Tetesi juu ya kusambaa kwa waandamanaji wa kifaransa waliovalia “fulana ya njano” katika nchi nyingine za Ulaya ilivuma sana katika mitandao ya kijamii nchini China kabla ya sikukuu ya Krismas.
Habari hiyo ilitokea baada ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kutangaza makubaliano kadhaa akihutubia juu ya malalamiko ya waandamanaji juu ya sera za uchumi. Wakati Macron akitegemea utulivu na amani kurejea, tetesi iliyotengenezwa china ilitabiri tofauti.
Matoleo mengi ya habari yalisambaa kupitia baadhi akaunti ndogo za kublogu kwenye Weibo na wechat, zikinukuu vyanzo kutoka bidhaa ya muuza jumla katika Yiwu—mji ambao unajulikana kama mji na kituo cha mauzo ya jumla —ambaye alieleza kuwa akiba yao yote ya fulana za njano imeuzwa nchi za nje na mahitaji zaidi ya bidhaa hiyo yanatoka katika nchi za Ulaya kama vile Swedeni, mji wa Prague, Uswisi, n.k. Habari hiyo ina maana kuwa waandamanaji wenye “fulana za njano” walikuwa wanasambaa katika bara zima.
Hapa kuna toleo moja la habari ambalo lilisambaa kupitia Weibo na WeChat:
【义乌指数】中国义乌的服装调研报告指出,现在来自欧洲的“黄背心”订单继续暴涨,现在黄背心制作工作已经在加班加点地进行,更有不少跨境电商卖家将此视为一次绝佳的销售机会。不少网友说,根据义乌商品市场的大数据,可以预测,未来黄背心运动的的浪潮还有可能蔓延到瑞典、捷克、瑞士、西班牙等国。早前就有外媒发文指出,义乌具有一股神秘力量,可以通过市场行情来预测国际政治大事件的走向。在义乌,接受的海外订单数量更被视为民意的风向标,可以惊人地对将要发生的事件做出准确预测。早在2016年美国大选的时候,义乌制造商就通过美国订购的旗帜和衣衫的数量提前5个月预测出特朗普将会成为总统。据了解,目前义乌的一些纺织厂已经开始陆续接受到美国订单,开始生产特朗普2020年竞选时的旗帜和支持者所穿的衬衫,由于订单量已经比民主党竞选所开出的需求高出数倍,因此也有人通过这点来预测特朗普很有可能连任美国总统。这是中国制造的大数据威力
[kiwango cha mauzo ya Yiwu ] taarifa ya utafiti wa Yiwu kuhusu mavazi ilionesha kwamba mahitaji kutoka Ulaya ya “fulana za najno” yameendelea kuongezeka. Watengenezaji walifanya kazi hadi masaa ya ziada ili kukabili mahitaji na wafanyabiashara wa nje wa jukwaa la kielekitroniki wanauona mwenendo huo kama ni fursa nzuri ya mauzo. Raia wa mtandaoni nchini china wanaamini kwamba kwa kuzingatia kiwango cha mauzo ya bidhaa ya Yiwu na taarifa yake kubwa, fulana za njano zinaweza kusambaa Sweden, Jamhuri ya Cheksolovakia, Uswisi na Hispania. Magazeti ya kigeni yaliandika kuwa kiwango cha mauzo ya Yiwu hakika kinaweza kutabiri mwenendo wa siasa za kimataifa. Uhitaji wa bidhaa kutoka katika soko la nchi za nje linakuwa kama viashiria vya maoni ya umma na kwa hiyo inaweza kutabiri matokeo sahihi katika matukio ya kisiasa. Mwaka 2016 miezi mitano kabla ya uchaguzi wa Urais Marekani, kutokana na mahitaji ya fulana na bendera kwa ajili ya uchaguzi watengenezaji wa fulana hizo katika mji wa Yiwu walikuwa wametabiri kuwa Donald Trump angeshinda. Waangalizi wanasema kwamba viwanda vya nguo katika Yiwu vimeanza kupokea mahitaji kutoka Marekeni na vimeanza kutengeneza bendera na fulana kwa wafuasi wa Trump kwa ajili ya uchaguzi wa urais wa 2020. Mahitaji sasa ni makubwa zaidi ya mahitaji ya wafuasi wa chama cha Demokrasia. Baadhi wameanza kutabiri kuwa Trump atachaguliwa tena. Hii inaoneshwa na nguvu kubwa ya taarifa za kutoka nchini china.
Wengi wametwiiti na kutoa maoni kuwa “Yiwu imekuwa msingi wa kutabiri mwelekeo wa mambo ulimwenguni”, na “ukiangalia taarifa za mauzo katika nchi za nje unaweza kuwa mchambuzi wa mambo duniani.”
Asili ya kiwango cha mauzo ya Yiwu
Yiwu ipo katika jimbo la Zhejiang,na ni mji wa kibiashara mshuhuri duniani kwa bidhaa ndogo ndogo, na moja ya soko linalojulikana sana nchini China kwa biashara ya kuuza bidhaa ndogo ndogo kwa jumla. Yiwu ni mji wa kimataifa wa biashara una kiwango kinachojulikana kama kiwango cha mauzo ya bidhaa ya China Yiwu ambayo huakisi mwelekeo wa soko.
Katika kipindi cha uchaguzi Marekani mwaka 2016, kiwango cha mauzo ya Yiwu kilikuwa ni mada nzito katika mitandao ya kijamii nchini China juu ya mjadala kuhusu takwimu za mahitaji ya bidhaa za uchaguzi kutoka Yiwu ambazo zilionesha kuwa Donald Trump alikuwa maarufu zaidi ya Hillary Clinton. Baada ya uchaguzi, hata vyombo vya habari vya serikali vilitaarifu kwamba takwimu za mahitaji ya bidhaa kutoka Yiwu na Alibaba yalikuwa ni nguvu ya kutabiria, na raia wengi mtandaoni wa nchi ya china wanaamini kwamba kiwango cha mauzo ya Yiwu kilitabiri sahihi kabisa juu ya uchaguzi wa Marekani. Baadhi ya waangalizi wa vyombo vya habari waliharakia kusema kuwa tafsiri hiyo ni tatizo kwa kuwa Clinton alipata kura zaidi ya Trump lakini uchambuzi huo ulipuuzwa..
Sasa , Global Times ambacho ni chombo cha habari cha serikali kimethibitisha habari iliyopo mtandaoni na kuripoti kuwa kuna akiba kubwa ya fulana za njano katika mji wa kibiashara na ukubwa wa mauzo yake katika miezi ya hivi karibuni sio mkubwa kama miezi ya mwaka jana. zithe. Hata hivyo taarifa ya Global Times haijazuia chochote juu ya kusambaa kwa taarifa ya kiwango cha mauzo ya Yiwu. Kiukweli, maoni mapya yameibuka baada ya sikukuu ya Krismas yanayothibitisha kiwango cha mauzo ya Yiwu kuwa na nguvu ya kutabiri. Habari iliyochapishwa katika majukwaa ya mitandao mingi ya kijamii yanakiri kuwepo na makosa ya kiasi cha mauzo ya fulana za njano, lakini inaendelea kusistiza kwamba kiwango cha mauzo ya Yiwu imefanikiwa kutabiri matokeo ya uchaguzi wa Urais wa Marekani mwaka 2016 na kombe la dunia la mwaka 2018.
Mwandishi alirudia hotuba ya tarehe 18 Desemba ya Rais wa china Xi Jinping kwenye sikukuu ya kumbukumbu ya 40 juu ya “uwazi na mageuzi ya nchi”, ambapo aliitaja Yiwu kama mfano wa mageuzi hayo. Hotuba hiyo ilihitimisha kuwa uwezo wa kutabiri wa kiwango cha mauzo ya Yiwu huakisi historia mpya ya mageuzi ya nchi:
实际上,义乌之所以能够一次次“精准预测“国际重大事件的走向,究其原因是义乌人通过几十年的奋力拼搏,将小商品产业在世界范围内做的了独树一帜、傲视群雄,成为世界多国所依赖的小商品产地。
在改革开放的历史浪潮中,就是无数个义乌这样曾经名不见经传的无名小城,在国家政策的鼓励扶持下,刻苦攻坚、努力拼搏、敢为天下先,使中国在短短40年里,实现了史无前例的惊天巨变。
Sababu ya Yiwu kuweza “kutabiri kwa usahihi” mwelekeo wa mambo ya dunia mara kwa mara yanatookana na mchango wa watu wa Yiwu miongo michache iliyopita. Wamepitia njia tofauti katika masoko ya bidhaa duniani na kuanzisha mji wenye hadhi ya juu kama mji wa viwanda vya kutengeneza mahitaji ya kila siku duniani.
Sera ya uwazi na mageuzi imesaidia miji mingi kama Yiwu kuwa na hatua na kupata mafanikio. Jitihada zao zimeleta mageuzi makubwa nchini China katika miaka 40 tu.
Huu mwingiliano wa uwezo wa kiwango cha mauzo ya Yiwu kutabiri na mageuzi ya kiuchumi nchini China umefanya hadithi ya asili ya Yiwu kuwa ngumu kubadilishwa.