Habari kutoka 25 Machi 2012
Zambia: Ban Ki-Moon atoa wito kwa taifa kuheshimu haki za mashoga
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliitembelea Zambia mnamo Februari 21; ambapo alilihutubia bunge, alikutana wanasiasa maarufu na kutembelea Maporoko ya Viktoria, hakuna katika haya yaliyogonga vichwa vya habari kama mwito wake wa taifa hili kuheshimu haki za mashoga.
Dondoo za Video: Utetezi wa haki za binadamu
Kuna masimulizi kusisimua katika siku za hivi karibuni kwenye tovuti ya Global Voices Video za Utetezi ikiwa ni pamoja na haki za wananchi wenyeji na habari za hivi karibuni kutoka Amerika ya Kusini, Mashariki ya Mbali, Ulaya Magharibi na Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zilizochaguliwa na Juliana Rincón Parra.
Iran: Wanawake wapinga ‘Jinamizi la Vita’
Utawala wa Kiislamu wa Iran umepuuza Siku ya Wanawake Duniani kwa zaidi ya miongo mitatu. Utawala huo hauitambui siku ya Machi 8, na umepiga marufuku mashirika ya wanawake kusherehekea siku hiyo. Lakini kila mwaka wanawake wa ki-Iran iwe kwa uwazi ama kificho bado wanasherehekea siku yao hiyo.
Korea Kusini: Wahudumu wa ndege wapigania haki ya kuvaa suruali
Katika Siku ya Wanawake Duniani, wahudumu wa moja ya mashirika makubwa ya ndege nchini Korea Kusini, waliitisha mkutano na waandishi wa habari mbele ya makao makuu ya shirika lao la ndege kudai haki ya kuvaa suruali. Madai hayo yamepata uungwaji mkono mkubwa sana na watumiaji wa mtandao wa nchini humo.