Wizara ya Umoja wa maendeleo ya wanawake na Watoto nchini India inaufikiria mswada ambao kama utapitishwa na bunge utahalalisha ulazima wa waume kumega sehemu ya mishahara yao na kuwalipa wake wasio na ajira kama ujira kwa kazi za nyumbani wanazozifanya.
Kwa mujibu wa pendekezo hilo la wizara, mswada huo unaandaliwa kiasi kwamba utaruhusu kupima kiwango cha kazi iliyofanywa na akina mama wa nyumbani kwa mtizamo wa makubaliano ya kiuchumi na kutambua mchango huu katika uchumi kwa kuwafidia akina mama hawa wa nyumbani kulingana na kazi wanazozifanya.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyakazi wa ndani wanachukuliwa kama “ wahandisi wa kazi za nyumbani “. Waziri Krishna Tirath alisema kuwa, kiasi hiki ambacho kinakadiriwa kati ya asilimia 10-20% ya mshahara wa mwezi wa mume, haipaswi kuchukuliwa kama mshahara kwa ajili ya kazi za nyumbani, bali unapaswa kuchukuliwa kama jambo la kuonesha heshima au jambo linalofanana na hilo.
Wakati waziri akiliona jambo hili kama hatua kubwa iliyopigwa kuhusiana na na wanawake kuwezeshwa, mswada huu wa sheria unajadiliwa vikali, nje ya mtandao wa intaneti na hata kwenye mitandao ya intaneti.
Baadhi ya watu wanahisi kuwa ” kupima thamani ya kazi za nyumbani zisizo za malipo kimantiki ni sahihi na ni jambo linalowezekana kujadiliwa, pamoja na kuwa, kulifanya jambo hili kuwa la lazima kwa waume kuwalipa wake zao asilimia fulani ya fedha za ujira wao kama njia ya kufidia kazi wanazozifanya wake zao nyumbani, kwa baadae linaweza kuwa si jambo zuri.
Wengine wanashangaa kuwa itawezekanaje kuweka kiwango sahihi cha fedha kwa kazi zote zinazofanyika majumbani na namna ambavyo sheria hiyo itakavyofanya kazi- huku maswali mengi yakitazamiwa kuulizwa kufuatia mswada huu wa sheria.
Na kwa hakika, maswali yanaulizwa. Kwa mfano, LordRaj anauliza:
Kwa hiyo unapendekeza uhusiano wa mwajiriwa/mwajiri kwa wanandoa?
div> Ni nani atakayehusika na kuweka masaa ya kazi na taratibu za kazi?Katika jarida la habari nyepesi nyepesi (Ground Report) ambalo ni jarida huru la habari, D. Chaitanya anaainisha zaidi baadhi ya maswali yanayohusiana na jambo hili ambayo watu (wanaume kwa wanawake) wamekuwa wakiyajadili kwa undani. Kwa mfano:
- Kama katika nafasi ya mke, mfanyakazi wa ndani anafanya kazi zote za ndani, mfanyakazi huyu wa ndani atachukuliwaje? Haipaswi mfanyakazi wa ndani kuangaliwa sawa na mke? (Kwa mtazamo huu) ni nani mwenye haki ya kupewa hiki cha asilimia 10 au 20?
- Kama kiasi hiki cha asilimia 10 au 20 cha fedha kitawekwa kwenye akaunti kwa jina la mke, vipi kuhusu mahitaji muhimu ya mke? Itakuwaje kama mke atamtelekeza Mume na kisha kumfungulia mashitaka ya kushishwa kutoa huduma za muhimu
- Je sheria hii italeta malumbano ya mapato kati ya wake na waume zao? Kama vile sheria namba 498-A ya hukumu, sheria za kulipana mirathi, sheria za migogoro ya kifamilia. Je, hata na sheria hii itatumiwa vibaya na baadhi ya wake?
Mwanablogu Surya Murali naye anashangaa jinsi serikali inavyopendekeza utekelezaji wa sheria kama hii. Katika blogu yake anasema:
Ninakubaliana na swala la kuwawezesha wanawake, pia na uhuru wao katika masuala ya kiuchumi…… lakini swali langu kubwa hapa kwa hawa watungaji wa sheria ni kuwa, ni kwa namna gani wataweza kuutekeleza mswada huu wa sheria? Kama bado wataendelea kuwa na msimamo wa kuwa mme lazima atoe asilimia kadhaa ya mshahara wake kwa mke wake kulingana na kazi za nyumbani anazozifanya, sioni ni kwa namna gani hali ya kiuchumi ya familia itakavyoboreshwa au ni kwa namna gani itamfanya mwanamke ajitegemee na kuwezeshwa. Pato la taifa linabaki pale pale na hali ya kiuchumi ya familia haibadiliki. Waume wanaowajibika moja kwa moja kwa wake zao, kwa kadiri ya ninavyoamini, wangeshirikiana na wake zao gharama za mahitaji muhimu ya familia bila shaka…. Kama hii si hoja, basi utaratibu huu hautaweza kuboresha usawazo wa kimahusiano kati ya Mume na Mke kuhusiana na mambo mbalimbali ya familia.
Katika iDiva, Archana Jayakumar anauliza:
Ni kwa vipi mambo yote haya hayatamfanya kuwa lolote bali mbarikiwa wa utumwa?
Sunit katika Supari.org anakubali na kuuita mswada huu uliopendekezwa kama “ mkakati wa kuharibu familia ” unaofanywa na serikali. Mwanablogu LordRaj anahitimisha kuwa:
Kufuatia mtazamo wa ‘maendeleo na ustawi’ wa wanawake, yote mliyokuwa mnayafanya ni kuonesha kuegemea katika upendeleo dhidi ya wanaume.
Makundi ya haki za wanaume yanaelekea kukubali. Vicky Nanjappa anafafanua:
Mswada wa kuruhusu sehemu ya mshahara wa Mme kupewa Mke umepingwa vikali na makundi ya haki za wanaume. ‘Asasi ya kusaidia familia’ imeshamwandikia barua waziri wa ushirikiano wa Maendeleo ya Wanawake na Watoto wakitaka mswada huo uondolewe mapema iwezekanavyo. Asasi hii inayojumuis