Palestina: Gaza yashambuliwa, watu 12 wauwawa na wengine wengi kujeruhiwa

Usiku kucha wa Machi 9 hadi asubuhi ya Machi 10, 2012, ndege za kivita za Israeli zilifanya mashambulizi kwa kuchagua maeneo kwenye Ukanda wa Gaza, na kuua takribani watu 12 na kuacha wengine 20 wakiwa majeruhi.

Mchana wa Machi 9, Zuheir al-Qaysi, katibu mkuu wa chama cha (PRC) Popular Resistance Committees , aliuawa pamoja na msaidizi wake Abu Ahmad Hanani kutokana na mashambulizi hayo ya Israel kwenye Jiji la Gaza. Hanani alitokea Nablus kwa asili na alihamishiwa Gaza kama mmoja wa wafungwa walioachiwa huru katika mpango wa kubadilishana wafungwa miezi michache iliyopita.

Katika kujibu mashambulizi, vikundi vya ulinzi vya ki-Palestina vilivyo kwenye Ukanda wa Gaza vililipua mabomu kuelekea Israel, bila kudhuru mtu yeyote. Israel ilijibu mapigo kwa mashambulizi makali ya angani yaliyoilenga Gaza na kuacha maiti wapatao kumi na wawili kwa mara moja. Majina yao yalitajwa na Shirika la Habari la Ma’an kuwa ni pamoja na: Muhammad al-Ghamry, Fayiq Saad, Muatasim Hajjaj, Ubeid Gharabli, Muhammad Hararah, Hazim Qureiqi, Shadi Sayqali, Zuheir al-Qaysi, Mahmoud Hanani, Muhammad Maghari, Mahmoud Najim, na Ahmad Hajjaj. Ripoti nyingine zinataja kuwa watu kumi na watano walipoteza maisha yao.

Mji wa Gaza ukipigwa mabomu na madege ya kijeshi ya Israel. Picha ya Mtumiaji wa twita aitwaye @journeytogaza

Watumiaji wa Mtandao waishio Gaza waliitikia mashambulizi hayo kwenye Twita:

@MaathMusleh: Watu 15 wameuawa mjini Gaza mpaka sasa, hakuna SHAKA watakuwa ni wa-Palestina!! #GazaUnderAttack

@ectomorfo: Ombea watu wa Gaza. Hakuna umeme, kuna dawa kidogo, hakuna gesi. Na sasa wanapigwa mabomu kutokea pande zote na #Israel. #GazaUnderAttack

@Omar_Gaza: Dakika 18 bila milipuko! Kimya cha tahadhari? Yamekwisha? Au niendelee kubana pumzi zangu kwa woga? #GazaMassacre #GazaUnderAttack

@najlashawa:sijui nimewezaje kuendelea kuchapa maandishi haya. Sauti ilikuwa KUBWA! #GAzaUnderAttack

@imNadZ: Karibu #Gaza. Ambapo mwanga wake unatokana na mabomu. Ndege zinazotumika ni aina ya F16.

Shambulio hili linakuja wakati wa kuhamisha ushirika wa kimaeneo na kisiasa. Juma lililopita, kwa kuongezeka kwa uwezekano wa vita ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, maafisa wawili wa juu wa Hamas walitangaza kwamba Hamasi haitajihusisha na itaiunga mkono Iran ikitokea Israel itashambulia. Hamas pia walitangaza kuwaunga mkono watu wa Syria katika mapambano yao dhidi ya Assad.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.