Juma hili, The Intercept ilibaini mfumo wa maswali kwamba serikali ya Marekani inawahamasisha watu wa ustawi wa jamii, walimu na polisi kutumia maswali fulani fulani ili kuwabaini magaidi.
Mfumo huo unatarajiwa “kuwaweka maafisa wa serikali ya Marekani katika hali ya tahadhari kwa watu wenye hatari ya kugeuka kuwa watu wa ghasia, na familia au jamii zilizo kwenye uwezekano wa kukumbatia itikadi za kikaidi.”
Maswali hayo yaliyochambuliwa kwenye karabrasha la ndani ya serikali lenye kurasa 36 lilipatikana kupitia jarida moja la mtandaoni na lilipangiliwa na Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa Kupambana na Itikadi Kali, unatoa mwito kwa jamii na viongozi wa dini wa kila mahali kufanya kazi na mashirika ya kiserikali na kusimamia sheria .
Ikulu ya Marekani hivi sasa ni mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa siku tatu kuhusu Kupambana na Itikadi kali ukiwa na wawakilishi kutoka kwenye nchi zaidi ya 60.
Kwenye kipengele kama “Kuonesha Kukata tamaa, Kutokujiamini,” “Kuzungumizia Kujidhuru au Kuwadhuru wengine,” na “Kujitambulisha na Makundi (Rangi, Utaifa, Dini, Kabila),” maswali hayo yanawaomba walimu, ustawi wa jamii na maafisa wa polisi kuwapa alama watu kati za 1 na 5.
Wakati tukizoma karabrasha hilo, hatukujizuia isipokuwa kucheka kwa sauti kwa sababu ya mtindo wa kupunguza mambo unaotumika kwenye utafiti huo. Tuliamua kutengeneza chemsha bongo yetu wenyewe kwa kutumia bashiri nyepesi zilizofanywa na Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi kwenye kutunga maswali yake.
Shiriki Chemshabongo yetu ya Kukuchekesha.
Chemshabongo hii imeandaliwa na Taisa Sganzerla, Elizabeth Rivera, Amira Alhussaini naSahar Habib Ghazi.