Mazungumzo ya GV: Ukoaji wa Mafuriko Uliowezeshwa na Watu Nchini SerbiaUngana nasi moja kwa moja kwenye Google Hangout Ijumaa, Mei 22 (saa 9:30 alasiri kwa saa za GMT/UTC)

Nyumba za maelfu ya watu zimefunikwa na maji kufuatia gharika kubwa nchini Serbia. Kimya cha srikali kimesabbaisha watu kujitafutia namna ya kujisaidia wenyewe, lakini kwa bahati mipango inayoanzishwa na watu wenyewe imesaidia kuwapatia misaada na jitihada za kusaidia kuuhabarisha umma zinaongezeka. Wakati huo huo, mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, na hata watu maarufu wanajikuta wanatishwa na mamlaka kwa “kusababisha tahayaruki” wakati ambao upatikanaji wa habari sahihi ndio unaohitajika. Nini kinaendelea?

Kwenye mazungumzo ya GV juma hilo, tunazungumza na marafiki waishio Serbia akiwemo Mhariri wetu wa Ulaya ya Kati na Mashariki Radisic ili kuelewa hali ya mambo kwa mtazamo wa wenyeji kuhusu habari hizo.

Pia tazama:
Maelfu wakwama, Waserbia waamua kujiokoa kwa mikono yao wenyewe

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.