Nijeria: Baada ya miezi miwili bila uongozi, kaimu Rais mpya


Tarehe 23 Novemba, 2009, Rais wa Naijeria, Umaru Musa Yar’Adua aliondoka nchini bila kusema hadharani ni lini angerudi. Katika majuma yaliyofuata, habari zilitolewa na kusema kwamba alikuwa akipata matibabu nchini Saudi Arabia, bado ubashiri uliendelea, ukijikita kwenye tetesi kwamba Rais anaugua majeraha ya ubongo au hata amefariki. Tarehe 12 Januari, Yar’Adua alihojiwa kuthibitisha kwamba alikuwa hai na akipata matibabu, ingawa hakusema ni lini hasa angerudi Naijeria.

Kutokuwepo kwa Yar’Adua kulisababisha ombwe la kiuongozi ambalo liliwasumbua Wanaijeria wengi, hasa wakati ambao matatizo yalijitokeza kama pale Umar Abdulmutallab alipofanya jaribio la ugaidi na mgogoro wa kidini katika mji wa katikati ya Naijeria wa Jos. Wanaijeria wengi walitoa wito kwa Makamu wa rais Goodluck Jonathan kuvaa viatu vya Yar’Adua, lakini hali ilikuwa tata: Kama mtu anayetoka Kusini, kukaimu madaraka ya Urais kwa Jonathan kungehatarisha kudhoofishwa kwa mpango wa kuachiana madaraka kati ya maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Naijera. Zaidi, bila maelekezo ya kiamandishi kutoka kwa Rais yeye mwenyewe, uhalali wa nafasi ya Jonathani kisheria ungekuwa haueleweki vyema.

Kwa zaidi ya miezi miwili wanablogu wa Najieria walilalamikia pengo hili la kiungozi. Chinedu Vincent Akuta kwenye Briefs from Akuta aliandika:

Ombwe la kimadaraka limetosha sasa, karibu na mgogoro wa kikatiba, na kuchemka kwa machakato wa kiserikali yote yalikuwa ni kwa sababu chama tawala (PDP) hakimwamini Makamu wa Rais (Janathan Goodluck) kukaimu rasmi Urais mpaka Rais Yar’Adua atakapopona ugonjwa wake. Hakuna uamuzi mwingine zaidi ya kuheshimu matakwa ya watu wa Naijeria, nguvu ni ya watu wenyewe.

Na kwa hakika, Wanaijeria wengi walikuwa na maoni kama yake. Wakati wote wa mwezi wa Januari Wanaijeria waliochanganyikiwa (na hali hiyo) waliandamana kwenye miji ya Lagos, Abuja na London. Adeolu Akinyemi aliandika juu ya kwa nini waliandamana:

Hatuna furaha na watu 300 kufa kwenye mitaa ya Jos kwenye vita vya kidini kwa sababu ya kutokuwepo hatua zinazochukuliwa kwa sababu tu hakuna kiongozi.

Imetosha sasa basi!

Hatutakubali kubandikwa alama ya ugaidi kwa sababu ya siku 58 za kutokufanya kazi kwa simu ya kiganjani ya Rais.

Imetosha sasa basi!

Ombwe la uongozi ni hatari na linawajibika kwa mauaji ya eneo la kaskazini, utekaji nyara mashariki ya nchi, magenge ya wanajeshi kubaka watu kusini mwa nchi na tofauti za kiufahamu zilizoko magharibi.

Imetosha sasa basi!

Yusef, mtoa maoni kwenye blogu ya Akinyemi, alikuwa si mtu rahisi kuamini (imehaririwa kutoka kwenye toleo halisi la kiiingereza):

Mara ngapi nitasoma mstari huu maarufu “Imetosha sasa basi”?????

Ni ajabu namna tunayoonyesha unafiki wa hali ya juu tunapokabiliwa na hali ngumu na bado tukawa na uwezo wa kugeuka mara moja hali ya hewa inapoharibika. Kama nitamwomba yeyote kufanya kile kitakachokuwa muhimu sana kuufanya mfumo wetu ufanye kazi, nitakuwaje na uhakika wa asilimia mia kwamba [mimi] ninayenatokea kaskazini, hatabadili akili yake mara moja anaposikia suala lenye mantiki limesemwa kwake na mtu wa kabila lake…Au kwamba [mimi] kwa kuwa Mwislamu na yeye kuwa wa imani nyingine, hataniona kutokea kwenye kilindi cha moyo wake, kwa kule kuwa adui.

Hakuna kitu kama “Imetosha sasa basi!” Deolu. Hatujui maana ya taifa bado, bila hata kuzungumzia undugu. Haitoshi kubandika mabango ya Ernesto Che kwenye kuta zake ukadhania kutafakari ama kuelewa kile kinachostahili kufanywa ili kuachana na yote ili kuwa na siku njema. Hatuijui hali hii ngumu…au tu wabinafsi sana kiasi cha kudhania kwamba “siku moja kila kitu kitakwenda vyema kwa upande wetu”!!!!

Hawa wanaoitwa viongozi wetu hawakushuka kutoka kuzimu, lakini wanaakisi jamii yetu. Chukua nafasi yao[kwa yeyote kati yao] hata wewe mwenyewe na utashangazwa na kile ambacho ungefanya au ungekuwa.

Mwandishi Maarufu wa utangazaji Funni Ayanda pia aliandika kuhusu mkanganyiko wa hali iliyopo ya kuvutana mikono kimya kimya:

Nimekaa kati ya Wakurugenzi Waendeshaji wa benki waliokwapua mabilioni ya fedha, viongozi wa chama tawala wanaoharibu michakacho ya uchaguzi na kuiba maibilioni ya naira, wachungaji wa makanisa mkubwa yasiyotozwa kodi ambako wote hapo juu wanalipa kiasi kikubwa sana cha mafungu ya sadaka na michango na kusikiliza bila kuamini namna wote hao wanavyolalamika kuhusu uongozi mbaya na hali ya Naijeria. Nimeangalia mara nyingi kwa tafakuri kwenye meno yangu kama kuna mabaki ya mboga za majani; labda nafanyiwa utani mimi mwenyewe?

Kwa hiyo sitaki kuhitimisha kwa kukakakaka ninauliza maswali rahisi kama vile, “kwa hiyo unafikiri tufanyeje” kile kilichopo kwenye uwezo wetu na kwa namna gani tutaweza kuendeleza kutokea hapo? “Nafasi yangu itakuwa nini kwenye hilo?” Mara nyingi, mazungumzo huwa hayafiki mbali kwa sababu mara nyingine mimi hufikiri Wanaijeria na watu wa mataifa ya nje wana mvuto wa huzuni katika na kushindwa kwa Naijeria ambako hakuwezi kukanwa.

Tarehe 9 Februari, baada ya majuma kadhaa ya mivutano ya siasa, Baraza la Seneti lilimthibitisha Jonathan kama kaimu Rais. Wanablogu wengi wameliona tukio hilo kama sababu ya kusherehekea. Solomonsydelle wa Nigeria Curiosity alitoa uchambuzi mzuri sana wa hali ya mambo kama ilivyojionyesha (angalia hapa kwa alichokiandika). Aliandika:

Februari 9 ingeweza kwenda kwenye historia kama siku ambapo hatua za kidemorasia za kisiasa zilichukuliwa kuifanya Naijeria kupiga hatua moja bele kuelekea kwenye njia ya kufanyika taifa la kidemokrasia ya kweli.

Akin, pia, alikuwa na matumaini yenye masharti:

Labda na labda tu, tunaweza kuwa na Rais mwema na bahati njema kwenye jina lake litaleta bahati njema kwa Naijeria, labda, tunaweza kutumaini, labda, tunaweza kuota, labda, tunaweza kutegemea, labda, tunaweza kuipata –Naijeria mpya.

Lakini wengine wanaona sababu ya kuangalia, wakionyesha kwamba ingawa kukaimu madaraka kulikofanywa na Jonathan kunaweza kuwa na umuhimu wa siasa, haikuwa imeruhusiwa moja kwa moja na Katiba ya Naijeria. Max Siollum alijumuisha hali hiyo mbaya kama ifuatavyo:

Kuthibitishwa kwa Jonathani kama Makamu wa Rais kunaweza kumaliza utata (angalau kwa muda), na kutaupa uongozi namna fulani ya uwepo kwa taratibu na michakacho inayokubalika. Wakati tumefikia kwenye suluhisho la KIHALISIA, sina uhakika kama suala hili na hali ya mambo iliyomteua Jonathan kuwa Makamu wa Rais ilikuwa kwa MUJIBU WA SHERIA.

Jide Salu anakiri kuwepo kwa utata wa kikatiba, lakini kimsingi alikuwa na shukrani kwamba nchi hatimaye ina mtawala.

Ninahitaji amani na mwelekeo. Kama ulikuwa unakaa nchini, ungeweza kuelewa zaidi. Naijeria si tu kuwa haikuwa na kiongozi, ilikuwa bila uelekeo pamoja na mitikisiko yote iliyopitia na inayoipitia. Ambayo kwa sasa iko chini ya mfuniko.

Ana Nimmos alikuwa na matumaini, lakini aliona sababu ya kuangalia:

[Utatuzi wa kisiasa] hauwezi kuwa mwisho wa kukingana kwa magogo kama kunavyoonyesha changamoto zake. Kwa mfano, kwa utatuzi huu –kama tutaukubali kwa sababu ya majadiliano –Naijeria kwa sasa inayo marais wawili –japokuwa mmoja ndiye anayefanya kazi. Yar’adua hajawahi kuacha madaraka na Goodluck itabidi awe makini na hatua anazozichukua.

Loomnie pia aliyaonyesha maswali yasiyo na majibu kwa mustakabali (wa nchi hiyo):

Mtu lazima afikiri kuhusu mashine ambayo ilikuwa inatawala nchi mara tu baada ya Yar’dua kutokuwepo. Je, Rais mpya Goodluck Jonathan ataweza kuwa na uwezo kuishughulikia mashine hiyo? Je, ataweza kuiweka pembeni/nazo? Hayo ni maswali ya msingi katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.