Zaidi ya wanablogu 60 wa Ki-vietinam walitia saini tamko la pamoja kuitaka serikali ya Vietnam kuboresha rekodi ya haki za binadamu na ahadi wanapowania uanachama katika Baraza la Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu:
Serikali ya Vietnam pia inahitaji kutathmini hali ya haki za binadamu katika nchi hiyo na wa-Vietinamu pia wana haki ya uhuru wa maoni na kujieleza, ikiwa ni pamoja na masuala haya.
Kama watetezi wa uhuru wa kujieleza nchini Vietnam na wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa sababu ya harakati zetu, sisi twaona mgombea Vietnam kwa Baraza la Haki za Binadamu kama jukwaa kwa ajili ya majadiliano ya kujenga haki za binadamu katika nchi yetu.