Mwimbaji Mwingine Akamatwa China kwa Kuusifu Utamaduni wa Kitibeti

Popular Tibetan singer Gepe was arrested after singing in a music concert. Screen capture from YouTube.

Mwimbaji maarufu wa Kitibeti amekamatwa baad aya kuimba kwenye tamasha la muziki. Picha imepigwa kwenye video ya YouTube.

Mwimbaji wa Kitibeti Gepe amekamatwa na kuwekwa kizuizini Mei 24, 2014 kwenye jimbo la Sichuan baada ya onyesho lake kwenye tamasha lililohudhuriwa na maelfu ya mashabiki.

Tamasha hilo, lililoandaliwa na kikundi cha vijana wa Kitibeti, liliruhusiwa rasmi na serikali za mitaa za sehemu hiyo, na kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utangazaji la Marekani, tamasha hilo lilikuwa lina maudhui ya kuonyesha umuhimu wa lugha na utamaduni wa Kitebeti.

Gepe ni mwimbaji maarufu kutoka eneo la Ngaba, Amdo. Mwaka 2012, baada ya kuzindua albamu yake iliyokuwa inaonyesha maumivu ya kutengenana na kiongozi wake wa kiroho na shauku yake kubw aya umoja wa Watibeti, alibaki kimya kwa muda mrefu. Hapa chini unaweza kusikia wimbo wake, “Ninakuja” ukiwa na maandishi ya kiingereza yaliyotafsiriwa na Grey Buffalo:

Gepe si mwimbaji wa kwanza wa Kitibeti kushitakiwa nchini China. Tangu maandamano ya Lhasa mwezi Machi 2008, wasanii wa Kitibeti wamekuwa walengwa wa ukandamizaji wa kisiasa. Mwandishi wa Kitibeti na mshahiri Tsering Woeser alieleza mfululizo wa matukio hayo kama “sera zilezile za Mapinduzi ya Kiutamaduni lakini kwa jina tofauti”.

Mwezi Desemba mwaka jana, Thinley Tsekar na Gonpo Tenzin walikamatwa wilayani Diru. Wawili hao wanaimba kuhusu utambulisho wa Kitibeti, utamaduni na lugha. Thinley alihukumiwa miaka tisa gerezani kwa “kuhamasisha hisia za kuipinga serikali miongoni mwa wasikilizaji wa muziki wake”. Hapa unaweza kusikia nyimbo zake zinazopatikana kwenye mtandao wa YouTube:

Mwezi Aprili 2012, mwimbaji maarufu wa Kitibeti Lo Lo naye alikamatwa baada ya kutoa albamu yake inayoitwa “Pandisheni bendera ya Tibet, enyi wana wa barafu”. Mwimbaji huyo hatimaye alihukumiwa miaka sita gerezani kuanzia mwezi Agosti 2013. Hapa chini unaweza kusikia wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube:

Sehemu ya mashairi ya wimbo yanayosomeka:

Kukuza heshima ya Nchi ya Barafu
Kwa uhuru kamili wa Tibet
Kwa kutambua malengo yetu
Tupandisheni bendera ya Tibet -enyi wnaa wa barafu

Mwezi Machi, 2012, mwimbaji maarufu Ugyen Tenzin alikamatwa bada ya kutoa albamu yake yenye wimbo “Mtiririko Usiokoma wa damu ya Moyo wangu”. Baadhi ya nyimbo zake zimeelekezwa kwa wviongozi wa kiroho ikiwa ni pamoja na Dalai Lama na Karmapa. Hapa chini ni wimbo wake uliobeba jina la albam yake, “Damu ya Moyo Yatiririka”, ukiwa na maneno ya kiingereza yaliyotafsiriwa na “High peaks pure earth”:

Mwaka 2011, mwimbaji wa kike anayefahamika vizuri Hortsang Lhalung Tso aliwekwa kizuizini kabla ya kuhudhuria onyesho la utamaduni wa Kitibeti wilayani Sangchu akiwana waimbaji na wanamuziki wengine maarufu wa Kitibeti. Hapa kuna nyimbo zake kwenye mtandao wa YouTube:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.