Rwanda: Mema, Mabaya na Matumaini

-Paul Kagame, President of Rwanda  at the World Economic Forum on Africa 2009 in Cape Town, South Africa- via wikipedia cc-license-2.0

Paul Kagame, Rais wa Rwanda, akiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Afrika uliofanyika mwaka 2009 jijini Cape Town, Afrika Kusini- kupitia wikipedia cc-license-2.0

Rwanda bado inauguza makovu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyoteketeza maisha ya watu kati ya 800,000 na milioni moja, ikiwa ni asilimia 80 ya idadi ya watu wa kabila la Watutsi ikiwa ni pamoja na Wahutu wengi. Inakadiriwa kuwa sehemu moja ya sita ya idadi ya raia wa nchi hiyo waliuawa ndani ya majuma kadhaa.

Miaka ishirini baadae mchakato wa maridhiano bado una safari ndefu kufikia mafanikio. Rais Paul Kagame anatuhumiwa kuwadhibiti wapinzani wake, moja yapo ya vitendo vingi vya uvunjifu wa haki za binadamu. Lakini jitihada za kujenga upya nchi hiyo zimeanza kuleta matokeo yanayoonekana.

Habari Njema

Moja ya mafanikio makubwa ya nchi ya Rwanda ni kukua kwa usawa wa kijinsia katika maeneo mengi. Idadi ya wanawake kwenye bunge la Rwanda, ni asilimia 64, ambayo ni idadi kubwa kuliko kwenye mabunge mengine duniani, kwa mujibu wa orodha ya 2014 ya Umoja wa Mabunge katika nchi 189.

Louis Michel, waziri wa zamani nchini Ubeligiji na kamishina wa Umoja wa Ulaya, alibainisha kwenye blogu yake [fr]:

Ces résultats sont spectaculaires : en moins de dix ans plus d’un million de personnes ont été sorties de la pauvreté extrême et le pays a enregistré un taux de croissance économique stable de 8% par an. Plus de 95% des enfants ont aujourd’hui accès à un cycle complet d’éducation primaire, la mortalité infantile a été réduite de 61% tandis que les trois quart de la population ont accès à l’eau potable. Enfin, près de 50% des femmes ont accès à un moyen de contraception, ….. Cela fait du Rwanda l’un des très rares pays d’Afrique qui pourra affirmer avoir atteint la quasi-totalité des OMD en 2015. 

Matokeo haya ni ya ajabu: kwa muda usiofika miaka kumi, zaidi ya watu milioni moja wameinuliwa na kuuaga umasikini uliokidhiri na nchi inaonekana kuwa na uchumi imara na unaokua kwa asilimia 8 kwa mwaka. Leo zaidi ya asilimia 95 ya watoto wanapata elimu ya msingi bora, vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 61, na robo tatu ya raia wa nchi hiyo wanapata maji safi. Mwishoni, takribani asilimia 50 ya wanawake wanapata huduma za uzazi wa mpango…hii ikiwa na maana kuwa Rwanda ni moja ya nchi chache za Afrika ambazo zinakaribia sana kufikia Malengo ya Milenia mwaka 2015.

Mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano kwenye eneo la teknolojia mpya [fr], ulibuniwa mwaka 2001, umeonyesha mafanikio makubwa. Wakati wa awamu ya pili ya mpango huo, iliyoishia mwaka 2010, Rwanda ilishuhudia asilimia 8,900 ya ongozeko la watumiaji, ukifananisha na asilimia 2,450 kwenye sehemu nyingine barani Afrika na asilimia 44 duniani. Jarida la African Renewal, linalomilikiwa na Umoja wa Mataifa, liliandika kwamba maeneo manne ya sekta ya umma (mawaziri, mawakala, majimbo na wilaya) na takribani theluthi ya sekta binafsi imeunganishwa na mtandao wa intaneti. Mji mkuu wa Rwanda, Kigali unafanya vyema kwenye maendeleo ya mfumo wa rada na mawasiliano ya anga kwenye eneo lote.

Rais Kagame anashikilia msimamo kwamba “intaneti ni huduma inayohitajika kwa umma kama ilivyo kwenye maji na umeme.” Kwa ushirkiano na kampuni ya mawasiliano ya Rwandan Telecentre Network (RTN), serikali imetekeleza mpango wa maendeleo ya upatikanaji wa huduma ya intaneti katika maeneo ya vijijini. Taarifa [fr] iliyochapishwa kwenye mtandao wa balancingact-africa.com inasema:

Rwandan Telecentre Network (RTN) s’est rallié aux efforts du gouvernement et s’est engagé à créer un réseau national de 1 000 centres TIC d’ici la fin de 2015 et à former du personnel local. 

Kampuni ya Rwandan Telecentre Network (RTN) ikishirikiana na jitihada za serikali, imekusudia kujenga mtandao wa kitaifa wa vituo 1,000 vya teknolojia mpanga ifikapo mwaka 2015 na kuendesha mafunzo ya wataalam wa ndani.

Dalili za maendeleo ya kiteknolojia ni kwamba Rwanda ni nchi yenye mafanikio ya juu zaidi miongoni mwa nchi za Afrika zinazoshiriki kwenye mpango uitwao Kompyuta Moja kwa Kila Mtoto. Kwa mujibu wa ukurasa wa OLPC   :

 Kufikia mwisho wa mwaka 2012, kompyuta 210,000 zimesambazwa kwenye shule 217 nchini kote. Mwaka 2013: Kompyuta 210,000 = 110,000 (kabla ya 2012) +100,000 (2012)[zilisambazwa] nchini 

Habari za Matumaini

Baada ya mauaji ya kimbari, nchi hiyo ilichukua hatua za kisheria, kujenga Tume ya Kitaifa ya Umoja na Maridhiano (NURC). Tume hiyo, iliyoanzishwa mwaka 1999, inakusudia kuchangia kwenye hatua za utawala bora; kukuza mshikamano, maridhiano na ushirikiano wa kijamii miongoni mwa Wanyarwanda; na kujenga nchi ambayo kila mmoja ana haki sawa.

Susan Thomson, profesa wa stadi za siasa za Afrika kwenye chuo cha Hampshire nchini Marekani, aliandika kwenye makala haya [fr] yaliyochapishwa kwenye mtandao wa machapisho ya kitaaluma wa Cairn.info:

Sous la férule du RPF, l’État postgénocide a largement contribué à restaurer la paix, l’unité et la réconciliation aux quatre coins du pays. L’appareil d’État rwandais, solide et centralisé, a facilité une reconstruction rapide. À la différence de La plupart des autres États africains, le Rwanda est capable d’exercer son contrôle territorial avec une efficacité extrême. Les institutions de l’État ont été restaurées. 

Chini ya utawala wa [chama tawala] cha Patriotic Front, nchi hiyo iliyowahi kukumbwa na mauaji ya kimbari imepiga hatua kubwa katika kurejesha amani, umoja na maridhiano nchini kote. Muundo wa serikali ya Rwanda, ulio imara na unganishi, umewezesha mabadiliko ya haraka. Tofauti na nchi nyingi za Afrika, Rwanda inaweza kutumia mamlaka yake ya ndani kwa mafanikio makubwa. Taasisi za kiserikali zimekarabatiwa.

Taasisi ya Amani ya Rwanda (RPA) ni mfano wa maendeleo hayo, Taasisi hiyo mwaka 2009 kwa kutumia misaada ya kifedha kutoka Japan na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, imekuwa na mpango wa kufanya tafiti na kujenga na kutekeleza mafunzo ya kitaalam na mipango ya kielimu inayotambulika kimataifa. Lengo ni kuwajengea ujuzi unaotakiwa watumishi wa jeshi, polisi na watumishi wengine wa umma ili kukabiliana na changamoto zilizopo na masuala ya amani na usalama kwa siku za usoni barani Afrika.

Habari Mbaya

Kwa bahati mbaya, kazi hii inayoleta matumaini imefukiwa kwenye kaburi la ukiukwaji wa haki za binadamu unaoripotiwa na makundi ya utetezi. Vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu zimekuwa vikitokea kwa miaka mingi. Mwaka 2012, baada ya kutuma wajumbe kadhaa kwenye nchi hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International liliishutumu nchi hiyo kwa vitendo hivyo:

Kati ya mwezi Machi 2010 na Juni 2012, Amnesty International ilikuwa na matukio 45 ya kukamatwa kwa wtau kinyume cha sheria na shutuma 18 ya utesaji au vitendo visivyo vya kiungwana kwenye Camp Kami, kambi ya kijeshi ya Mukamira, na kwenye nyumba salama kwenye jiji la Kigali. Wanaume walikamatwa na J2 katika kipindi cha kati ya siku 10 na miezi kadhaa bila kuonana na wanasheria, madaktari na wanafamilia.

Matukio ya kuuawa kisiasa kwa wapinzani [fr] yamekuwa yakiripotiwa nje ya nchi hiyo. Waandishi wa habari na viongozi wa zamani wa kisiasa walio karibu na rais wa Rwanda wamekuwa wakikamatwa na kuuawa [fr]. Matukio ya ukamataji ya hivi karibuni yalithibitishwa mwanzoni mwa mwezi Aprili 2014.

Singer and activist Kizito Mihigo - Public Domain

Mwimbaji na mwanaharakati Kizito Mihigo – Picha kwa matumizi ya umma

Tovuti ya arretsurimages.net [fr] iliripoti kukamatwa kwa mwimbaji maarufu Kizito Mihigo, mhangan wa mauaji ya kimbari, na watu wengine watatu, akiwemo mwanandishi wa habari kwa tuhuma za kupanga shambulizi la bomu kwenye jengo moja jijini Kigali. Kizito Mihigo, hata hivyo, anafahamika kwa uanaharakati wake kwa masuala ya amani. Alianzisha Asasi isiyo ya Kiserikali kwa ajili ya kutoa elimu ya amani. Blogu yake [fr] imeeandika:

Depuis l'année 2003, il a œuvré pour le pardon, la réconciliation et l'unité dans la diaspora rwandaise en Europe. En 2010 quand il est rentré au Rwanda, il a Fondé la Fondation KMP (Kizito Mihigo pour la Paix), une ONG rwandaise qui utilise l'art (musique, theatre poesie, ..) dans l'éducation à la Paix, à la Réconciliation et à la Non-violence après le génocide. 

Tangu mwaka 2003, amekuwa akifanya kazi za kuhamasisha watu kusameheana, kuridhiana na kuungana hususana kwa raia wa nchi hiyo waishio ughaibuni barani Ulaya. Aliporejea Rwanda mwaka 2010, alianzisha Mfuko wa Amani wa Kizito Mihigo, AZISE inayotumia sanaa (muziki, maonyesho, ushairi…) kuelimisha kuhusu amani, maridhiano na kuepuka matumizi ya nguvu baada ya mauaji ya kimbari.

Mwimbaji huyo alipatwa na hatia, lakini mashaka makubwa  [fr] yanazunguka maeneo mengi ya kesi hiyo.

Zaidi, kwa miaka kadhaa iliyopita Kigali imekuwa mahusiano duni ya kidiplomasia [fr] na nchi nyingine kadhaa. Nchi ambayo iliwahi kuwa kipenzi cha nchi za Magharibi, Rwanda sasa imeanza kuwa eneo la kukwepwa na inakosa misaada ya kijeshi [fr] pamoja na ile ya kimaendeleo. Mahusiano ya kidiplomasia na Afrika Kusini yamekuwa mabaya kufuatia mauaji ya kisiasa ya wapinzani waliokuwa nchini humo. Tayari kumekuwa na matukio ya kuwafukuza wanadiplomasia  [fr] katika pande hizo mbili.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.