Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu

Hatimaye Misri imepata rais mpya katika uchaguzi wa tatu kufanyika baada ya miaka mingi. Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi alishinda kwa kishindo, akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye amekuwa wa tatu. Baada ya siku tatu za upigaji kura, matokeo ya awali yametangazwa. Sisi ametangazwa kushinda kwa asilimia 93.3 ya kura, wakati Hamdeen akijikusanyia asilimia 3 na asilimia 3.7 zikitangazwa kuharibika.

Kwenye mtandao wa Twita, watumiaji wa mtandao wa twita walipokea habari hizo kwa kejeli na dhihaka.

Mmisri Aida Elkashef anasema [ar]:

Kinachokufanya ucheke na kulia kwa wakati ule ule ni kwamba kwenye uchaguzi huu, uliokuwa na wagombea wawili tu, Hamdeen kawa wa tatu baada ya idadi ya kura zilizotangazwa kuharibika

Sherief Gaber anauliza:

Kwa hiyo kama mwaka 2011 kulikuwa na upinzani, je tunaweza kuita uitikiaji huu mdogo kwa Sisi kuwa ni upinzani kinyume chake?

Na Mmisri Hosam El Sokkari anabainisha [ar]:

Binadamu ni mnyama wa kupiga kura (zaidi ya uwezo huo hana maana yoyote) T

Wakati huo huo, Nabeel anashangaa kwa nini watu wamekasirishwa kwa nini Sabahi hakugombea. Anauliza:

Kwa nini kumbebesha lawama Hamdeen? Kwa sababu amepata kura kidogo? Nani alidhani angeshinda?

Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Sisi, Amro Ali anaonyesha changamoto:

Sisi hataweza kuwa kama Nasser mpaka aweze kupata ushindi wa asilimia 99.9 alioupata Nasser kwenye uchaguzi wa mwaka 1956.

Mwandishi wa mtindo wa dhihaka mwenye asili ya Lebanoni Karl Sharro anaongeza:

Unaweza kusema kuwa Sisi sisi hawezi kupata zaidi ya asilimia 100 ya kura kwa sababu ya uchovu wa kimahesabu tu

Kutoka Bahrain, Abo Omar Al Shafee alifananisha matukio hayo na hali ya mambo nchini Bahrain. Anatwiti:

Kama ambavyo uchaguzi wa rais ulivyofanikiwa nchini Misri, uchaguzi wa wabunge umekuwa wa mafanikio nchini Bahrain. Hakuna faraja kwa wale waliosusia

Na, kwa kuhitimisha, mwanaharati wa Kimisri Alaa Abdel Fattah alitwiti:

Umegeuka na kuwa mjinga sana [Jenerali] Sisi

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.