Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Septemba, 2012
Pakistani: Msichana wa Kikristo wa Miaka 11 Awekwa Kizuizini kwa Kukashifu Dini.
Rimsha Masih msichana Mkristo mwenye umri wa miaka 11 ametuhumiwa kwa makosa ya kukashifu na ameshikiliwa kwa siku kumi na nne katika gereza za watoto huko Rawalpindi, nchini Pakistani. Anashitakiwa kwa kuchoma kurasa za kitabu cha Noorani Qaida, kinachotumika kwa wanafunzi wa lugha ya kiarabu, na kuziweka katika mfuko wa 'rambo'.
Palestina: Maandamano Yalipuka Kupinga Ongezeko la Bei za Bidhaa na Ukosefu wa Ajira
Maandamano yanashika kasi katika mipaka ya Palestina, hasa katika miji mikuu katika Ukanda wa Magharibi. Waandamanaji wanalalamikia kupanda sana kwa gharama za maisha na ukosefu mkubwa wa ajira miongoni mwa vijana wa kipalestina.
Global Voices Yashinda Tuzo Ya Highway Africa
Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba,...