Mradi wa Tafsiri: Kauli ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni

Katika siku saba zijazo, Wafasiri wa Kujitolea wa Mradi wa Lingua wa taasisi ya Global Voices watakuwa wakitafsiri makala maalumu ambayo ni harakati ya utetezi unaofanywa na umma mtandaoni na ambao unasaidia kulinda haki za watu kwenye mitandao ya intaneti na kuzitaka serikali zilizo wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Simu (International Telecommunication Union — ITU) kutunza matumizi huru ya Intaneti katika mkutano mkuu ujao wa ITU.

Utetezi huu uko wazi kutiwa saini na mtu mmojammoja au asasi ya kiraia, kauli hii ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni inasomeka kama ifuatavyo:

Mnamo Desemba 3, serikali mbalimbali ulimwenguni zitakutana ili kupitia upya mkataba muhimu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalojulikana kama Ushirika wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Simu (ITU). Kuna serikali zinazofikiri kupendekeza kupanua mamlaka ya ITU ili isimamie utawala wa Intaneti kwa njia ambazo pengine zitatishia uhuru na ubunifu katika kutumia Intaneti, huenda hatua hiyo itaongeza gharama za kutumia huduma, na hata pengine kumomonyoa haki za watu za mtandaoni. Tunatoa wito kwa asasi za kiraia na wanaharakati wa mtandaoni kutoka mataifa yote kutia saini kwenye Kauli hii ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni:

Uamuzi kuhusu uendeshaji wa Intaneti hauna budi kufanywa kwa namna iliyo wazi kwa kuhakihisha wadau wengi mbalimbali na halisi wanashirikishwa hasa kutoka asasi za kiraia, serikali na sekta binafsi. Tunaiomba ITU na nchi wanachama wake kuzingatia uwazi na kukataa mapendekezo yoyote yanayoweza kupanua mamlaka ya ITU kwenye maeneo ya uendeshaji masuala ya Intaneti yanayoweza kutishia haki za watu kwenye mitandao ya intaneti.

Ili kutia saini kwenye wito huu wa utetezi, tembelea tovuti ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni. Ili kutia saini, andika jina lako la kwanza, la ukoo, barua-pepe yako, jina la asasi yako (ikiwa unatia saini kwa niaba ya asasi ya kiraia), weka kiungo cha URL cha asasi hiyo, na chagua nchi yako.

Tafsiri zote pia zitapandishwa kwenye tovuti ya utetezi huu, ambayo imepata uhifadhi hapa OpenMedia, ambalo ni kundi la utetezi wa haki za watu la nchini Kanada.

Kadiri tafsiri zinavyojitokeza (tazama hapo juu), tafadhali washirikishe wengine pia viungo kupitia mitandao ya kijamii na marafiki!

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.