Ethiopia: Wanablogu walitetea Shirika la Ndege la Ethiopia baada ya ajali ya ndege

(Ilichapwa kwanza kwa Kiingereza tarehe 26 Januari 2010)
Wanablogu waishio Ethiopia wameharakia kuitetea rekodi ya usalama wa safari za ndege za nchi hiyo siku ya Jumatatu baada ya ndege moja kuanguka karibu na Beirut, ikihofiwa kupoteza maisha ya watu wote 90 waliokuwepo.

Owen Abroad alisema “alikasirishwa sana” na habari katika posti ya Shirika la Ndege la Ethiopia, akiongeza:

Shirika la Ndege la Ethiopia lina rekodi ya nhali juu ya usalama. Wafanyakazi wake ni wataalamu, wenye ari na wafanisi. Nitasafiri kwa ndege kutoka Uingereza kwenda Addis siku ya Ijumaa kwa Shirika la Ndege la Ethiopia na, pamoja na balaa la leo, bado ninatarajia (safari).

Mtoa maoni kwenye blogu hiyo alikubaliana naye, akiandika:

Nimesafiri nazo (ndege za Ethiopian Airlines) mara kadhaa, na sijawahi kukutana na uzoefu mbaya. Pia wana utaratibu mzuri wa kubadikili tarehe kuliko mashirika mengine ya ndege.

Kero mbili juu ya namna tukio hilo lilivyoripotiwa na vyombo vya habari nchini Uingereza

Wakati ajali hiyo ilipotangazwa kwa mara ya kwanza katika vyombo vya habari, tuliambiwa kwamba kulikuwa na Waingereza wawili, raia wa Canada mmoja na raia wa Ufaransa mmoja. Kiuwazi kabisa watu wa mataifa mengine si wa muhimu wala kuvutia hisia.

Pili:- Mtaalamu wa safari za anga aliulizwa mara kadhaa kuhusu rekodi ya usalama wa Mashirika ya Ndege ya Afrika, na ilibidi ajibu maswali kadhaa kuhusu kiwango bora cha safari za anga za Shirika la Ndege la Ethiopia (hasa hasa umri wa ndege zenyewe). Sikumbuki maswali kama hayo kuulizwa bada ya kuanguka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, Air France kiangazi kilichopita.

Mwandishi wa habari wa Reuters aliyeko Addis Barry Malone aliandika posti kwenye blogu ya shirika hilo iitwayo Africa News Blog yenye kichwa cha habari Kuanguka kwa ndege ya Kiethiopia kusipake matope habari za mafanikio:

Habari za kuanguka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia zilipotapakaa asubuhi ya leo moyo wangu ulisinyaa kwa mawazo ya kuelezea habari nyingine mbaya kuhusu Ethiopia.

Kwa hakika inakera sana kwa Waethiopia kwamba shirika la ndege ni moja ya mafanikio adimu ya kimataifa ya nchi hii inayofahamika kwa njaa na vita.

Habari zilipojitokeza nilifahamu mara moja namna gani wafanyakazi wa shirika hilo wangezichukulia. Nimewahi kuwepo kwenye maeneo yanayofanya kazi kama makao makuu ya shirika la ndege linaloongoza Afrika mara kadhaa. Mara ya mwisho ilikuwa juma lililopita nilipoongea na Mkurugenzi Mtendaji Girma Wake na nikaondoka na zawadi ya kahawa ya Ethiopia na picha niliyoipata ambayo ni nadra sana kuona watu wenye upendo na kujivunia kazi yao na kile inachokitenda kwa ajili ya nchi yao.

Nazret.com inatoa habari za hivi karibuni kuhusu ajali hiyo kadri habari hii ilivyoendelea hadi leo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.