Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Aprili, 2009
Rwanda: Miaka kumi na tano baada ya mauaji ya Kimbari
Hivi karibuni zilifanyika sherehe za kitaifa nchini Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya kutimiza miaka 15 tangu mauaji ya Kimbari. Mauaji hayo yaliangamiza maisha ya watu wapatao 800,000. Mnamo tarehe 7 Aprili, maadhimisho yalifanyika katika mji mkuu wa Kigali, na pia katika mji wa Nyanza, ambapo watu wapatao 5000 waliuawa kinyama. Katika Uwanja wa Mpira wa Kigali, maelfu ya mishumaa iliwashwa na kupangiliwa katika namna ambayo iliunda neno "Matumaini" katika lugha tatu.
Afrika ya Kusini: ANC Yafanya Mjadala wa Uchaguzi Kwa Kutumia huduma ya Twita
Vyama vya siasa nchini Afrika ya kusini vimo katika hatua za mwisho za kampeni ya uchaguzi ujao. Chama tawala cha ANC (African National Congress) kilifanya mjadala kwa kutumia huduma ya twita.
Nguvu ya Watu Maarufu Katika uchaguzi wa India
Waigizaji na watengenezaji filamu maarufu nchini India wana ushawishi mkubwa. Kushiriki kwa watoa burudani kutoka Bolywood (watengeneza wa filamu za Kihindi) wenye makao yao huko mjini Mumbai na wale wa filamu za Kitamil na Kitelugu kumepanda ghafla wakati huu wa kampeni za uchaguzi ujao wa India. Soma jinsi ambavyo wachezaji filamu maarufu wa India wanavyotoa ushawishi wakati wa kampeni.
Wanawake na Uchaguzi Nchini India
Demokrasi kubwa zaidi duniani, India, itafanya uchaguzi mkuu utakaoanza katika wiki chache zijazo kutoka sasa. Wanawake wa India, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyimwa nafasi yao ya haki majumbani, kazini na katika hatamu za uongozi wana dau kubwa katika uchaguzi ujao. Japokuwa wanawake wengi wanaanza kuwa na ufahamu wa haki zao za kupiga kura na wanashiriki katika siasa kwenye ngazi za chini, ripoti hii inaeleza kwamba inavyoelekea mwaka huu ni wanawake wachache zaidi watakaochaguliwa katika bunge la nchi.