Venezuela: Tathmini za Baada ya Uchaguzi

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Uchaguzi wa Venezuela 2012.

Palikuwa na msimuko mkubwa siku ya Jumapili baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi yauchaguzi wa Rais tarehe 7 Oktoba, 2012. Rais Hugo Chávez alichaguliwa kwa mara nyingine kwa asilimia 55.14 ya kura, wakati mgombea wa upinzani,Henrique Capriles, akipata asilimia 44.24, kwa mujibu wa Baraza la Uchaguzi la Nchi hiyo[es].

Sehemu ya nchi hiyo ilisherehekea mwendelezo wa Mapinduzi ya Bolivia” chini ya Chávez, wakati upande mwingine ukilalamikia kupoteza uchaguzi kwa mara nyingine.

Wafuasi wa Chávez wakitathmini

Tamara Pearson katika blogu ya Venezuelan Analysis anayarejea matokeo hayo ya Jumapili kama “ushindi usiokamilika”. Anaandika kwmaba pamoja na hisia za kusherehekea ushindi walizonazo wafuasi wa Chavez usiku wa Jumapili, alionekana “mnyonge kidogo”:

kwa sababu zaidi ya watu milioni sita walimwunga mkono, kwa kumpigia kura Capriles, ubinafsi (alielekeza kampeni zake kwa kuitaka nchi hiyo kuachana na ushirikiano na nchi nyingine) na uharibifu na kuuzwa kwa nchi yao.

Anaendelea zaidi kwa kuchambua kwa nini tofauti ya kura kati ya upizani na Chavez inaendelea kupungua. Kwa mtazamo wake, “upinzani umetoka kwenye uchaguzi huu ukiwa na nguvu mpya” kwa hiyo “mapinduzi hayatabaki bila tahayari”:

Kama hatutaushinda ufisadi na urasimu katika kipindi kijacho, tunaweza kuyapoteza mapinduzi haya. Sasa wakati uchaguzi wa Rais umemalizika, tunayo maswali mawili makubwa: Tutaimarishaje mapinduzi, na je yataendelea kuwepo?

Supporters of President Hugo Chavez during the presidential elections on October 7, 2012. Photo by Alejandro Rustom. Copyright Demotix.

Wafuasi wa Rais Hugo Chavez wakati uchaguzi wa rais tarehe 7 Oktoba, 2012. Picha ya Alejandro Rustom. Haki miliki Demotix.

Antonio Aponte, wa blogu ya Un Grano de Maíz [es], anawapongeza wafuasi wenzake wa Chávez kwa ushindi huo, lakini vile vile anatazama changamoto za mbeleni zinazoyakabili Mapinduzi ya Venezuela. Anachambua pia kupungua kwa tofauti ya kura baina ya wafuasi wa serikali na wale wa upinzani:

[…] de un 26% de diferencia en las elecciones presidenciales del 2006 pasamos a un lánguido 10%.  Perdimos casi 20% de nuestra votación, los análisis preliminares indican que los perdimos en los sectores pobres y sin aumentar la votación en los sectores de clase media.

¿Por qué la mengua? La respuesta reside en la esencia del Socialismo, sin comprenderla estamos destinados al fracaso: el Socialismo tiene como esencia al amor, a la relación fraterna, al sentido de pertenencia a la sociedad. El capitalismo tiene como esencia al egoísmo, a las soluciones individuales. Ese es el fundamento de la batalla, el egoísmo enfrentado en feroz lucha contra el amor, y hacia allí deben ir dirigidos nuestros esfuerzos.

[…] kutoka tofauti ya asilimia 26 katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2006 sasa tumefikia katika tofauti ndogo ya asilimia 10. Tumepoteza takribani asilimia 20 ya kura zetu. Uchambuzi wa awali unaonyesha kwamba tumepoteza katika sekta za watu wenye kipato kidogo na wala hatukujiongozea kura kutoka katika sekta za tabaka la kati.

Kwa nini kura zimepungua? Jawabu liko kwenye umuhimu wa ujamaa, bila kuuelewa sisi ni wa kushindwa: Ujamaa ni msingi wa upendo, mahusiano ya kindugu, hisia za kuwa sehemu ya jamii. Ubepari msingi wake ni ubinafsi, majawabu binafsi. Huo ndio msingi wa mapigano, ubinafsi katika mapigano dhidi ya upendo, na kwamba hapo ndipo juhudi zatu zapaswa kuelekezwa.

Anahitimisha kwamba “wanamapinduzi” lazima wajijengee ‘utamaduni wa mijadala': “Mapinduzi ambayo hayajadili, hufa”:

El estudio, la discusión, deben ser las tareas principales de la sociedad. La ignorancia es contrarrevolucionaria. ¡Viva Chávez!

Kusoma, kujadili, lazima viwe ndiyo majumu makuu ya jamii. Ujinga ni kizuizi cha mapinduzi. Uishi maisha marefu Chávez!

Tathmini za wapinzani

Wanablogu wengi wa upinzani walifuatilia kwa karibu kampeni za Capriles, kwa hamasa ya kile kilichoonekana kuwa wakati muafaka wa mabadiliko nchini Venezuela. Waliotoa maoni yao pindi tu matokeo yalipotangwa, wakiambizana namna wanavyojisikia huzuni na fadhaa, lakini vilevile wakitazama mbele kwa jicho la kujikosoa.

Mwanablogu Alex Boyd anasema “hajawahi kutegemea matokeo tofauti”. Anaweka ramani ya matokeo na kuongeza dokezo la wizi wa kura:

Hugo Chavez amemwangusha mgombea wa upinzani kwa mara nyingine. Miaka sita sasa, Chavez bado ni chaguo la raia walio wengi. Na hiyo ni sawa, sina tatizo na hilo. Uzuri wa hayo ni kwamba Henrique Capriles, Leopoldo Lopez, Ramon Guillermo Aveledo na wengine walilizika jinamizi la wizi wa kura nchini Venezuela. Kwa kudai, mara kwa mara, kwamba mfumo ulikuwa umekaguliwa vya kutosha, na kwamba upinzani umeweza kuweka waangalizi katika asilimia 100 ya vituo vya upigaji kura, hakuna ten nafasi ya kuendekeza wazo la wizi wa kura.

Manuel Silva wa blogu ya No solo con la palabra [es] anadhani moja ya mambo mabaya kabisa ambayo upinzani umeyafanya katika michakato ya chaguzi hizi ni kutokuwa na maandalizi ya kushindwa. Hata hivyo, Silva anahoji kwamba kushindwa kwa upinzani si kushindwa kwa siasa:

Aquí se perdió porque […] la mayoría de los venezolanos se identifica con esta forma de gobernar. Nosotros estamos dispuestos a aceptar el abuso y el atropello como forma de vida, naturalizamos la inseguridad, nos conformamos con la miseria, aceptamos gustosos vivir como lo hemos hecho en los últimos años: odiándonos.

Hapa tumeshindwa kwa sababu […] wengi wa wa-Venezuela wanajitambulisha kwa serikali ya namna hii [Chávez]. Tuko tayari kukubali kutukanwa na kufanyiwa dhihaka kama sehemu ya maisha, tumefanya kutokuwa na usalama kuwa kitu cha kawaida, tumeridhika na ufukara, tumekubali kuishi kwa furaha kama tulivyofanya katika miaka ya hivi karibuni: tukichukiana.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa mwanablogu Mirelis Morales Tovar wa Caracas Ciudad de la Furia [es], upinzani haujajifunza vya kutosha:

hay muchos que deben mirar un poco más allá. Venezuela no es Caracas, no es La Lagunita ni mucho menos Twitter. Somos un país divido en partes iguales y debemos aprender a mirar el otro lado.

Kuna wengi wanaohitaji kuangalia kwa kina zaidi. Venezuela sio Caracas, si La Lagunita wala mtandao wa Twita. Sisi ni nchi iliyogawanywa katika sehemu zilizo sawa na ni lazima tujifunze kutazama upande wa pili.

Alejandro Tarre [es] anahoji kwamba upinzani lazima uwe tayari na ukubali kuendelea kuonyesha mbadala kwa wa-Venezuela, wakizingatia kwamba “siasa, kama yalivyo maisha, inabadilika ” na kwamba mwezi Desemba wananchi watapiga kura kuwachagua mameya na magavana:

La masa opositora está ahí; el reto es simplemente sacudirla hasta sacarla del estupor en el que se encuentra para luego movilizarla. Se ha dicho mucho que, después de su estupenda campaña, Capriles está en una posición ideal para asumir el liderazgo opositor y blindar la unidad. Pues bien, ahí tiene su primer reto. Ahora más que nunca necesitamos a nuestro rock star animando a la gente y recorriendo el país para apoyar a los candidatos a alcaldes y gobernadores.

Umma wa wapinzani upo, changamoto ni namna ya kuwafanya wafuasi wake waelewe mambo ili wawezi kuwashawishi. Mengi yamesemwa kwamba, baada ya kampeni hii kubwa, Capriles anaweza kuongoza vyema upinzani na kuongoza mshikamano. Hii ni changamoto yake ya kwanza. Sasa tunahitaji nyota huyo wa muziki kuwatia moyo watu na kuzunguka nchi nzima kuwaunga mkono wagombea wa umeya na ugavana.

Haya ni mawazo machache sana ya upande wa upinzani baada ya uchaguzi unaotajwa kuwa na ushindani mkubwa sana katika miaka mingi. Miitikio mingine iko kwenye mtandao wa twita, jukwaa la vyombo vya kiraia linalotumiwa zaidi na wana Venezuela wengi watumiao mtandao.

POsti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Uchaguzi wa Venezuela 2012.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.