Mwanaharakati mashuhuri nchini Misri na mwanablogu Alaa Abd El Fattah alikamatwa akiwa nyumbani kwake takriban saa nne jioni mnamo Alhamisi, Novemba 28. Hati ya kukamatwa Abd El Fattah ilitolewa Jumanne iliyopita, kufuatia kusambaa kwa vurugu ya waandamanaji mjini Cairo. Baba mzazi wa mwanablogu huyo aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa aliamini kukamatwa kulikuwa ni kutekeleza sheria mpya iliyotungwa kupiga marufuku maandamano mitaani nchini Misri. Takribani watu 51 walikamatwa siku hiyo, miongoni mwao wakiwemo wanaharakati kadhaa maarufu. Wengi walipigwa na kunyanyaswa kijinsia.
Alaa alichukuliwa na polisi licha ya kuwa alitangaza kwamba yeye ndiye angejisalimisha kwa polisi siku ya Jumamosi, kulingana na taarifa aliyoitoa na ambayo shangazi yake, mwandishi mashuhuri wa misri Ahdaf Soueif, aliiweka kwenye mtandao wa Facebook.
Kulingana na taarifa ya mkewe, polisi wa Manal walitumia nguvu na vurugu wakati kukamatwa:
Polisi walitushambulia katika nyumba yetu na kumkamata @alaa na kunipiga mimi. Wao waliiba kompyuta ndogo za kupakata na simu za mkononi.
— لا لدستور العسكر (@manal) Novemba 28, 2013
alama za damu katika chumba chetu cha kulala ambapo polisi walimpigia @alaa اثار الدم في غرفة نومنا بعد ان ضربته الداخلية pic.twitter.com/DZZEKQwHz3
— لا لدستور العسكر (@manal) Novemba 28, 2013
Kama polisi tayari wamenipiga mimi katika nyumba yetu, nini watakachomfanyia @alaa . Nahofia usalama wake.
— لا لدستور العسكر (@manal) Novemba 28, 2013
Hakuna maelezo rasmi ya sababu ya kukamatwa kwake leo, hiyo ni kwa kuwa Alaa alikuwa ametangaza hadharani kuwa angejisalimisha mwenyewe siku ya Jumamosi.
Mkurugenzi wa Shirika la Utetezi wa Haki za Binadamu nchini Misri Heba Morayef alihusisha kukamatwa kwake na sheria ya kupambana na maandamano, ilitungwa mapema wiki hii:
Kukamatwa kwa Alaa kunaonyesha kwa nini MOI alitaka sheria hii iwe wazi kufafanua lugha isiyoeleweka katika ibara ya saba = kuwapa mamlaka ya kuamua kumkamata mwanaharakati yoyote wanayemtaka
— hebamorayef (@hebamorayef) Novemba 28, 2013
Hesham Mansour alitoa majibu yake mwenyewe ya kejeli:
ما تقولش مصر عملتلنا إيه.. قول مصر قبضت علي علاء عبد الفتاح كام مرة
— Hesham Mansour (@Heshoz) Novemba 29, 2013
Usiulize nini Misri imefanya kwa ajili yetu. Uliza mara ngapi Misri imemkamata Alaa
Mwanaharakati Mona Seif, dadake Alaa, alitoa taarifa kwa wafuasi wake eneo ambalo kakake amewekwa kizuizini:
اتأكدنا إن علاء في معسكر أمن مركزي اللي جنب الإدارة العامة لقوات أمن الجيزة على طريق القاهرة الإسكندرية الصحراوي. يا رب
— Mona Seif (@Monasosh) Novemba 28, 2013
Sisi sasa tuna uhakika kwamba Alaa anashikiliwa katika kambi ya CSF katika Giza, mjini Cairo – barabara ya Alexandria
Alaa Abd El Fattah alifungwa jela chini ya utawala wa Hosni Mubarak kwa siku 45 na tena na Baraza Kuu la Vikosi vya Jeshi mwaka 2011, ambapo yeye alibakia jela kwa karibu miezi miwili. vilevile alikakabiliwa na mashtaka chini ya utawala wa Mohamed Morsi mwaka wa 2013, pamoja mwandishi maarufu anayetumia jina la uandishi Bassem Youssef, katika kile wengi walijua kuwa mashtaka ya kisiasa kutumika kama mbinu ya vitisho. Kila mara, #FreeAlaa alama ashiria huibuka kuonyesha mshikamano. Inaonekana kwamba hali hii imerudi tena.
2 maoni