Kambodia Yaomboleza Kifo cha Mfalme Norodom Sihanouk

Nchi ya Kambodia inaomboleza kifo cha baba Mfalme Norodom Sihanouk aliyefariki tarehe15 Ockoba, 2012. Sihanouk anajulikana kama shujaa wa dola ya Kambodia kutokana na mafanikio yake ambayo ni pamoja na kuipatia uhuru nchi yake kwa njia ya amani kutoka kwa ukoloni wa Kifaransa mnamo mwaka 1953, kuiongoza nchi katika njia ya mafanikio wakati wa Sangkum Reastr Niyum kwa kushinda kesi katika Mahakama ya Kimataifa mnamo mwaka 1962 iliyoifanya Kambodia kupata umiliki halali wa hekalu la Preah Vihear karibu na mpaka wa Thai, na haswa haswa jukumu lake kubwa katika Mkataba wa Amani wa Paris mwaka 1991 uliohitimisha vita vya kiraia na hatimaye kuleta amani nchini Kambodia.

“Wewe ni shujaa wetu, tutakukosa” ni ujumbe uliokuwa unatolewa na waombolezaji wote, raia wasio wa mtandaoni na wale wa mtandaoni kufuatia kifo cha mfalme wao. Mwili wake ulirudishwa nchini kutoka Beijing mahali ambapo alipendelea kwenda kwa ajili ya matibabu.

Cambodians were mourning the late King Sihanouk

Watu wa Kambodia walijipanga katika misafara pembezoni mwa barabara pana ya Kirusi karibu na jengo la mikutano la Mawaziri wakisubiria kuupokea mwili wa Baba Mfalme Norodom Sihanouk. Picha na mwandishi wa posti hii.

Mnamo Oktoba 17, 2012, mamilioni ya watu walijipanga katika misafara pembezoni mwa barabara itokayo uwanja wa ndege wa kimataifa kuelekea katika Kasri Tukufu ili kutoa heshima yao ya mwisho kwa Mfalme, tukio linalokumbusha tukio la kihistoria la kurudi nchini Kambodia kwa mfalme Sihanouk mwaka 1991 baada ya kuwa nje ya nchi kwa miaka 13.

Habari za kifo cha Sihanouk zilianza kusambaa wakati wa likizo ndefu ya sherehe ya Pchum Ben. Hali ilibadilika ghafla katika mitandao ya intaneti mara baada ya watu kuanza kutuma maneno ya kumkumbuka hayati mfalme wao. Watu wa Kambodia walitumia kiungo habari#RIPKingSihanouk cha Twita katika kuomboleza:

@Cambodian_VIPz #RIPKingSihanouk Tuna huzuni na tunalia, umetuacha. Baba Mfalme wa uhuru Norodom Sihanouk. pic.twitter.com/11x8wRXD

‏@lanycassie #Pumzika kwa amani Mfalme Sihanouk, babu yangu shujaa ameutumikia ulimwengu ipasavyo <3 pic.twitter.com/fuD2ilqt

@Nida_CamELF Bila yeye, Kambodia inaweza tena kuwa mtumwa wa ukoloni wa Kifaransa. #RIPKingSihanouk

@PinkyElevenShi Hata kama mvua inanyesha, watu wa Kambodia bado wanaendelea kuwepo mbele ya Kasri Tukufu. Hali hii inanifanya nijisikie kulia. # Pumzika kwa amani mfalme Sihanouk

Pia kuna kurasa za Facebook zilizoanzishwa kwa kumbukumbu ya Baba Mfalme:

Pumzika kwa amani Norodmo Sihanouk

King Norodom Sihanouk

Watu wa Kambodia kutoka katika majimbo na maeneo mbalimbali waliungana kuomboleza kifo cha Mfalme Norodom Sihanouk. Picha kutoka katika hifadhi ya picha za Facebook ya Somdech Ta (Mfalme Norodom Sihanouk)

Khmerbird Anategemea kuwaona wanasiasa wa Kambodia wakifuata mafundisho ya hayati mfalme:

Baba Mfalme aliwahi kusema (chanzo):

Nahitaji nchi yangu kuwa huru, wakati wote kuwa huru. Nimefanya kwa kadiri ya uwezo wangu, lakini mimi kama binadamu, siwezi kuwa mkamilifu, hakuna aliye mkamilifu.

Ni matumaini yangu kuwa wanasiasa wote wa Kambodia watayafuata maelezo haya.Baba Mfalme alikiri kuwa yeye si mkamilifu, lakini alikuwa na maono thabiti ya kuifanya nchi yake kuwa huru.

Khmerbird anaainishaurithi ambao Sihanouk ameuacha:

Aliijenga nchi nzuri na kuifanya nchi ya Kambodia kuwa nchi inayovutia sana katika bara la Asia. Kuna jambo moja tunalolifahamu fika kuwa (Sihanouk) aliipenda nchi yake na alitaka kuleta furaha kwa watu wake.

Kifo cha Mfalme kiliwahamasisha raia kama vile raia huyuKoh Tha ambaye alihamasika kuchangia zaidi katika maendeleo ya nchi:

Nilifuatilia Televisheni zilizokuwa zinaonesha sherehe, picha za kihistoria na hati za hayati Mfalme wangu. Sifahamu ni kwa nini akili yangu inajisikia kuchanganyikiwa, yenye huzuni na masikitiko. Chozi lilinitoka moyoni. Ninapata hisia kali kuwa mimi mwenyewe pia na nchi yangu tumempoteza shujaa mkubwa. Na ndipo nguvu kubwa ikaja katika moyo wangu na kujisemea “Kok Tha , kuna jambo ambalo unapaswa kuliwekea juhudi zaidi la kusaidia na kuijenga nchi yako”. Nilijisikia kuwa, kile nilichokwisha kukifanya hadi sasa hakitoshi na ni kidogo sana ukilinganisha na kile alichokifanya Mfalme wangu. Ninapaswa kuendelea kujituma na kujitolea kwa wenzangu, mashirika ya vijana, watu wa kupigiwa mfano, marafiki zangu, vijana, familia na mpenzi wangu.

Hafla ya kitaifa ya maombolezo ya Mfalme itaendelea hadi tarehe 23 Oktoba, 2012. wananchi wanaweza kutoa heshima yao ya mwisho kwa kufika katika Kasri Tukufu kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo. Baada ya muda huu, mwili wa Mfalme utachomwa hadi kuwa majivu kulingana na mila na desturi za Budha.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.