India: Mgogoro wa Mtambo wa Nyuklia wa Kudankulam Waendelea.

Mradi wa Nguvu ya Atomiki wa Koodankulam katika wilaya ya Tirunelveli iliyoko katika jimbo la India ya Kaskazini lijulikanalo kama Tamil Nadu, tangu mwezi uliopita walikwisha anzisha maandamano miongoni mwao. (tazama taarifa za Mtandao wa Sauti za Dunia). Mtambo huu umeshaanza kuzalisha umeme lakini hali inaendelea kuwa mbaya kwani watu wanaendelea kuwekwa kizuizini na waandamanaji wanaendelea kushikiliwa magerezani. Wiki hii pia ni mwanzo wa maandamano ya wiki mbili katika maeneo yote ya India kwa ushirikiano na watu wenye kupinga matumizi ya Mitambo ya Nyuklia.

Mapema Jumapili ya tarehe 14 Oktoba, Chama cha RDF (Revolutionary Democratic Front) kilitoa tamko linalolaani watu kushikiliwa na kuwekwa kizuizini kwa wanachama wote wa India wanaojaribu kuutafuta ukweli kuhusu mtambo wa nyuklia wa Koodankulam ulio katika jimbo la Tamil Nadu. Kundi hilo lilishikiliwa huko Nanguneri mnamo tarehe 12 Oktoba, kilomita 20 kutoka Koodankulam kwa mashitaka ya kuitisha “mikutano isiyo ya halali”. Baada ya kuzuiwa kwa takribani siku nzima, polisi waliwahukumu kwa kutumia vifungu tofauti tofauti vya sheria ya marekebisho ya makosa ya jinai. Wanakikundi hao hao wamepelekwa katika mahabusu ya Palayamkottai.

Kwa mujibu wa Sanhati:

“Watu wa Koodankulam wamekuwa wakipinga mitambo ya nyuklia kwa ustadi mkubwa uliojengwa katika makazi yao na kusababisha uonevu kwa miezi kadhaa sasa. Badala ya serikali kusikiliza matakwa yao na kuzingatia suala la kutokuwa na hali nzuri ya ulinzi pamoja na madhara ya uharibifu wa mazingira unaotokana na mitambo hii ya Nyuklia. serikali imewajibu waandamanaji kwa kutumia njia ya ukandamizaji wa kikatili kabisa. Jaribio la serikali la kuzuia na kulikandamiza kundi hili linalojaribu kuutafuta ukweli inaonesha kwa uwazi kabisa kuwa serikali haitaki watu wazungumzie wala kufahamu hali ilivyo huko Koodankulam au kuhusiana na juhudi ambazo watu wanazoziweka na mambo wanayoyapigania. Serikali inachokifanya ni kujaribu kuwaogopesha watu pamoja na kujaribu kuua sauti za mshikamano wa watu wanaowaunga mkono watu wanaopinga uwepo wa Mtambo wa Nyuklia wa Koodankulam.

Waandamanaji nchini kote wanatuma saini zao huko Kudankulam, India, kama namna ya kuonesha mshikamano katika mkakati wa kutokubaliana na matumizi ya nguvu ya nyuklia. Picha na Dipti Desai. Hati miliki Demotix (15/03/2012)

Pia, siku ya Jumapili, chama cha Kijamaa cha Janata (cha kidemokrasia) huko Kerala kilitoa tamko la kuonesha ushirikiano na watu wanaopinga mpango wa mradi wa Mitambo ya Nyuklia huko Koodankulam katika jimbo la Tamil Nadu.

Wanawake kutoka miongoni mwa waandamanaji bado wangali gerezani. Anitha S. anaandika kukuhusiana na wanawake hao katika makala yenye kichwa cha habari Wanawake wa Koodankulam kutoka Gerezani: mwambie kila mmja kuwa bado tungali huku!:

Xavieramma anasema, “tupo hapa ili ulimwengu usiendelee zaidi kuona mitambo ya nyuklia iliyo hatari na isiyokuwa na manufaa…. Nimeona kuwa kuna watu wengi sana katika maeneo mbalimbali nchini wanaoendelea na maandamano. Sio tu kuhusu kupoteza ardhi na bahari yao, lakini ni kuhusiana na kujenga matabaka na huku ukichukulia maisha yenyewe yanavyokuwa katika hatari. Nani angependa kuishi katika mazingira kama haya?”

Kama alivyosema mwanamke mmoja aitwaye Selvi, “hii ni mara tu baada ya kuwa miongoni mwa sehemu ya kujituma ndipo tulipogundua kuwa kujaribu kuweka misingi ya haki ya mtu ya kuishi kama mtu anavyotegemea, akiendeleza utamaduni wa kuishi kindugu na pia kuhoji mambo yanayotekelezwa bila hata ya kujadiliana na watu ni karibu sawa na kosa la jinai na uhaini”.

Kama Sundari alivyosema, “Tupo hapa kwa ajili ya jambo moja tu- tupo hapa kwa ajili ya ulimwengu.

Walitaka kuuambia ulimwengu kuwa tupo hapa, ndani, tumezuiwa kimwili tu kwa kuta za matofali na chuma.

“Mwambie kila mmoja kuwa bado tuko hapa”.

Bado wapo katika gereza la wanawake la Trichy, wakiwa bado wanashikilia msimamo wa dunia wa “kutokomeza moja ya silaha hatari sana duniani iliyogunduliwa na mwanadamu”.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.