Mkanganyiko wa Makubaliano ya OIC Kuanzisha Ofisi Nchini Myanmar

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum Rohingya ya Myanmar .
Machafuko ya Juni 2012 huko magharibi mwa Myanmar yanayowahusisha Rohingya na Rakhine yaligusa mashirika ya kimataifa ya Kiislamu pamoja na nchi mbalimbali katika kujitolea kusaidia kutatua mgogoro huu pamoja na kutoa misaada kwa wahanga.

Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC), kwa mfano, limependekeza kuanzishwa kwa ofisi yake ya kudumu nchini Myanmar. Hatua hii iliibua hali ya kupingwa nchini kote, haswa haswa huko Yangon, Mandalay, Pakkoku, Sittwe na Phyar Pone. maoni ya mtandaoni pia yanaonesha msimamo mmoja wa kupinga uwepo wa OIC nchini Myanmar.

Watu wengi wa Myanmar wanaamini kuwa Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) halina ulazima wa kuwepo ili iwasaidie waislam wachache nchini Myanmar. Daktari Aye Maung ambaye ni mbunge na Rais wa chama cha Rakhine Nationalities Development alihoji [my] kuwa utoaji wa misaada unaweza kufanyika bila ya kuweka Ofisi ya OIC nchini:

Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) ni mahususi kwa dini, shirika linalojumuisha nchi 57 zilizo na ushirika na nchi za kiislam. Sio kama ASEAN ambayo ipo kikanda na yenye kujumuisha dini mbalimbali na wala siyo Umoja wa Ulaya.[…] na hivyo tunaweza na tulipaswa kupokea misaada kupitia serikali bila ya kufungua ofisi ya OIC.

Myo Set aliishauri Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) kuwasiliana moja kwa moja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya binafsi kama wameona kuwa kupitia serikalini sio njia muafaka:

Burma ina ushirikiano mzuri na mashirika binafsi pamoja na Umoja wa mataifa na ndio sababu hakuna haja ya siasa za mseto kama lengo kuu la OIC ni kusaidia tu chakula, malazi, huduma za afya na ulinzi kwa Waislamu. Chochote watakachohitaji kukitoa kinaweza kupitia Umoja wa Mataifa kama wameona mamlaka za Barma si njia muafaka.

Ko Htike aliandika akiwa na mtazamo kuwa fujo hazikutokana na vurugu za kidini, hivyo hali inajieleza wazi kuwa OIC haipaswi kubadili hali kuwa la uelekeo mmoja.

Jambo hili la Rohingya si mzozo wa kidini wala wa kikabila. Ni tatizo tu kati ya wahamiaji na wazawa. Ni jambo la kawaida kabisa ambalo mara nyingi hutokea katika nchi mbalimbali duniani. Siyo zaidi ya hapo.

Nadhani OIC isilifanye jambo hili kuwa la kidini. Ninaheshimu ukarimu wao wa kutoa misaada ya kibinadamu. Kama lengo ni misaada ya kibinadamu, basin a majimbo na mikoa mingine inapaswa pia ipewe misaada kama tu jinsi nchi nyingine (mfano. Japani, Amerika) wanavyofanya.

Ko Htike anakumbushia maoni yaliyozoeleka yanayozungumzwa nchini Myanmar, yanayopinga juhudi za Rohingya ya kutambua kama yechoed the popular domestic opinion in Myanmar, opposing the Rohingya's struggle for recognition as an ethnic minority in the country. Maonin kuhusiana na Rohingyas yamegawanyika; jamii za kimataifathe zinawachukulia wao kama kikundi kidogo mno kinachodharauliwa sana barani Asia.

Kwa wiki kadhaa kumekuwa na fununu kuhusu uwepo wa Hati ya Makubaliano iliyotiwa saini kati ya Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) na Wizara inayoshughulika na mambo ya Mipaka ya Myanmar pamoja na kuwa kuna taarifa zisizo za kina sana kama kweli makubaliano hayo yapo, na kama ndivyo, inajumuisha mambo gani. Walipoanza kutuma maoni yao wakipinga makubaliano hayo, Hmuu Zaw kutoka ofisi ya Rais alifafanua[my] kuwa, ofisi ya Oic itakuwa ni ya dharura tu itakayofanya kazi kama ofisi ya uwakilishi ya dharura na si kama ofisi ya kudumu ya uwakilishi.

Ufafanuzi huu haukuwashawishi watu wengi. Tyfone Athene alihoji muda halisi wa uwepo wa ofisi hii ya dharura:

Ofisi ya uwakili ya dharura? Itachukua muda gani? Miaka 60 au miaka isiyo na kikomo?

Poe Pwint Phyu anafikiri kuwa kama serikali ililitazama tukio la awali kuwa halikuwa la kidini, basi serikali isingepitisha makubaliano na OIC:

Maandamano dhidi ya OIC

Picha- CJ Ukurasa wa Facebook wa Myanmar

swali langu la mwisho kwa washauri wa Mheshimiwa Rais: mnafikiri mgogoro wa hivi karibuni kuwa umesababishwa na vurugu za kidini ( na hivyo mkaruhusu ofisi ya dharura ya OIC)Do you see this recent conflict as merely a religious riot (thus you allowed a temporary office for OIC) au ni jambo muhimu la kutelekeza na uonevu lililowaacha wazawa wa Rakhine kuwa wahanga? or urgent issue of neglect and violence which victimized Rakhine natives? Jibu litafafanua uelekeo wa serikali iliyopo madarakani na utayari wake kwa Rakhine na uwepo wa Umoja wa kidemokrasia—- ambapo kila msichana anaweza kupata elimu bure na haki sawa kutoka kwenye taasisi.

Wengine walikosoa kukosekana kwa uwazi kwa yale yanayofanywa na wizara za serikali. Ah Moe alitoa pendekezo [my] lake:

Iwe ni ofisi ya uwakilishi ya dharura au ni tawi la ofisi ya kudumu, tunachokiomba kwa sasa ni kuwa ni kuiweka wazi nakala ya hati ya makubaliano, hilo ndilo haswa tunalolihitaji.

Serekali ilijaribu kuwashawishi watu wasijihusishe na maandamano ya kupinga kuanzishwa kwa ofisi ya OIC; pamoja na ushawishi huu, maandamano yalifanyika Oktoba 15 katika majiji kadhaa nchini kote. Kwa kuhofia msukumo wa watu, ofisi ya Rais ilitangaza siku hiyo hiyo kuwa serikali isingeruhusu kuanzishwa kwa ofisi ya uwakilishi ya dharura OIC nchini Myanmar. Hata hivyo, haikutaja yaliyomo kwenye hati ya makubaliano iliyosababisha mkanganyiko. Haikueleweka wazi kama serikali ilishaitaarifu OIC kufuatia maamuzi haya.

Serikali imeihakikishia [my] umma kuwa itaendelea kupokea misaada ya kibinadamu kwa ushirikiano wa karibu na OIC na makundi mengine ya kimataifa.

Wakati huohuo, OIC wanasema kuwa bado hawajapokea taarifa rasmi kutoka serikali ya Myanmar kufuatia maamuzi yaliyofikiwa ya kutoruhusu kuwepo kwa ofisi ya uwakilishi ya OIC.

Katika habari zinazohusiana na hizi, Jumuia ya Msalaba Mwekundu ya Myanmar ilitoa tamko kupitia kwa waandishi wa habari ikikanusha uvumi kuwa inafadhili ofisi ya OIC iliyoanzishwa kinyemela katika jingo lao.

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum Rohingya ya Myanmar .

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.