· Agosti, 2009

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Agosti, 2009

Mexico: Simulizi za Siri Kwenye Twita

  25 Agosti 2009

Rafa Saavedra ni mtaalamu wa utamaduni wa chini chini kutoka mji wa Tijuana, Maxico. Katika mahojiano, anaelezea kila kitu kinachohusu mradi wake mmoja wa hivi karibuni unaojumuisha Twita na utoboaji wa siri.

Iangazeni Naijeria: Imetosha Sasa Basi

Pamoja na kuwa nchi yenye utajiri wa mafuta, hali ya ugavi wa umeme nchini Naijeria hairidhishi. “Katika sehemu nyingi za nchi, giza linatawala na majenereta yamechukua nafasi kama vyanzo vya nishati ya umeme” Inasema blogu ya Adebayo. Sasa Wanaijeria wameanzisha kampeni kubwa ya mtandao wa intaneti inayopinga hali hii inayogharikisha kwa kutumia tovuti za kijamii, hasa kwenye Twita kwa kutumia anwani ya #lightupnigeria (#iangazenaijeria).