Dondoo za Video: Utetezi wa haki za binadamu

Sehemu hii inakusudia kuonyesha posti zinazovutia za hivi karibuni kwenye tovuti ya Global Voices zinazoonyesha njia nyingi ambapo video zinaweza kuwasaidia watu kusimulia habari zao duniani kote. Unaweza kufuatilia matukio kwa maeneo kwenye chaneli yetu ya You Tube..

Mwezi huu habari kadhaa kupitia video zimejikita kwenye ukiukwaji wa haki za binadamu na hatua zinazochukuliwa kupaza sauti dhidi ya vitendo hivyo na jitihada za kuyalinda makundi ya watu wanaoonewa na jamii zilizo masikini. Bofya kwenye habari inayohusika kuona video zaidi na kujifunza juu ya masuala hayo.

Haki ya kuishi na kutokunyanyaswa

Guatemala: Kupaza sauti dhidi ya Mauaji ya wanawake wenyeji wa nchi hiyo

Shukrani kwa wanaharakati na mahakama za kimataifa kufuatia taratibu za mashtaka dhidi ya Guatemala. Tunaamini zitazingatia matumizi ya nguvu waliyokumbana nayo wanawake wenyeji kwa zaidi ya miaka 36, ambapo walikuwa waathirika kwa sababu tu ya kuwa wanawake na kwa sababu ya kuwa wenyeji.

Simulizi hilo la kina  pamoja na shuhuda kadhaa za video vinasimulia masaibu ya kutisha waliyoyapitia, masimulizi ambayo kwa sababu ya unyanyasaji waliokumbana nao waathirika hao kwenye jamii zao na hofu ya adhabu wengi wao walinyamaza kwa miongo kadhaa.

Kupigania tofauti za mitizamo ya kimapenzi

Uganda: Muswada wa kupinga ushoga ambao hautazimwa

Muswada uleule uliokuwa umewasilishwa mwaka 2009 umejitokeza tena kwa ajili ya kupigiwa kura nchini Uganda:

Uganda imeuwasilisha mezani kwa mara nyingine tena muswada wenye utata unaopinga ushoga. Mbunge wa ki-Ganda, David Bahati, aliyetoa hoja ya muswada huo mwaka 2009 kwa mara nyingine amefikiria kuurudisha tena muswada huo wa kikatili lakini ukiwa na mabadiliko kadhaa. Anadai kuondoa kipengele cha hukumu ya kifo na kile kilichopendekeza kuwafunga wanafamilia watakaoshindwa kutoa taarifa za vitendo vya kishoga kwenye mamlaka zinazohusika.

Hata hivyo, baada ya kufanyiwa upembuzi zaidi imeonekana kwamba hakuna mabadiliko yaliyofanyika kwenye mswada huo, na bado uko vilevile kama ulivyowasilishwa mwaka 2009. Video ifuatayo inaeleza athari za mswada huu kwa jamii ya mashoga (LGBT) pamoja na familia na marafiki zao:

Hong Kong: Video dhidi ya uzomeaji shuleni unaofanywa na watu wanaochukia ushoga

Nchini Hong Kong, wanafunzi katika shule wanakiri kwamba wanafunzi mashoga wanazomewa na kunyanyaswa, kwa hiyo kuna shirika limeanzisha kampeni ya kukuza uelewa wa suala hili, wakijikita zaidi kwenye kuandaa video zenye mahojiano na wanafunzi wenye mihemuko tofauti ya kimapenzi pamoja na wataalamu katika mada zinazohusika.

Haki ya kupata Elimu

Uhispania: Matumizi ya nguvu ya Polisi dhidi ya wanafunzi mjini Valencia

na

Uhispania: Mapambano makubwa dhidi ya wanafunzi yaendelea mjini Valencia

Mjini Valencia, wanafunzi wameamua kuandamana kupinga kupungua kwa bajeti kwa kuwa kunaathiri shule zao. Imefika mahali wanalazimika kwenda na mablanketi kwa sababu ya kukosekana kwa vipasha joto, katika msimu huu wa baridi kali barani Ulaya. Polisi wamewashambulia waandamanaji wakitumia nguvu kupita kiasi na kuwajeruhi baadhi yao huku wakiwatupa mahabusu wengine; video vyingi zinaonyesha kudhalilishwa kwa makundi ya watu wanaonyanyasika, wanawake na wazee.

Siku chache baada ya mapambano makali ya polisi katika taasisi ya Elimu ya Sekondari ya Luis Vives mjini Valencia [es], wanafunzi wamekuwa ndio shabaha ya vipigo, kusukumwa na ghasia kutoka kwa polisi wakati wakiwa katika maandamano ya amani, kwa kweli, wakiandamana kupinga ghasia za polisi. Wakati huu mapigano yalianza mchana  kwa nguvu isiyotarajiwa.

Haki ya kuwa na nyumba

Brazil: Jamii ya Quilombo huko Bahia nusura Itoweshwe

Moja wapo ya jamii zilizotokana na uzao wa kale wa kitumwa nchini Brazil, Quilombo Rio dos Macacos, ambapo kadri ya familia 50 zinaishi, wapatiwa tarehe kamili ya kuondolewa: Machi 4, 2012. Dai la kuwanyang’anya ardhi linakuja kutoka kwa jeshi la Brazil, ambalo linakusudia kuongeza makazi kwa maafisa wake katika eneo hilo, mpakani mwa eneo la Salvado na Simoes Filho, katika jimbo la Bahia…

Uzao wa watu wa asili ya Afrika ambao wakati wa ukoloni, walichukuliwa kutoka kwenye nchi yao kuwa watumwa nchini Brazil, wa-Quilmbola sasa wanajiona kwenye tishio jingine la kupoteza nyumba zao, pamoja na haki waliyonayo ya kumiliki ardhi wanayoishi inayolindwa na katiba ya nchi.

Simulizi hili fupi la video  [pt] linaonyesha hali wanayokabiliana nayo wa-Quilombola: wanaoogopa kupoteza nyumba zao, wakishindwa kuhama kwa uhuru wakihofia usalama wao, familia na nyumba zao.

: mwandishi wa Kiraia Atishiwa kufuatia video aliyotumiwa pasipo ridhaa yake

Video [es] hiyo iliyotengenezwa kwa ghasia zilizosababishwa na serikali dhidi ya waandamanaji waliosimama kidete kupinga kuchepushwa kwa mto kwenye jamii yao ili kupisha ujenzi wa bwawa umesabaisha mwandishi wa kiraia kupokea tishio la kuuawa.

Brazil: Mfumo wa Kimarekani wa Magereza wenye mapungufu

Matukio ya hivi karibuni katika magereza ya Amerika ya Kusini yanayogharimu maisha ya mamia ya wafungwa yamesababisha watu kuyaangalia mazingira ya kuishi na kujazana mno kunakoyakabili magereza hayo, na kuainisha iwapo kuna majanga yanayongoja kutokea. Watu ambao wamenyimwa uhuru kama adhabu ya makosa yao wanapaswa kuhakikishiwa angalau hali za maisha ya kawaida, na wakati mwingine haya hayapatikani kama inavyooneshwa katika masimulizi ya kina maisha ya magereza ya Brazili, , yanayotoa suluhisho kwa kwa hali hii ngumu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.