Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Agosti, 2010
Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam
Mwanamwali mdogo wa Kivietnam aliuwawa na mumewe wa Kikorea nchini Korea. Wanablogu wa Korea wanatoa rambirambi zao kwa kifo kibaya cha mke huyo mwenye umri mdogo huku wakiitaka serikali kutokomeza eneo hili lisiloonekana kwa urahisi la haki za binaadamu, linalohusiana na wachumba kutoka nchi za kigeni.
Italia: HAPANA kwa Vikwazo Dhidi ya Uhuru wa Kujieleza wa Mtandaoni
Muswada mpya wa habari na Unasaji wa siri wa Mawasiliano ambao umewasilishwa kwenye bunge la Italia unaweza kuanzisha "hatari ya malipo ya fidia" kwa wanablogu wote na vyombo vya habari vya mtandaoni.
Udhibiti Nchini Singapore
Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.