Utawala wa Kiislamu wa Iran umepuuza Siku ya Wanawake Duniani kwa zaidi ya miongo mitatu. Utawala huo hauitambui siku ya Machi 8, na umepiga marufuku mashirika ya wanawake kusherehekea siku hiyo. Lakini kila mwaka wanawake wa ki-Iran iwe kwa uwazi ama kificho bado wanasherehekea siku yao hiyo.
Kwa kadiri vikwazo vya kimataifa vinavyozidi kuitafuna nchi hiyo na shinikizo dhidi ya mpango wa Iran wa nyuklia linavyoongezeka, mwaka huu wanaharakati kadhaa wameweka video kwenye tovuti ya haki za wanawake iitwayo Mabadiliko kwa Usawa ikisema, “Napinga vita.”
Wanaharakati hawa wanasema::
Vita si tu mabomu na uharibifu wa nyumba zetu. Hata kabla hatujaingia vitani, inaonekana kwamba maisha ya wanawake tayari yamekuwa magumu. Vita inatishia zaidi wanawake na inakaribia, hatua kwa hatua. Hatutaki kuwa waathirika walio kimya kwa jinamizi hili. Wakati tumenyimwa fursa ya kusherehekea siku ya Machi 8, 2012 au kuonyesha matakwa yetu mitaani, tumechukua fursa hii kusema kwamba tunapinga vikali vita na kila moja ya filamu hizi fupi inaeleza sababu zetu za kufanya upinzani huo.
Ukweli nyuma ya picha za vita
Hakuna onyo kwa watoto
Vita huacha makovu kwa wanawake
Vita ni jinamizi la kweli, lakini bahati mbaya vilevile ndivyo ulivyo udikteta na gereza. Mwanablogu wa ki-Iran Jaarchi anatukumbusha [fa] kwamba wanawake wamefungwa nchini Iran kwa sababu ya harakati zao za kijamii na kisiasa.