India: Gazeti pekee duniani linaloandikwa kwa mkono

Magazeti ya mwanzo [1]yalikuwa yakiandikwa kwa mkono ‘Inawezekana kwamba hivi sasa gazeti la ‘The Musalman [2]‘ pengine ndiyo pekee lililobaki linaloandikwa kwa mkono ulimwenguni. Gazeti hili linalochapishwa kwa lugha ya Ki-Urdu lilianzishwa mwaka 1927 na Chenab Syed Asmadullah Sahi ambapo hivi sasa linachapishwa kila siku katika jiji la Chennai huko India tangu kuanzishwa kwake.

Anayeliendesha hivi sasa ni mjukuu wa Syed Asmadullah anayeitwa Syed Arifullah. Anasaidiwa na wataalamu wa miandiko wapatao sita ili kuchapisha gazeti hili la kurasa nne kila siku. Huku likichapisha idadi ya nakala zipatazo 23,000, gazeti hili huchapisha habari mbalimbali zikiwemo zile za siasa, utamaduni na michezo katika lugha ya Ki-Urdu.

Kufuatia maendeleo ya kiteknolojia siku hizi, ambayo yanasababisha magazeti katika muundo unaobebeka kuanza kupotea, na watu kusoma zaidi magazeti kwenye mtandao wa internet, uwepo wa gazeti hili ni tunu ya pekee. Gazeti hili huuzwa kwa Paise 75 (kiasi cha kama senti 2 za dola, au Sh40).

Signboard of the office. Screenshot from the video The Musalman

Bango la ofisi ya gazeti. Limechukuliwa kutoka kwenye video za The Musalman

MadanMohan Tarun [4] anaripoti kwamba:

Hivi sasa mhariri wa gazeti hilo ni Wb. Syed Arifullah. Alichukua nafasi hiyo baada ya baba yake kufariki dunia. Baba yake aliliendesha kwa miaka 40. Lilianzishwa na kupewa muundo na babu yake mwaka 1927. Gazeti limeendeleza mwonekano wake wa asili na halikupokea mabadiliko ya mwandiko wa kompyuta ya Ki-Urdu. [..]

Maandalizi ya gazeti huchukua takribani saa tatu kila siku. Baada ya habari kupokelewa katika lugha ya Kiingereza kutoka kwa waandishi ambao wako kwenye ajira ya muda, inatafsiriwa katika lugha za Ki-Urdu na Katibis – wataalamu wa mwandiko, wanaoenzi mwandiko wa toka zama za kale wa Ki-Urdu, wanaindika habari yote kwa mkono. Baada ya hapo, nakala hasi ya gazeti zima lililoandikwa kwa mkono inapelekwa kiwandani tayari kuchapigwa chapa..

Afsar Shaheen [5] anaandika maoni kwenyehref=”http://luthfispace.blogspot.com/2011/05/musalman-and-its-fossilised-dream.html”>kupitia makala kwenye Luthfispace [6]< akieleza kwa nini sanaa ya mwandiko huo bado inaendelezwa:

Kuandika maandishi ya Ki-Urdu lilikuwa suala gumu sana; na pia kutumia mashine kuandika kwenye lugha hiyo hakukuwa na mvuto machoni kwa kulinganisha na kuandika kwa mkono. Kwa hiyo Ki-Urdu kiliendelea kutumia sanaa ya kuandika kwa mkono wakati lugha nyingine zilichukua muundo wa miandiko ya mashine.

Baada ya kuingia kwa kompyuta, mwandiko wa Ki-Urdu ulichukua sura mpya, bora zaidi. Ilimruhusu mtaalamu wa mwandiko kuandika bila kupata shida sana ya kiundishi. Hata hivyo, kitabu au gazeti lililoandikwa kwa mkono na mwandishi na kupata upigaji chapa mzuri ni zuri na linavutia sana machoni; wala mwandiko wa Ki-Urdu wa kompyuta hauwezi kufua dafu.

Tazama video hii iliyoongozwa na Ishani K. Dutta na kuandaliwa na kupandishwa kwenye You Tube na Kitengo cha Diplomasia ya Umma cha Wizara ya Mambo ya Nje ya India:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.