Wanawake Watatu Wauawa katika Maandamano ya Kumtetea Morsi

Wanawake wasiopungua watatu wameuawa kwa kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huko Mansoura wakati wa maandamano ya kupinga kung’olewa madarakani kwa aliyekuwa Rais wa Misri Mohamed Morsi. Inmeripotiwa pia kuwa, zaidi ya makumi mawili ya watu walijeruhiwa kwa risasi na visu.

Mwanablogu wa Misri, Zeinobia aonesha kushitushwa na tukio hili:

Na @egyrevolution12 anaongeza [ar]:

Maandamano ya Ikhwan huko Mansoura huanza mara baada tu baada ya sala na nusu yao huwa ni wanawake. Wote wanaowashambulia hawawezi kuvumiliwa kamwe.

Ibrahim Elgarhi anashangazwa na wote wanaowahurumia wauaji. Anaandika:

Tuuze thamani yetu na kufumbia macho mauaji ya wanawake. Hebu tupingane na dhamira zetu na tutafakari kile kilichowafanya wanawake hawa waungane na wenzao kwenye maandamano

Tarehe 30 Juni, raia wa Misri waliandamana wakishinikiza kuondoka madarakani kwa kiongozi wa Chama cha Kindugu cha Kiislam (Muslim Brotherhood0na Rais wa Misri Mohamed Morsi. Juni 3, Serikali ya Morsi iliondoshwa madarakani na kupelekea nchi hiyo hadi sasa kuongozwa kwa serikali ya mpito. Tangu kuondolewa madarakani, wafuasi wa Morsi wamekuwa wakifanya maandamano kushinikiza arudishwe madarakani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.