Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Februari, 2015
Watoto Waliokosa Masomo kwa Miezi kadhaa, Wafundishwa kwa Njia ya Skype Nchini Libya
Haifa El-Zahawi, raia wa Libya aishiye New York, kwa mara ya kwanza amewapatia fursa ya kusoma watoto wa nchi atokayo ya Libya kufuatia watoto hao kushindwa kwenda shuleni kwa miezi kadhaa sasa. Shukrani kwa mawasiliano kupitia Skype
Asasi ya Kiraia Inayofuatilia Bunge Yawaunganisha Wabunge Wanawake na Wananchi wa Uganda
Asasi ya Kiraia ya Parliament Watch Uganda iliandaa mjadala wa kujadiliana na wabunge wanawake kwenye mtandao wa Twita kuhusu mada 'Kuwafanya Wanawake Wathaminiwe Kwenye Shughuli za Kibunge'.
Mradi wa Video Waelezea Mapambano ya Kimaisha ya Watu wa Papua ya Magharibi
"Hizi ni habari tofauti na zile za mgogoro uliopo: Harakati za kupata elimu, mazingira, usawa na utu."
Kampeni ya Facebook Yampa Mwandishi wa Iran Masih Alinejad Tuzo ya Haki za Wanawake
Mwandishi wa ki-Iran ameshinda Tuzo ya Haki za wanawake kufuatia harakati zake za kwenye mtandao wa Facebook unaoitwa "My Stealthy Freedom."
Ufisadi Uliofanywa na Makampuni Makubwa Katika Kupambana na Ebola Nchini Sierra Leone
Makampuni matano nchini Sierra Leone yanasemekana kutumia fedha zilizokusudiwa kupambana na Ebola kwa njia za kifisadi: Haya hapa makampuni matano yaliyokuwa yameingia mikataba mikubwa ya kusambaza vifaa na kutoa huduma...
Wanafunzi Nchini Tanzania Kufundishwa kwa Lugha ya Kiswahili, si Kiingereza
Rais Jakaya Kikwete amezindua sera mpya ya elimu nchini Tanzania juma lililopita, ambayo pamoja na mabadiliko mengine, inaingiza rasmi Kiswahili kama lugha ya kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa elimu.
Mwanamke Atumia Mtandao wa Instagram Kubadili Mtazamo Kuhusu Somalia
Ugaaso Boocow anataka kubadili mtazamo wa watu kuhusu nchi ya Somalia. Lakini badala ya kuingia mitaani au kutumia radio, ameamua kuingia kwenye mtandao wa Instagram na anakuwa maarufu humo.
Mapendekezo Yanapokelewa kwa Ajili ya Mwezi wa Historia Nyeupe 2015
Likiwa limeandaliwa na blogu ya Africa is a Country [Afrika ni Nchi], tukio la Mwezi wa Historia Nyeupe linajongea mwezi ujao: Mwezi Machi mwaka jana ndio ulikuwa mwezi wa uzinduzi...
2015 Mwaka wa Kufanyika Chaguzi Huru na Haki Barani Afrika
Wekesa Sylvanus anataraji kwamba 2015 utakuwa mwaka wa chaguzi huru na haki barani Afrika: https://wekesasylvanus.wordpress.com/2015/02/18/will-2015-be-a-year-of-free-and-fair-elections-in-africa/ Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi barani Afrika, ushindani nyakati za uchaguzi...
Chemsha Bongo: Je, Uko Kwenye Hatari ya Kugeuka Gaidi?
Chemsha bongo hii imeandaliwa kwa kutumia utafiti unaofanywa na serikali ya Marekani unaotumiwa kuwabaini watu wenye hatari ya kuwa magaidi au jamii zilizokwenye hatari ya kukumbatia na kuleta itikadi zenye msimamo mkali.