· Oktoba, 2012

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Oktoba, 2012

Misri: Ushauri kwa Waandamanaji wa Kuwait

Wakati watu wa Kuwait walipoanzisha maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kutokea ya kuonesha waziwazi kutokukubaliana na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaliyopitishwa chini ya mtawala wa kurithi kufuatia kuvunjwa kwa bunge, watu wa Misri wametumia muda wao mwingi katika Twita wakitoa ushauri kwa watu wa Kuwait kuhusiana na yapi ya kufanya na yapi ya kutokufanya.

‘Mazungumzo ya Kitaifa’ Nchini Singapore Yatafanikiwa?

  27 Oktoba 2012

Katika juhudi za kupangilia mustakabali wa Singapore, serikali imezindua “mazungumzo ya kitaifa” yatakayodumu kwa mwaka mmoja ili kukusanya maoni ya watu. Baadhi ya wananchi wameupokea mpango huo kwa mikono miwili lakini pia wapo wengine wanaoupinga wakiuona kama mbinu tu ya kujiweka karibu na wananchi.

Kuwait: Ni Maandamano Makubwa Kabisa Kuwahi Kutokea?

Mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ya kumfanya mtu kupoteza fahamu yalitumika kutawanya maandamano ya kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi nchini Kuwait. Maandamano hayo yaliyofanyika siku ya Jumapili, na kuratibiwa kupitia katika mtandao wa Twita na yaliyowavutia takribani watu 150,000 kati ya watu milioni 3 ambao ndio idadi ya watu wa Kuwait. Taarifa za vyombo vya habari zinaichukulia idadi hii kuwa ni kubwa kabisa katika historia ya Falme za ghuba ndogo.

Kambodia Yaomboleza Kifo cha Mfalme Norodom Sihanouk

  27 Oktoba 2012

Nchi ya Kambodia inaomboleza kifo cha baba Mfalme Norodom Sihanouk aliyefariki tarehe15 Ockoba, 2012. Mamilio ya watu walisubiri pembezoni mwa barabara itokayo uwanja wa ndege kwenye kwenye makazi ya kifalme kutoa heshima zao za mwisho kwa Mfalme.

India: Mgogoro wa Mtambo wa Nyuklia wa Kudankulam Waendelea.

  22 Oktoba 2012

Mradi wa Nguvu za Nyuklia mjini Koodankulam katika wilaya ya Tirunelveli iliyo katika Jimbo la kusini la Tamil Nadu nchini India umeanza kufanya kazi mwezi uliopita lakini maandamano ya kuupinga mradi huo umeendelea na kamata kamata inasababisha waandamanaji kuishia jela. Juma hili limeshuhudia maandamano yakienea India yote kwa ushirikiano na watu wanaopinga matumizi ya Mtambo wa Nyuklia.

Ghana: Vikwazo Vinavyowakabili Wanawake Kimaendeleo

  16 Oktoba 2012

Betty Mould Iddrisu, Jaji na Waziri wa Sheria wa Ghana, anaandika [fr] kwenye blogu ya pambazuka.org: Kufikia ngazi za juu kabisa za utawala si rahisi, na hata unapopanda mpaka juu kabisa, bado unajikuta unakabiliwa na hisia za watu zenye uadui na watu wanakuwa na mashaka na uwezo wako, kwa sababu...

Venezuela: Tathmini za Baada ya Uchaguzi

  15 Oktoba 2012

Msisimko ulikuwa mkubwa sana usiku wa siku ya Jumapili baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi wa Rais wa Venezuela kutangazwa. Sehemu ya nchi ilisherehekea kuendelezwa kwa 'Mapinduzi ya Venezuela' chini ya Rais Hugo Chávez, wakati upande mwingine ulilalamika kwa kushindwa tena kwenye uchaguzi huo.

Zambia: Filamu yaYouTube Kuhusu Athari za Machimbo ya Madini

Filamu ya Uchunguzi yenye jina "Zambia: Shaba Nzuri, Shaba Mbaya" inayohusu machimbo ya shaba nchini Zambia na athari zake kwa jamii imewekwa kwenye mtandao wa YouTube na mpaka sasa imevuta watazamaji zaidi ya 6,000. Baada ya kuitazama filamu hiyo, mtumiaji mmoja wa mtandao wa YouTube aliandika, "Jililie eeh nchi yangu nzuriKwa nini tubaki masikini katikati ya utajiri huu wa madini yanayochimbwa kwa gharama ya afya za wenyeji?"