Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusiana na maandamano nchini Syria 2011/13
Madhara ya Vita kwa Watoto wa Syria:
Inakadiriwa kuwa, watoto wa Syria 4,355 wamekwishakuuawa (hadi tarehe 15/1/2013) katika mgogoro unaoendelea nchini Syria, hii ni kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na hifadhi ya Mapinduzi ya Syria ya Martyrs . Maelfu ya watoto wameshajeruhiwa, kushikiliwa, au kuachwa bila ya ndugu, au pia kutokupata msaada wa kimatibabu na pia misaada ya kibinadamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Wakimbizi za Umoja wa Mataifa (UNHCR), wakimbizi takribani 650,764 kutoka Syria wanaandikishwa au wanasubiri kuandikishwa ndani na nje ya Syria. Zaidi ya nusu yao (asilimia 52) ni wenye umri chini ya miaka 18. Hata hivyo, idadi kubwa ya watoto nchini wamekuwa wakikabiliana na maumivu makali ya kupoteza makazi yao, mali zao na wazazi wao. Tovuti ya Haki za Binadamu inataarifu:

watoto wa Syria katika mahangaiko, mbali na vita, pia wanakabiliana na baridi. Chanzo: Wasaidie Watoto
kiuhalisia, katika mazingira haya, mahitaji yote muhimu kwa ukuaji wa watoto yameharibiwa, , and the psychological damages of armed conflicts are incalculable…. waototo hawa, wanaoshindwa kukua katika mazingira mazuri na badala yake wanakabiliana na matukio ya ukatili wakiwa na umri mdogo kabisa, mara nyingi wanajijengeaa dhana ya kwamba vurugu ni njia kama zilivyonjia njia nyingine za kutatua migogoro, na kwa hiyo inakuwa vigumu sana kwao kutuma ujumbe wa amani na ulinzi wa kimataifa kwa vizazi vijavyo.
Watoto wa Syria wasaidiweje?
Mapema wiki hii, tulitoa taarifa kuhusiana na hali ngumu wanayokabiliana nayo watoto wa Syria kuhusiana na vita hii inayoisambaratisha nchi yao vipande vipande. Leo tunaangalia njia ambazo watu wangeweza kuzitumia ili kuondoa baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo watoto wa Syria.
Kwa namna utakavyofanya, unaweza kuonesha namna unavyoguswa na madhila wanayoyapata watoto wa Syria, na unaweza pia ukapaza sauti yako ili Umoja wa Mataifa utimize wajibu wake katika kulinda haki za watoto wa Syria wanaodhalilishwa nchini mwao. Onesha mshikamano wako pamoja na watoto wa Syria kwa:
- Onesha kujali kwako kwa kusambaza makala hii popote palipo na namna mbalimbali zitakazofanikisha kusaidia kuwaokoa watoto wa Syria kutoka katika mustakabali wa kutisha wa maisha yao>
- Sambaza matukio haya kupitia Rise 4 humanity ambayo ni:
Harakati maalum kwa ajili ya kuujulisha umma kuhusiana na makosa dhidi ya ubinadamu ulimwenguni kote pamoja na kusaidia kuyakomesha, kwa kuanzia na matukio ya kikatili yanayowapata watoto nchini Syria.
Video inayofuata [Tahadhari: Picha, zinaonesha watoto waliofariki] inawakilisha hali halisi ya Watoto wa Syria iliyoandaliwa na mpango wa Kupinga Unyanyasaji dhidi ya Binadamu, yaani Rise 4 Humanity.
- Jijini London Uingereza, tambua kuwa kwenye njia ya chini kwa chini ya treni ya mji kuna matangazo ya UNICEF yenye lengo la kuhamasisha kuwachangia watoto wa Syria, Changia paundi 5.
- Changia, KIASI CHOCHOTE, katika ukurasa mkuu wa UNICEF.
- Changia vitabu ili kusaidia elimu ya watoto wa Syria kupitia tovuti ya Kujitolea: Vitabu kwa ajili ya Syria(Books4Syria)
- Changia kupitia Safeworld ili kuisaidia shule iliyoko katika kambi ya wakimbizi ya Zaatari inayojulikana kama “kambi ya watoto” kwa kuwa takribani nusu ya wakazi ambao idadi yao ni 33,000, ni chini ya miaka 18.
- Changia ili usaidie watoto kupata mavazi, viatu na mablanketi kwa watoto, toa msaada kwa vitu muhimu vitakavyowasaidia watoto wakati wa baridi, hususani kwa ajili ya watoto wachanga.
Shirika la “Saidia Watoto (Save the Children) lilizindua kampeni ya kusitisha ukatili dhidi ya watoto nchini Syria. Muitikio ulikuwa wa kiwango kisichoelezeka– uliopelekea ulimwengu wote kutupia macho matukio ya kikatili wanayoyapitia watoto nchini Syria. Hii ilikuwa ni kampeni yetu iliyokuwa na kasi kubwa kabisa kuliko nyingine yoyote ambapo, maelfu ya watu walikuwa wakijiunga kila siku.

Tangazo la Hali ya Hatari ya baridi kwa Watoto wa Syria liliowekwa na UNICEF mnano mwezi Desemba 2012 katika njia ya treni ya chini kwa chini jijini London. Chanzo: Tafiti ya dunia (Global Research)
- Imeweka habari na picha za Watoto wa Syria katika ukurasa wa Facebook. Kwa kuusambaza ukurasa huu, unawezesha ukurasa huu kutembelewa na uungwaji mkono wa ukomeshwaji wa mauaji ya watoto nchini Syria.
- Katika Ukurasa wa Facebook: Saidia watoto wa Syria
- Katika ukurasa wa facebook: SRC Wakimbizi wa Syria nchini Lebanon[ar] (تنسيقية اللاجئين السوريين في لبنان)
- Sambaza ujumbe, shiriki katika matembezi ya Dunia kwa ajili ya watoto wa Syria
- Mfadhili yatima leo kwa kiasi cha $50 katika Yatima wa Syria (Syrian orphans)
- Change.org: Jiunge na Kampeni Komesha Ukatili Dhidi ya Watoto wa Syria
Weka Saini katika hati za Malalamiko Dhidi ya Serikali:
Saidia kwa kutuma tovuti hizi pamoja na hati za malalamiko kwa rafiki zako na kwa viongozi wako. Wanaweza kufanya mambo makubwa. Unaweza kufanya mambo makubwa.
- Avaaz: Walinde Watoto wa Syria sasa!
- Avazz: Komesha mateso ya Watoto wa Syria!
- Petition to Google: Badilisha michoromichoro ya 05/25/2012 ili kuonesha mshikamano pamoja na watu wa Syria.
- Huko Marekani, waambie viongozi walioteuliwa wakomeshe uchinjaji wa watu wa Syria kupitia Ubalozi Mdogo wa Syria Amerika
- Hati ya Malalamiko kwa Bunge la Marekani na kwa Rais ObamaPetition: Komesha Mauaji ya Syria
- Tovuti ya hati ya malalamiko: Kwa ndugu Rais Bashar Assad: Iambie Serikali ya Syria: Sitisha Unyanyasaji wa wa Watoto!

Mgogoro wa Syria unawadhuru watoto milioni 2. Tunahitaji mchango wako ili tumfikie kila mmoja. Chanzo: UNICEF España katika ukurasa wa Twitter.
Jumuia za Ndani Zinazowasaidia Watoto wa Syria:
- جمعية سردة للتنمية Jumuia ya Maendeleo ya SRDH
- مؤسسة الإغاثة والتنمية الإنسانية السورية Najda-Now International E.V
- Kwa ajuli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Syria. Taasisi ya Elimu ya Kimataifa: Hali ya hatari katika Elimu Nchini Syria: Namna ya Kusaidia
- Na zaidi ya mashirika 32 ya kitaifa na ya kimataifa yaliyo na jukumu la kuwalinda watoto kutoka nchini za Iraq, Lebanon, Jordan and Misri katika tovuti ya UNHCR ya wakimbizi wa Syria.
Video inayofuata, (wakiwa nje kwenye baridi: Familia za wakimbizi wa Syria wakikabiliana na baridi), imetumwa na savethechildrenuk ili kuelezea hitaji la watoto na harambee ya kuwasaidia watoto wa Syria ambao ni waakimbizi:
Watoto wa Syria ni wahanga wasio na hatia wa vita hii na kutoa msisitizo kwa wakati mgumu wanaoupitia na ujaribu kusaidia kuwaepusha na mateso wanayoyapa kwa kadiri ya utakavyoweza.
Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusiana na maandamano nchini Syria 2011/13