Makala haya na taarifa ya habari iliyoandaliwa na Bradley Campbell kwa ajili ya kipindi cha The World kama sehemu ya kipindi cha Across Women's Lives kilichoonekana mwanzo kwenye kwenye tovuti ya PRI.org mnamo Februari 18, 2015, na inachapishwa tena kama sehemu ya makubaliano ya kushirikiana maudhui.
Somalia ni nchi iliyoharibiwa vibaya kwa vita.
Tumelitangaza hilo kwa kina.
Lakini kuna mengi zaidi kuhusu nchi hiyo. Hicho ndicho Ugaaso Boocow anachotaka kukionesha. Wazazi wake wana asili ya Toronto, na amehamia Mogadishu hivi majuzi. Hata hivyo, ili kuweza kuwasiliana na rafiki zake na familia yake inayoishi nchini Kanada, ilibidi kuanza kuweka picha na video fupi fupi kwenye mtandao wa Instagram.
Na sasa, zaidi ya watu 47,000 na idadi wanaendelea kuongezeka, wanafuatilia anuani yake. “Ningependa kuonesha picha za vitu visivyokuwepo nchini Kanada, kama vile juisi za matunda, matikiti maji na maembe, malimao yanayokamuliwa kuwa juisi -kwa ujumla nchi nzuri yenye pwani ndefu zaidi barani Afrika,” anasema. “Ili kuonesha kwamba ni kawaida sana kutembelea maeneo ya hapa na kuishi hapa na kufanya kazi hapa na kuwa mwanamke binti nchini hapa.”
https://instagram.com/p/zP9MypMR2A/
Picha zake ni nzuri. Lakini kwa kuziangalia kwa haraka, huwezi kuona picha zikisema mengi, hasa zile zinazoonesha barabara zilizochongwa au taa za barabarani. “Huwezi kuamini mambo madogo niliyokuwa nayabandika na kuyaona hayana maana kama ungekuwa Kanada, anasema. “Kwa nini upige picha taa za barabarani? Hiyo ni kwa sababu kuna taa hapa. Barabara zimetengenezwa. Tunayo majengo. Hayo yote yanawashangaza watu kwa sababu yoyote.”
Wafuatiliaji wake wanaishi kwenye mabara yote na wanatoka kwenye nchi mbambali. Wapo wanaotoka kwenye mji wake wa Toronto. Wengine wako kwenye nchi za ki-Skandinavia. Wengi wako Naijeria. ANataka watu wawe na mtazamo chanya kwa maneno kama vile Somalia, Mogadishu, na Afrika Mashariki.
Amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu, pia. Mogadishu ni nyumbani kwake. “Siku zote Mogadishu imekuwa nyumbani kwangu moyoni. Sikuwa Mogadishu kwa miaka 20, lakini siku zote Mogadishu imekuwa, na itaendelea kuwa nyumbani kwangu.”