Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia

Waandishi wa Kimasedonia walilazimishwa kwa nguvu na polisi kufuta picha na video walizokuwa wamezipiga kwenye matukio ya ghasia zilizoibuka wakati wa maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi, hali iliyosababisha kuteketezwa kwa mali kadhaa za umma  kwenye mitaa ya Gorce Petrov jijini Skopje. 

Maafisa wa polisi walianza kwa kuwakamata maandamanaji 27, ambao ni waandishi wa Radio Free UlayaNovaTV, na Focus wanasema wao pia ni shababa ya polisi kwa kuwa wanazo picha za tukio hilo. Polisi waliwasukuma na kuwaburuza waandishi, huku afisa mmoja akifikia hatua ya kuichukua kamera na kufuta kipande cha video yeye mwenyewe. 

Ghasia wakati wa nyakati zajioni za tarehe 19 na 20 mwezi Mei, 2014 zilikuwa ni  mwitikio wa mauaji ya kijana asiye na hatia mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa ndio kwanza amemaliza sekondari baada ya yeye na baba yake kumfukuza mwizi aliyekuwa ameiba baiskeli yao.

Mtuhumiwa kwa sasa aliyeko mahabusu kwa tuhuma za mauaji ni wa asili ya Albania, na wakati ghasia zikisababisha hali ya kutokuelewana kati ya watu wenye asili ya Albania na wenzao wa Kimasedonia waishio Skopje, raia wa Masedonia wenye asili tofauti walitoa mwito kupitia mitandao ya kijamii kuwaomba wananchi wenzao kuwa watulivu na kumaliza hali hiyo.

Mwanaharakati wa Kimasedonia Biljana Ginova aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba watu wote nchini humo wanaugua maradhi ya chuki. Bandiko lake kwenye mtandao wa facebook lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadae kuhamia kwenye vyombo vikuu vya habari.

Треба да сме револтирани оти полицијата која ја плаќаме не нѐ штити, не е на наша страна, таа е само оружје на истите сеирџии кои од фотелјите нѐ гледаат како гинеме 

Tunapaswa kukengeuka kuwa tunawalipa polisi ili wasitulinde, hawako upande wetu na wanatumiwa tu kama silaha na watu wale wale wanaotutazama tukifa wakiwa kwenye viti vyao.

Masedonia ni makazi ya watu milioni 2.1, ambao asilimia 63 wana asili ya Masedonia na asilimia 25 ni wa asili ya Albania. Nchi hiyo ina historia ya misuguano ya kiubaguzi na kutokuvumilia, ya hivi karibuni kabisa ikiwa ni mgogoro uliotumia silaha wa mwaka 2001 kati ya vikosi vya usalama vya Masedonia na waasi wenye asili ya Albania. Hali hiyo ilimalizika kwa  Mpango wa Makubaliano wa Ohrid uliotoa haki kwa walio wachache kwa Waalibania nchini humo. 

Walio wachache waliokuwa miongoni mwa wale walioandamana kwenye mitaa yote ya jiji la Skopje, walifunga mitaa, wakitupa mawe kwa maafisa wa usalama, wakichoma majengo, na wakitoa matusi kwa watu wa asili ya Albania. Polisi waliwatupia mabomu ya machozi ili kuwatawanya, wakati wazee wanaoishi sehemu hizo waliwaomba polisi kutumia nguvu za wastani kupambana na waandamanaji wakisema, “Msiwaburuze namna hiyo!”

prevrteniKontejneriGorce20maj1

Picha ya A1on, imetumiwa kwa ruhusa.

Mwandishi kutoka kwenye chombo cha habari cha mtandaoni kiitwacho NovaTV, Sashka Cvetkovska, aliiambia Radio Free Ulaya kwamba walikuwa wamepewa ruhusa na polisi kupiga picha na kuchukua vieo za ghasia hizo, lakini mambo yanaonekana yalibadilika wakati polisi walipoanza kuwakamata waandamanaji:

Со многу висок тон и речиси насилно почнаа од нас да бараат да ги избришеме сами снимките. Една од колешките ја турнаа, мене ме влечеа за рака, не навредуваа. Јас одбив да ги избришам снимките, не ја дадов камерата, при што едниот од полицајците насилно ми ја одзема и почна самиот да брише 

Walianza kutufuata na kwa kweli ni kama walitumia nguvu kututaka tufute vyote tulivyokuwa tumevipiga kuhusiana na tukio hilo. Mwenzangu mmoja alisukumwa, mimi mwenyewe nilivutwa kwa nguvu mkononi huku nikidhalilishwa. Nilikataa kufuta nilivyokuwa nimevirekodi na sikuwapa kamera yangu, na baada ya hapo mmoja wa maafisa wa polisi aliichukua kwa nguvu na akaanza kufuta kwa mikono yake mwenyewe.

Mwandishi Meri Jordanovska wa tovuti ya Plusinfo alisema walishuhudia polisi wakitumia nguvu wakati wakimkamata kijana na kumweka chini ya ulinzi: 

Го влечеа за земја, го фатија за раце, а кога падна на земја го удрија со клоци. И ние тоа го снимавме и го фотографиравме

Walimkwida kwa mikono, wakamvuta akaanguka na wakaanza kumpiga mateke. Hayo yote tuliyarekodi kwa picha za mnato na za video..

Waandishi walifungua malalamiko kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani dhidi ya ukatili uliofanywa na polisi, lakini waligonga mwamba. Wizara hiyo ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosema:

Од извршените разговори со сите 34 полициски службеници кои учествувале во активностите на полицијата, не може да се утврди дека некој воопшто бил инволвиран во настан како што е наведен во претставката, односно одземање и бришење на снимен видео-материјал и фотографии.

Baada ya kuongea na maafisa wote 34 wa polisi walioshiriki kwenye zoezi hilo la kipolisi, hatuwezi kuthibitisha kwamba wote waliotajwa kwenye malalamiko walihusika kwenye tukio hilo, au walinyang'anywa na kufutiwa picha na video zao.

Mwakilishi wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya Dunja Mijatovic alionyesha kusikitishwa mno na tabia ya polisi hao kwa waandishi waliokuw wakitafuta habari za maandamano hayo jijini Skopje:

Новинарите мора да бидат во можност да  покријат демонстрации слободно и без страв од малтретирање. Секое прекршување на правата на новинарите е јасно кршење на правото на слобода на медиумите и не може да се толерира.

Waandishi wa habari lazima waweze kuandika habari za maandamano kwa uhuru na bila wasiwasi wa kubughudhiwa. Kuvunja haki za waandishi ni wazi ni uvunjaji wa haki ya uhuru wa vyombo vya habari na hali hiyo haitavuliwa.

Umoja wa Waandishi wa Habari Nchini Masedonia vile vile ulilaani vitendo hivyo vya polisi: 

Kushinikiza kufutwa kwa picha na video kulikofanywa na polisi kunaonyesha wazi kuvunjwa kwa Ibara ya 16 ya Katiba inayozuia kufuatiliwa na inayotuhakikishia upatikanaji huru wa habari na uhuru wa kupokea na kusambaza habari. Kwa tabia hii   polisi wamewazuia waandishi kuandika/kutangaza tukio hilo na kujipa jukumu la kufuatilia na kuamua kile ambacho kinaweza kuonwa au kutokuonwa na umma wa Wamesedonia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.