Je, Ghana Ipo Tayari kwa Upigaji Kura wa Kwenye Mtandao?

Tukio la siku mbili lililoanza jana; linaratibiwa na Taasisi ya Danquah (DI), kituo cha kutafakari sera, utafiti na uchambuzi, kutengeneza jukwaa la kitaifa kwa washikadau kuongoza majadiliano kuhusu uwezekano wa uanzishwaji wa kuandikisha wapiga kura kwa njia za vipimo vya kibaiolojia na hatimaye mfumo wa upigaji kura kwa njia ya mtandao nchini Ghana.

Taasisi ya Danquah kimesifu mafanikio makubwa ya matumizi ya mtandao kwa upigaji kura katika nchi ya demokrasi kubwa zaidi duniani na kutoa wito kwa Tume ya Uchaguzi ya Ghana kuangalia faida nyingi za kupiga kura kwa njia ya mtandao kama iliovyooneshwa kwenye uchaguzi wa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mheshimiwa Haruna Iddrisu, Waziri wa Mawasiliano,

ingawa utekelezaji wa uandikishaji wapiga kura wa kwa njia za vipimo vya kibaiolojia unaoratibiwa na Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa na upigaji kura wa mtandao ungeweza kutumika katika kipindi kirefu kijacho, mchakato huo haungeweza kuanza kutumika hivi karibuni”.

Aliongeza pia:

“Vyama vyote vya siasa vimesisitiza uandikishaji kwa njia za vipimo vya kibaiolojia, ambao ni mwanzo wa upigaji kura wa mtandoni na tunachofanya hapa leo kitatusaidia kurekebisha mchakato wa uchaguzi katika siku zijazo, lakini hatuna miundo mbinu inayohitajika kwa utekelezaji wa kasi wa miradi yote muhimu katika kipindi kifupi”.

Kwa hiyo, serikali ni lazima iendelee kutafiti zaidi kwenye utekelezaji wake ifikapo mwaka 2016 na sio mwaka 2012.

Musah Yahaya Jafaru kutoka Graphic Ghana pia amearipoti tukio hili na alikuwa na haya ya kusema;

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi; Dk. Kwadwo Afari Gyan alisema; “Kama serikali haitaeulimisha umma pamoja na mama yake kikongwe aliyeko kijijini kuhusu faida za upigaji kura wa mtandaoni na namna ya kuutumia, hatauunga mkono”.

Pia alisisitiza;

Mpaka tuwafanye watu waridhike na matumizi ya tarakilishi, hatuwezi kuanza upigaji kura wa mtandaoni”.

Dk. Afari-Gyan alisema hata katika nchi zilizoendelea kama Uingereza, Canada na Australia hazikuchagua njia ya upigaji kura wa mtandao na akashangaa kwa nini Naijeria na Kenya zinataka kuanza upigaji kura wa namna hiyo”.

Alieleza ongezeko la matumizi ya fedha kwa wanasiasa katika kutafuta madaraka, umuhimu unaotiwa chumvi wa vyama vya siasa, na ushirikishwaji wa vijana kwenye ghasia za uchaguzi, ahadi za ajabu wakati wa kampeni na matumizi ya vyombo vya habari kuchochea vurugu kama baadhi ya mielekeo inayotia hofu wakati wa chaguzi za nchi hiyo. Alisema kwa kiasi kinachoongezeka watu wanasaka nafasi za madaraka si kwa ajili ya kuwatumikia watu bali kimsingi kama njia rahisi ya kujipatia umaarufu, ushawishi na utajiri.

Katika Tamko kwa vyombo vya habari la Taasisi ya Danquah lenye kichwa cha habari: Demokrasia ya Ghana bado haijafika, Upigaji kura wa mtandao unaweza kutufikisha huko.

Hayford kutoka Sydney, Austarlia alitoa maoni:

“Ninajisikia fahari kama Mghana kwamba nchi ina watu wenye kiwango cha juu cha uelewa. Ninakubaliana na mapendekezo hayo hapo juu. Kama kweli Tume yetu ya Uchaguzi inataka mfumo wa upigaji kura unaoaminika na wenye sifa nchini Ghana, basi nadhani tume ni lazima iongoze mawazo yaliyowekwa hapo juu. Ninataka kuiomba Tume ya Uchaguzi kutokupuuza mfumo wa upigaji kura wa mtandaoni lakini itumie nguvu zake kwenye mfumo huu. Wanawake wetu, watoto na masikini wanasitahili kuepushwa na hofu, wasiwasi na ugumu unaohusiana na mfumo uliopo unaoweka uwezekano wa hali kama ya Kenya.”

Kwa mtazamo wangu wa dhati na uzoefu wangu wa kufanya kazi na Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa inayoandikisha watu ili kutengeneza taarifa za Waghana wote, ninaunga mkono ushauri wa kamishna wa Tume ya Uchaguzi katika mada hii.

Swali langu ni; Je, Ghana kweli iko tayari kwa upigaji kura wa mtandaoni?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.