Zambia: Filamu yaYouTube Kuhusu Athari za Machimbo ya Madini

Filamu ya uchuguzi kuhusu uchimbaji wa madini ya shaba nchini Zambia na madhara yake kwa jamii imewekwa kwenye mtandao wa YouTube na mpaka sasa imetazamwa takribani mara 6,000.

Sehemu ya filamu hiyo iitwayo “Zambia: Shaba nzuri, Shaba mbaya” iliripotiwa na ulimwengu wa blogu na Zambian Economist. Chola Mukanga, mtengenezaji wa blogu hiyo, aliandika:

Ni filamu bora kabisa na yenye maudhui mazito ya uchunguzi kuhusu udhaifu wa sekta ya uchimbaji wa madini nchini Zambia na uharibifu wa kimazingira unaoambatana na shughuli hizo. Haya ni masuala ambayo tumeyajadili mara nyingi katika tovuti hii lakini imekuwa vyema kuona masuala hayo yameletwa tena kupitia filamu hii. Filamu husika ilitengenezwa mwezi Aprili 2012. Kwa masikitiko, imebidi waandishi wasio wa ki-Zambia kuifanya filamu hii iwe kama tunavyoiona. Wako wapi waandishi wetu wa habari za uchunguzi?

Watumiaji wa mitandao wameitikia kwa maoni tofauti kuhusu maudhui ya sehemu ya filamu hiyo iliyowekwa kwenye YouTube. George Chisenga alikuwa na maaoni haya:

Hata sijui nini cha kusema lakini kile ninachoweza kusema sasa ni kwamba ninajisikia kukerwa na kwa kweli sijui cha kufanya na kile ambacho sote kama taifa tunaweza kufanya ili angalau sekta ya madini itufaidishe na sisi siku moja

TheJosok aliomboleza:

Jililie eh nchi yetu nzuri. Kwa nini tubaki masikini katikati ya utajiri huu wa madini yanayochimbwa kwa gharama ya afya za wenyeji?

Ramani ya Zambia kuonyesha maeneo yenye machimbo ya madini nchini humo. Picha imetolewa na mtumiaji wa Wikipedia Acntx chini ya Creative Commons (CC BY-SA 3.0).

gogohasme2 aliandika:

[…] Mimi ni m-Zambia pia na baada ya kutazama filamu hii sasa ninadhani tunahitaji kuja pamoja tujaribu kupigania nchini yetu na sio kuishia tu kuiangalia filamu hii na kuacha mambo yaendelee jinsi yalivyo. Tunahitaji kuja na kitu cha kufanya, si muda wa kusmea MMD AU PF WAMEFANYA HIVI, tunaweza kusimama na kupaza sauti zetu zisikike…

Kitu kidogo ambacho Wa-Zambia wanaweza kutegemea ni kwamba viongozi wa kisiasa katika nchi hii si tu waitazame filamu hii ya uchunguzi bali wachukue hatua madhubuti.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.