‘Mazungumzo ya Kitaifa’ Nchini Singapore Yatafanikiwa?

Katika juhudi za kuwahusisha wananchi wa tabaka la chini katika kupangilia mustakabali wa Singapore, serikali ya nchi hiyo imezindua “mazungumzo ya kitaifa” yatakayodumu kwa mwaka mmoja ili kukusanya maoni ya watu.

Ikiongozwa na kamati yetu ya Singapore, mazungumzo hayo ya kitaifa yatafanyikia mtandaoni na pia kwa njia ya mahojiano kadhaa na mikutano. Mazungumzo hayo ya Singapore tayari yanapatikana katika tovuti na pia ukurasa wa Facebook, na yanawataka watu watoe maoni yao katika mtandao wa twita kwa kutumia kiungo habari cha #oursgconv.

Zoezi hili limeshapokewa vizuri na baadhi ya watu wa Singapore. Petunia Lee anaandika kuhusiana na uzoefu wake wa kuhudhuria katika vipindi vya mazungumzo:

Kutoka katika ukurasa wa facebook wa mazungumzo yetu ya SG

Napaswa kusema kuwa, uzoefu wangu katika mazungumzo ya SG ulifungua macho yangu kwa wananchi wenzangu wa Singapore. Jambo la kwanza, sikuweza kutambua namna wazee wa Singapore walivyojisikia kwa kunyimwa haki ya kumiliki na kutengwa hadi pale mzee mmoja mchangamfu kutoka katika kikundi changu alipotoa maoni yake. Jambo jingine ni kuwa, nilikuwa na mtizamo hasi kuwa mahusiano ya amani kati ya watu wa rangi tofauti ni sehemu ya maisha yetu kiasi kwamba hatuhitaji kulifuatilia kabisa. Alikuwa ni daktari mwanadada mtu wa Malaysia ambaye katika hotuba yake iliyojaa hamasa alinishawishi kuwa mahusiano kati ya watu wa rangi tofauti yanaweza kuleta madhara leo kama ilivyotokea katika miaka ya 1960.

Ndiyo…. nafikiri kwamba, kama jinsi ilivyoelezwa na ndugu Tan, dhumuni la mazungumzo ya SG ni kutufundisha ukweli fulani kuhusu nchi yetu, na kwangu mimi, lengo hili lilitimia.

Hata hivyo, wapo watu wengi wanaotilia mashaka zoezi hili, wakiona kuwa si chochote zaidi ya jitihada za mahusiano ya umma. Molly Meek anaamini kuwa mazungumzo yote ya kitaifa ni hila tu za kubadilisha taswira ya chama tawala:

Mbinu ya chama tawala (PAP) ni yenye kutumia akili sana—mtu anaweza kujiuliza kama waliwasiliana na wataalamu kuhusiana na jambo hili kabla ya kuendelea na juhudi zao hizi- mtu hawezi kusaidiwa bali kuridhishwa kwa mafanikio yao yanayopimika. Mbinu iliyotumika kwa hakina ni rahisi— imelenga raia wachache ikiwa ni pamoja na watu maarufu na wale wanaojulikana kidogo tu na kwa wastani, wale wanaokipinga chama tawala cha PAP, wakiwapa mawazo tofauti na kuwaacha wakisambaza taarifa kuwa chama tawala cha PAP sio kweli kuwa ndio wanaokikashifu. Kwa hakika, mambo haya hayapaswi kuwa na maana yoyote, ni maneno matupu kwa chama cha PAP ambacho kinawaacha wakiwa hawana chochote cha kupinga itakuwa ni njia muafaka sana kwa wengine ambao bado wanaweza kushawishika kukiunga mkono chama cha PAP.

Mhariri katika gazeti la publichouse.sg anafafanua kuwa mazungumzo haya yanaweza yasiishie kwenye mabadiliko ya kweli:

Hata kama itafikiriwa kuwa mawaziri wanaoratibu mkakati huu wa sasa wanafanya udanganyifu makini wa wazi, waangalizi wa zamani katika baraza la mawaziri bado wanaweza kupiga kura ya turufu kuhusiana na matokeo ya mpango huo. Inaelekezwa kuwa, mengi ya mapendekezo huru na yaliyo makini yaliyoandaliwa na kamati teule ya Singapore- kama yale ya serikali kuweka bayana waundaji wasio na mipaka ya midahalo ya kisiasa, uanzishwaji wa mpango wa kuwasaidia kiuchumi watu wasio na ajira pamoja na kupunguza gharama za bidhaa kwa makundi ya watu wa kipato cha chini hayakutiliwa maanani.

‘jiunge na tovuti ya mazungumzo ya Singapore’


Howard Lee, anayeliandikia gazeti la The Online Citizen, alitoa maoni kwa mfuasi wa chama anayedhaniwa kupendelewa katika mazungumzo hayo:

Hatutaki kuona mazungumzo yanayotawaliwa na watu wanaoonekana kuvumilia utendaji wa chama tawala katika mambo ya kitaifa, na ambao ndio wanaosadikiwa kuwa sehemu ya mwangwi wa kale wa chumba cha siri cha majaji. Tungewezaje kufikiria yajayo kama ndivyo?

Kwa maneno mengine, Wong na wengine kama yeye wanatakiwa kutambua kuwa mpira kwa sasa upo katika mipaka ya chama tawala cha PAP ili kuthibitisha kuwa wanaweza wsiwe wafuasi wa chama, bali ni watu wanaokipinga chama kwa nguvu zote na ambao wanaipeperusha bendera nyekundu kwa ushirikiano wao wakiwa kama watu waliofundishwa siasa. Kuthibitisha kupo kwenye matendo na si kwa maneno.

Tunahitaji sauti kutoka sehemu tofauti tofauti, hata wale wapinzani walio mbali kabisa ya wigo wa mantiki na wasio na manufaa, wahusishwe kwa kila jambo na wahamasishe midahalo kwa moyo na kama sio kwa kuguswa, kuliko kujenga muafaka mwingine wa kuonesha na kusema. Na watu wa Singapore wana haki ya kutegemea mazungumzo ya kitaifa kuwa namna hiyo.

Wakati mazungumzo yanaendelea katika vikao vya maongezi na katika facebook, kiungo habari cha Twita, #oursgconv kinaonekana kuingiliwa bila idhini na jumbe za watu wanaopinga mpango huu:

@SGSilentMaj : Uhuru wa kutoa maoni ni mbaya kwa #Singapore #sgpolitics #sgelections http://bit.ly/REUBsd http://bit.ly/TJjDZX

@SGLaoBaiXing : WP wanajinufaisha kupitia kazi ya PAP #sgpolitics #sgelections http://bit.ly/TcBoTM http://bit.ly/R4RV9G

@theonlinesg : WP hawana maono#sgpolitics #sgelections #oursgconv http://bit.ly/T1qhqo http://bit.ly/RWyvlo

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.