iliyoridhiwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa Unaohusu Hadhi ya Wakimbizi mnamo mwaka wa 1951, huzuia kitendo cha kumrudisha mtu kwenye nchi ambapo maisha yake au uhuru wake unaweza kuwa hatarini. …

Kuanzia mwezi Mei hadi mwezi Julai 2009, wahamiaji 602 walisimamishwa baharini na papo kwa hapo wakakatazwa kuendelea. Wakarejeshwa nchini Libya hasa, ambapo “kila mtu anayekamatwa anakuwa katika hatari ya kufanyiwa vitendo vikali vya kikatili, ” au kurejeshwa kwenye nchi ambapo hatari za aina hii zipo, KKM (Kamati cha Kuzuia Mateso) ilisema.

Kwa hakika, KKM inakiri, “Nchi zina haki ya kulinda mipaka yao na kudhibiti uhamiaji,” lakini Italia inapaswa kupitia taratibu zake kuhakikisha kwamba wahamiaji wote wanaosimamishwa watapewa huduma kwanza,  kisha kuruhusiwa kuomba hifadhi.

Bahati mbaya barani Ulaya, Italia si nchi pekee kuwarudisha watu wengi kwa mara moja katika nchi walizotoka. Chama hiki cha kutetea wakimbizi kinaarifu [it] kwamba:

Dal 1988 sono morte lungo le frontiere dell'Europa almeno 18.058 persone. Di cui 2.251 soltanto dall'inizio del 2011. Il dato è aggiornato al 7 dicembre 2011 e si basa sulle notizie censite negli archivi della stampa internazionale degli ultimi 23 anni. Il dato reale potrebbe essere molto più grande. Nessuno sa quanti siano i naufragi di cui non abbiamo mai avuto notizia. Lo sanno soltanto le famiglie dei dispersi, che dal Marocco allo Sri Lanka, si chiedono da anni che fine abbiano fatto i loro figli partiti un bel giorno per l'Europa e mai più tornati.

Tangu mwaka 1988, watu wasiopungua 18,058 [it] wamepoteza maisha yao katika mipaka ya Ulaya. 2,251 wao wamefariki tangu mwanzo wa 2011. 2,251 wao wamefariki tangu mwanzo wa 2011.Takwimu hizi zilihuishwa Desemba 7, 2011, na zilizotokana na sensa iliyofanywa na kumbukumbu ya vyombo habari vya kimataifa kwa zaidi ya miaka 23 iliyopita. Takwimu halisi zaweza kuwa kubwa zaidi. Hakuna anayefahamu ni meli ngapi zilizozuiliwa kwa maana hatujawahi kusikia. Familia za waliopotea pekee ndizo zinazofahamu. Familia hizi, kutoka Moroko mpaka Sri Lanka, zimekuwa zikiuliza kwa miaka mingi ni kipi kilichotokea wanao walipoondoka siku moja kwenda Ulaya na kutowahi kurudi tena.

Paolo Lambruschi, kwa upande wake, aliandika [it] katika tovuti ya gazeti la Kongamano la Kiaskofu la Kiitalia:

E, cosa che interessa tutta l’Ue, andranno riviste le operazioni Frontex di pattugliamento del Mediterraneo perché per la prima volta viene equiparato il respingimento di gruppi alla frontiera e in alto mare allé espulsioni collettive. A 22 ricorrenti su 24, 11 somali e 13 eritrei, l’Italia dovrà versare un risarcimento di 15 mila euro più le spese processuali. Gli altri due sono morti.

Na kuna jambo linalozihusu nchi zote za Ulaya: Operesheni za doria za Frontex katika Bahari ya Mediterania zitarekebishwa kwa sababu, kwa mara ya kwanza, kurudishwa kwa makundi ya watu yakiwa mipakani na katika vilindi vya bahari ni sawa na kuwarudisha watu kwa nguvu. Itabidi Italia iwalipe Euro 15,000 pamoja na gharama za kisheria wadai 22 kati ya 24: Wasomali 11 na Waeritrea 13. Wengine wawili wamefariki.

Blogu ya Gabriele Del Grande ya fortresseurope.blogspot.com inahitimisha [it]:

Un giorno a Lampedusa e a Zuwarah, a Evros e a Samos, a Las Palmas e a Motril saranno eretti dei sacrari con i nomi delle vittime di questi anni di repressione della libertà di movimento. E ai nostri nipoti non potremo neanche dire che non lo sapevamo. Di seguito la rassegna completa e aggiornata delle notizie, dal 1988 a oggi. Per un'analisi delle statistiche, frontiera per frontiera, leggete la scheda Fortezza Europa.

Siku moja, huko Lampedusa na Zouara, huko Samos na Evros, au huko Las Palmas na Motril, maziara yataundwa yenye majina ya wateswa wa miaka hii ya ukandamizaji wa uhuru wa uhamiaji. Na hatutaweza kuwaambia wajukuu wetu kwamba hatukujua. Hapa, unaweza kupata uwasilishaji pambanuzi na taarifa mpya, tangu mwaka wa 1988 mpaka hivi leo. Kuona uchambuzi wa takwimu hizi, mpaka kwa mpaka, soma ramani Fortezza Europa (Ngome ya Ulaya).

3 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.