Baada ya Miezi Sita, Waathirika wa Kimbunga Haiyan Waendelea Kudai Msaada na Haki

Typhoon Haiyan caused a ship to ran aground in Leyte, destroying houses in a crowded coastal village. Photo by Alessandro Pavone/ Save the Children

Kimbunga Haiyan kilichosababisha meli kukwama katika eneo la Leyte na kuharibu nyumba katika kijiji cha pwani. Picha kwa hisani ya Alessandro Pavone / Tuwaokoe Watoto

Pia tazama Haiyan yaikumba Ufilipino.

Miezi sita iliyopita, maelfu walifariki katika eneo la Mashariki mwa Visayas nchini Philippines baada ya kukumbwa na kimbunga kikubwa cha Haiyan (ama kwa jina lingine Yolanda). Leo, maelfu bado wanaendelea kuteseka kutokana na ukosefu wa mpango wa kina wa serikali wa kukarabati eneo lililoharibiwa.

Baada ya kufahamu kuhusu ripoti hii, Seneta Chiz Escudero alikosoa maafisa wa serikali kwa kushindwa kuelewa uzito wa hali:

Inahuzunisha sana. Miezi sita baada ya kimbunga cha Yolanda, zaidi ya mwaka baada ya maafa yaliyopita hatujui hata ni nini hasa wanajamii walioathirika wanachohitaji? Sio juu ya nini tunaweza kutoa au tunachotaka kuwapatia? Tabia hii ya kutojali ni ya kuwaongezea machungu waathirika. Tunachokifanya ni sawa na jinai.

Kuongezeka kwa matatizo ni ukosefu wa uratibu miongoni mwa mashirika ya serikali:

Haiyan ilisababisha kuongezeka kwa dhoruba mwezi Novemba mwaka jana hali iliyoharibu maelfu ya vijiji. Zaidi ya watu milioni 16 waliathirika na maafa.

Mashirika kadhaa yalibainisha kwamba waathirika wa kimbunga wanapata nafuu pole pole lakini matatizo mengi yanaendelea. Shirika la Msalaba Mwekundu lilielezea kuwa huduma za msingi bado hazijarejeshwa katika baadhi ya maeneo:

Jamii zilizoathirika zimeonyesha nguvu ya ajabu na wengi wanaelekea kupona. Hata hivyo, viwango vya juu vya umaskini vya awali vililivyokuwa vyafanya watu kubaki nyuma na katika baadhi ya maeneo huduma za msingi hazijatengemaa

Ni nusu tu ya vituo vya afya katika mikoa iliyoathirika na kimbunga zimerudisha tena shughuli za kawaida hali ambayo imedhoofisha afya ya akina mama na watoto wanaozaliwa. Hii ni ripoti kutoka Hifadhi ya Watoto

Katika kituo cha afya katika eneo la Mashariki mwa Visayas, watoto kadhaa walikufa kutokana na hali ambayo kwa kawaida hutibika, kama vile hypothermia na hypoglycemia, kwa sababu wauguzi hawakuweza kuchunguza watoto wachanga vizuri usiku kwa sababu hapakuwa na umeme kuwezesha kuwasha taa.

Miezi minne baada ya kimbunga, nusu tu ya jamii zilioathirika ndio wameshuhudia vituo vyao vya afya vikifunguliwa tena upya. Changamoto katika huduma muhimu za kujifungua na kutunza watoto wachanga huduma zilikuwa sawa katika Tacloban na Leyte.

Wakati huo huo, Oxfam ilionya kuwa waathirika 200,000 katika maeneo ya pwani wako katika hatari ya kuathirika zaidi na umasikini kwa sababu mipango ya serikali ya kuwahamishia kwenye makazi salama bila kuzingatia jinsi wataendesha maisha yao baadae.

Profesa Carl Ramota alitembelea chuo kikuu cha Palo na kutoa taarifa ya hali ya kusikitisha katika shule:

Miezi sita baada ya kimbunga Yolanda kuathiri chuo chake cha Palo, Leyte, bado hakuna mpango wa wazi kwa ajili ya ukarabati au kuhamishwa kwa Shule Kuu [kitivo] ya Sayansi ya Afya. Wakati vyombo vya jirani tayari vinajengwa upya, chuo kikuu cha Palo bado kiko katika hali mbaya. Mbaya zaidi, paa la jengo kuu la kitivo hicho bado halijaondolewa, na ni tishio kwa kliniki ya uzazi inaendelea na shughuli zake pembeni mwake pamoja na wakazi wengine jirani.

Photo from Facebook page of Carl Ramota

Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Carl Ramota

Kiongozi wa vijana Divs Mosquera pia alitembelea Tacloban, eneo lililoathirika zaidi na maafa, na kuhuzunishwa na habari za waathirika wa kimbunga.

Miezi kadhaa baada ya Yolanda, Leyte bado ni mji uliotawaliwa na mahema. Nimelia sana tangu nilipofika, kusikiliza habari za waathirika. Inavunja tu moyo wangu.

Takwimu za serikali zilitaja kuwa idadi ya waliopotezha maisha imefikia 6300. Lakini takwimu zinaweza kuwa za juu kwa sababu maiti bado zinaendelea kuondolewa katika eneo hilo. Al Octaviano, mkazi wa mkoa wa Leyte, alisema kuwa mingi ya miili ya waliokufa hairipotiwi kwa mamlaka:

Mimi binafsi niliondoa miili 14 – watoto wawili, wanawake wanne, wengine walikuwa wanaume. Niliwafunga wote pamoja ili wasibebwe na maji ya bahari, lakini unajua wakati miili imezama katika maji ya bahari, humomonyoka. Pia kuna mifupa mingi iliyozikwa katika matope ya kina, lakini watu hawatoi taarifa tena.

Kwa upande wake, serikali ilikubali kukosolewa kwa kazi yake ya kutoa misaada lakini ilionya dhidi ya wanasiasa ambao wanaitumia hali hiyo kuendeleza ajenda zao za kisiasa:

…Vivyo hivyo Kudanganywa na wale ambao agenda yao ni pamoja na kupotosha watu wetu kuamini kwamba serikali haikuwa makini vya kutosha kupunguza mateso ya waathirika. Sisi tunachukizwa na wanasiasa na makundi ya kisiasa ambayo hujitahidi kuweka vizingiti katika kutumia mazingira magumu ya waathirika wa Yolanda.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.