Habari kutoka 30 Mei 2014
Mwimbaji Mwingine Akamatwa China kwa Kuusifu Utamaduni wa Kitibeti
Kufuatia kukamatwa kwa mwimbaji wa Kitibeti Gepe nchini China,hapa ni mtiririko wa matukio ya jinsi hiyo sambamba na video za nyimbo husika kwenye mtandao wa YouTube.
Rwanda: Mema, Mabaya na Matumaini
Ingawa Rwanda imepiga hatua kubwa katika kuponya majeraha ya mauaji ya kimbari ya 1994, makundi ya utetezi yanaripoti vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu.
Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu
Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi ameshinda urais kwa kishindo, huku akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye ameshika nafasi ya tatu. Baada ya siku tatu za zoezi la upigaji kura, Sisi ameshinda kwa asilimia 93.3 ya kura zote. Hamdeen alipata asilimia 3 wakati asilimia 3.7 zimeharibika.
Je, Madaraka ni Matamu Kiasi cha Watawala wa Afrika Kushindwa Kuyaachia?
Gershom Ndhlovu anaangalia sababu za kwa nini watawala wa Afrika hawataki kuachia madaraka: Kumekuwepo na tetesi, dondoo na hata uvumi kuhusu afya au basi udhaifu wa afya ya Rais wa Zambia Michael Chilufya Sata, aliye madarakani tangu Septemba 2011. Tetesi hizi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba serikali...
Changamoto za Elimu kwa Karne ya 21
Mikel Agirregabiria kwa kujifunza kutoka kwenye filamu Dead Poets Society aliweza kubainisha [es] mahitaji ya sasa ya elimu: Elimu katika karne ya 21 yahitaji kushughulikia masuala ambayo hayakuwa bayana siku za nyuma, kama vile wapi unapotaka kuishi au kufanya kazi, kwa kutumia lugha gani au kwa utamaduni upi unaweza kujisikia...