Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini

Ukuta wa Berlini na Natalie Maynor

Ukuta wa Berlini na Natalie Maynor


Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.

Huko Ujerumani, mfululizo wa mifano ya vipande vya mchezo wa domino iliundwa kutumia maboya na kisha kunyanyuliwa ili baadaye yaangushwe kama ishara ya kumaliika kwa zama za Vita Baridi. Video hii iliyotayarishwa na NoCommentTV inaonyesha vipande hivyo vya domino, ambavyo vilichorwa na watoto huko Ujerumani na pia na wasanii wanaoishi maeneo mengine ambapo kuna migawanyiko na kuta, vikisimamishwa. Kipande cha kukupa vitu vya kuchagua kimezuiwa kufanya kazi, lakini unaweza kuona jinsi vipande hivyo vya domino vilivyoangushwa kwa kubofya kiungo hiki ili kuiona katika ukurasa wake wa YouTube.

Kule Kolombia, wanafunzi waliigiza uangukaji wa ukuta huo, kwa kupokezana kuvunjilia mbali ukuta wa zege:

Kutoka Ujerumani, mshabiki wa kuangusha domino Annodomino2007 amepandisha mtandaoni domino yake mwenyewe ili kuenzi kuanguka kwa ukuta huo, na pia kama kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 tangu alipoanza mapenzi yake makubwa kwa michezo ya domino:

Kule Marekani, wanachuo waliinua mfano wa Ukuta wa Berlini ambao mtu angeweza kuandika juu yake, yaani kama njia ya kuiamsha jamii:

Kutoka Mexico, VarinVxx alipandisha picha ya video ikionyesha ukuta mwingine ambao bado uko imara, Si Berlini, si Palestina, bali ni kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, Ukuta wa Aibu huko Marekani:

Krista Schyler pia analinganisha ukuta ulio kwenye mpaka wa Mexico na Marekani na ule wa Berlini, safari hii siyo tu kukazia kuhusu madhara ya uhamaji wa binadamu, lakini kutoka kwa mtazamo wa utunzaji wanyama pori pia:

Mradi huu wa majaribio (Mradi Rubani) kwa ajili ya makala ya video ya Ziashere inaonyesha kuta nyingine ambazo bado ziko imara, mojawapo ikiwa kule Ireland:

Video hiyo ya mwisho ina umri wa miaka 2 sasa, lakini bado ujumbe wake una maana: mtengeneza filamu Adam aliwahoji vijana kutoka pande zote mbili za ukuta Kaskazini na Kusini mwa Cyprus, ukanda wa kijani unaolindwa na vikosi vya helmeti za kibuluu vya Umoja wa Mataifa ambao unatenganisha WaCyprus wa Kituruki na Wacyprus wa Kigiriki, jambo linaoufanya mji huo uwe na heshima ya kuwa mji wa mwisho uliogawanyika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.