Misri: Mwanablogu apoteza kazi kwa kufichua ukweli kuhusu habari ya bikra za bandia

Wakati kuvuja damu kwenye usiku wa harusi bado ni ushahidi wa heshima ya bibi harusi nchini Misri na nchi za Mashariki ya Mbali, Radio Uholanzi imetangaza tafsiri ya Kiarabu ya tangazo la Kichina la Kifaa cha Ngozi nyembamba ya kutengenezwa yenye kurudisha ubikra wa mwanamke. Gazeti la Youm7 lilitangaza kwamba bidhaa hiyo itapatikana kwenye soko la Misri kwa ajili ya LE 83. Na kama vile wanawake wote wa Misri walikuwa wakiungoja muujiza huo wa bikra ya kutengeneza, wabunge wahafidhina wanataka bidhaa hiyo ipigwe marufuku na mwagizaji yoyete afukuzwe ama kukatwa kichwa. Wamisri wameanza kujiuliza ikiwa Misri itaanza kuingiza ‘vijingozi hivyo vya bikra’ na Amira Al Tahawi, ambaye alikuwa akifanya kazi na Radio Uholanzi kwa wakati huu, alifukuzwa kazi kwa kupuliza kipenga dhidi ya habari hiyo ya ‘bikra ya Kichina.’

Katika blogu yake Amira Al Tahawi aliandika:

Ndio! Nilifukuzwa kazi kwa ajili ya posti ya blogu yangu niliyoiweka mwezi Desemba! Tarehe 26 Januari, 2010, nilipokea barua ya kusitiza ajira yangu kuhitimisha kazi yangu kama mwandishi wa Kairo wa Radio Uholanzi. Katika posti yangu nilionyesha kwamba kituo hicho kilikuwa kimetangaza habari za uongo zisizodhibitishwa tarehe 22 Agosti, 2009 kuhusu kuingizwa kwa ‘Bikra za kichina’ katika nchi za kiarabu. Kutangazwa kwa taarifa hiyo kwenye redio ilidai kwamba bikra hiyo bandia ilikuwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya wanawake wa Kiarabu na Waislamu ikipuuza ukweli kwamba bidhaa hiyo imekuwapo Japan tangu mwaka 1993 na haikuwa imetengenezwa maalumu na Wachina waliogundua ugonjwa wa akili wa wanawake wa Kiarabu wanaohitaji kudanganya kuhusu ubikra wao. Nilikiomba kituo hicho cha redio kurekebisha makosa hayo ya kiuhalisia kwa habari hiyo ya kutengeneza kwa njia ya barua pepe ya tarehe 14 Septemba. Maombi yangu yaliangukia kwenye masikio yasiyosikia na watunza habari wa mtandaoni wa Kimisri walisambaza zaidi uongo huo bila kujali kuchunguza ukweli au kunukuu chanzo cha habari.

Wanablogu wengi wameuona uamuzi huo wa kumfukuza kazi kama wa kijinga na usiweza kuhalalishwa; Nawara Negm alijiuliza:

Kwa nini wanamfukuza kazi? Hakuandika chochote kwa madhumuni ya kuishambulia Redio Uholanzi. Anawashtaki…hebu na tumwonge mkono jamani!

Eman Hashim analalamikia uadilifu wa uandishi wa habari; anaandika:

Uandishi wa Habari nchini Misri umeingiliwa na watu wanaoitwa waandishi wa habari ambao kazi yao ni kutengeneza habari kwa kutumia maelezo ya watumiaji wa Facebook. Amira amefukuzwa kazi na amenyimwa haki zake za fedha na maadili kwa sababu alisema HAPANA! Amira aliandika kwa kina kwenye blogu yake kwa hiyo hebu na tumpe sauti kubwa zaidi ili kila mtu aujue ukweli. Tunawalaumu wakimya kwa ukimya wao lakini tunawadai wale wenye sauti kwenye kipaza sauti. Je, hivyo ndivyo Radio Uholanzni wanashughulikia habari za uongo? Uko wapi uadilifu wao? Iko wapi heshima yao kwa wasomaji na wasikilizaji wao? Wangeweza kirahisi tu kutangaza marekebisho au jambo fulani…chochote kile. Ukweli kwamba hawakutangaza ufafanuzi au uthibitisho wa lolote katika hili unasikitisha lakini kumfukuza kazi mwandishi mwaminifu kwa kuibua mkanganyiko wa hoja ni kitendo cha mzaha.


Dkt. Mostafa El Nagaar
aliandika katika utetezi wa Amira akisema:

Amira sasa anaathirika na matokeo ya utaaluma na uthamani wake. Analipia gharama kubwa sana kwa uandishi wenye maadili. Anahitaji mtu kumtetea kwa namna alivyowatetea wasichana wa Kimisri wakati waongo walipodai kwamba wanasubiri kudanganya kuhusu ubikra wao ili kufunika ukosefu wao wa kimaadili. Ninatoa wito kwa kila mwanamke Mmisri kurudishia fadhila kwa kumtetea Amira aliyepoteza kazi. Ninayaomba mashirika yote ya Haki za Wanawake kuonyesha mshikamano wao na Amira. Tunaomba rasmi tamko lililo wazi la kuomba msamaha kutoka kwa wale waliotupaka matope na ninawaomba wote wanaozungumza kwa jina la heshima kuonyesha ushirikiano wao.


Mostafa Fathi
pia aliweka makala yake kwenye Facebook na Karim El Beheiry akaiweka posti hiyo kwenye blogu yake kushikamana na Amira.

Mwezi Oktoba 2009, Mohamed Al Rfahal aliagiza kikabrasha chenye bikra hiyo na kuweka picha kwenye blogu, kama ilivyoonekana kwenye habari zilizopita za Global Voices.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.