Upinzani Waongezeka dhidi ya Mapendekezo ya Tanzania na Zambia katika Makubaliano ya CITES

Pembe ya ndovu iliyovunjika iliyopatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Hwange nchini Zimbabwe, Na Terry Feuerborn

Pembe ya ndovu iliyovunjika iliyopatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Hwange nchini Zimbabwe, Na Terry Feuerborn


Upinzani unaongezeka dhidi ya mapendekezo ya Zambia na Tanzania ya kuruhusiwa na Makubaliano ya Biashara ya Kimataifa ya Makundi ya Mimea na Wanyama Walio Katika Hatari ya Kutoweka (CITES), kuuza hifadhi ya pembe za ndovu walizonazo.
Huku Kenya ikiwa mpinzani wa muda mrefu wa biashara yoyote ya pembe za ndovu, haistaajabishi kwamba upinzani mwingi unatoka kwenye makundi yenye kutetea hifadhi katika nchi hiyo. Kwa kuongeza, Kenya imehuisha shinikizo lake la kuwa na katazo la miaka 20 ya kutokuuza pembe za ndovu baada ya pendekezo kama hili kusababisha kushinikiza katazo kuwa la miaka 9 baada ya mwaka mmoja (2008) wa kupiga mnada pembe zilizopo katika nchi nne za kusini mwa Afrika. Vyombo vya habari vya Kenya vimeichukua habari hiyo. Kituo cha NTV Kenya kina video kwenye YouTube yenye jina Wildlife Worries, yaani Hofu ya wanyama pori.

Blogu ya Baraza ilichapicha maudhui ya makubaliano hayo ambayo Zambia na Tanzania imeyaleta pamoja na pendekezo la Kenya la kuupinga. Maina anaelezea kwenye Baraza

Kwa upande mmoja ni ukanda wa nchi zinazopinga biashara ukijumuisha Kongo, Ghana, Kenya, Liberia, Mali na Sierra Leone. Kwa upande mwingine, kila mmoja ikiwa na pendekezo lake ni Zambia na Tanzania, ambazo zinataka kuruhusiwa kuuza hifadhi ya pembe za ndovu zilizonazo kwa mkutano ujao wa Doha Machi 13-25 –mkutano wa 15 wa CITES. Pande zote zimetuma mapendekezo kwa sekretarieti ya CITES ba sekretarieti imekuwa na uungwana kwa kuweka mapendekezo hayo kwenye wavuti yao.

Katika posti nyingine kwenye blogu hiyo ya Baraza, Paula anaandika kuhusu kusudio la Uingereza la kupiga kura ya kupinga mapendekezo yote mawili:

Uingereza imesema hapana kwa uuzaji wa pembe za ndovu. Waziri wa Mazingira Hillary Benn alisema usiku wa jana: “Katika mkutano wa CITES mwezi Machi, Uingereza itapiga kura kupinga mapendekezo hayo kutokaTanzania na Zambia ya kuuza pembe za ndovu, na tutazitaka nchi nyingine kupiga kura ya kupinga uuzaji huo.

Paula anaandika kwenye blogu mpya ya WildlifeDirect iitwayo Ban Ivory -inayojitoa mahususi kupiga kampeni kupinga pembe za ndovu- akiuliza “Je, tembo wanathamani kuliko meno yao?”. Anauliza: “Je, tembo ni chanzo tu cha bidhaa ya thamani, pembe zake? Au, je, tembo wanastahili kutendewa kwa upekee?”

Paula anasema kwamba pamoja na kuungwa mkono ambako Waafrika wanakutegemea kutoka nje, vita kwa ajili ya tembo itabidi ianze na Waafrika wenyewe. Anasema:


Mwisho wa siku maandamano upinzani dhidi ya biashara ya pembe za ndovu itabidi uongozwe na Waafrika ikiwa ulimwengu uliobaki utatakiwa kuona kile kinachoifanya kampeni ya Kenya kuwa na nguvu. Lakini ikiwa Wachina na Waasia wengine wataendelea kuwa masoko ya pembe za ndovu na kukataa kufanyia kazi makubaliano ya ndani, katazo hili jipya kwa biashara ya pembe litashindwa na tutaendelea kupoteza tembo.

Kikundi kinachojulikana kama Jukwaa la Ndovu Kenya kinaongoza jamii ya kiraia ya Kenya katika upinzani dhidi ya biashraa ya pembe za ndovu na yameandaa maelezo muhimu kuhusu suala hilo. Harvey Coroze, anayeblogu kwenye blogu ya Mfuko wa Amboseli kwa Tembo anasema:

Asasi ya ATE inapinga biashara hiyo. Tumekuwa tukifanya kazi na AZISE pamoja na watu wenye msimamo uanaoshabihiana chini ya mwamvuli wa Jukwaa la Tembo Kenya (KEF) kutoa taarifa za kimkakati kwa vyombo vya nchi za Afrika zenye tembo vinavyoitwa Umoja wa Tembo Afrika (AEC).

Katika makala hii ya blogu yake, Harvey ameweka viungo vya maelezo muhimu kuhusu suala hilo ya KEF ambayo unaweza kutaka kuyasoma ili kuona tatizo la pembe za ndovu na maana ya mapendekezo ya Tanzania/Zambia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.