Korea Kusini: Wahudumu wa ndege wapigania haki ya kuvaa suruali

Katika siku ya wanawake duniani mwaka huu, mnamo Machi 8, 2012, kuna maandamano yaliyofanyika katika jiji la Seoul, Korea Kusini. Wahudumu wa kike wa moja ya mashirika makubwa ya ndege ya taifa hilo, Shirika la Ndege la Asiana, , waliitisha mkutano na waandishi wa habari mbele ya jengo la Kumho Asiana wakiituhumu kampuni hiyo kwa kuwa na sharti la ubaguzi wa kijinsia kuhusu namna wahudumu wanawake wanavyopaswa kuonekana.

Park Bong (@jayparkbong),mwanachama wa shirika la kutetea haki za wanawake, alituma ujumbe [ko] :

실핀 개수, 눈화장 색, 스타킹 색까지 규정하고 있는 아시아나 외모복장규정. 안경 불가 규정 때문에 건조한 비행기안에서 렌즈를 껴야 하고, 커트 머리도 몇 년 전 파업으로 간신히 따낸것이라 한다. 여성노동력을 어떤 시선으로 보고 통제하고 활용하고자 하는지 너무 티난다.

Sharti la Asiana juu ya mwonekano na sare linadhibiti idadi ya pini zinazotumika kufungia nywele, rangi gani za kuremba macho na hata rangi ya soksi. Kwa kuwa miwani hairuhusiwi kuvaliwa ndani ya ndege, wanapaswa kuvaa lensi maalumu machoni katika mazingira hayo makavu. Haki ya kutengeneza nywele fupi waliipigania na kufanikiwa kupitia mgomo miaka michache iliyopita. Vitendo hivi vinaonyesha wazi namna gani kampuni hii inavyomtazama mwanamke, yaani kama nguvu kazi tu, na huku ikiwa na shauku kubwa ya kuendelea kumdhibiti na kumtumia mwanamke kama chombo.
Asiana Flight Attendants

Picha iliyopigwa kutoka kwenye video ikiwaonesha wahudumu wa Shirika la Ndege la Asiana. Picha hii iliwekwa awali kwenye mtandao wa YouTube na mtumiaji alitwaye Rogapol.

Baadae alituma ujumbe [ko] kuhusu maandamano hayo:

금호아시아나 빌딩 앞에서 여성승무원에게 바지를 허하라는 기자회견을 하고 사무실 들어가는 길. 104주년 여성의날인데 정말 이런 내용의 시위를 하고 있어야 한다는게 이 나라 여성의 현실. 짜증난다.

Sasa ninarudi ofisini baada ya kuhudhuria mkutano na waandishi wa habari mbele ya jengo la Kumho Asiana tukitoa wito kwa shirika hili la ndege kuwaruhusu wahudumu wanawake kuvaa suruali. Leo ni maadhimisho ya 104 ya siku ya wanawake duniani na sasa ndio ninafanya maandamano ya namna hii. Hali na hadhi ya namna hii kwa mwanamke katika nchi hii vinachanganya.

Kwa mujibu wa makala ya habari ya Hankyoreh ambayo ilisambazwa sana kwa watu bila ruhusa zao siku chache zilizopita, Shirika la ndege la Asiana ndilo lenye kanuni ngumu kupindukia kwa ajili ya wahudumu wa kike: sare zao ni sketi pekee – hakuna mbadala wa suruali. Sketi ni lazima zifike angalau kwenye magoti. Wahudumu hao wa ndege hawawezi kuvaa miwani. Nywele lazima ziwe mahali pake angalau ziache sehemu kubwa ya uso bila kufunikwa. Pini mbili tu za kufungia nywele ndizo zinazoruhusiwa. Masharti pia yanahusu ukubwa wa hereni na mikufu. Mistari ya kuchora kuzunguka macho na nyusi lazima iwe myeusi au kahawia.

Asiana walijibu kwamba sababu ya kutokuwa na suruali kama sare za wanawake ni kwamba suruali “hazifanani na sura ya biashara ya kampuni hiyo.”

Wakiunga mkono kwa minajili ya kupaaza malalamikoya wahudumu hao wa kike, watumiaji wengi wa mtandao wa Korea Kusini walionyesha hasira zao kwa sera ya ubaguzi wa kijinsia ya kampuni hiyo. Mtumiaji wa Twita  @vanilladoll8 alituma ujumbe [ko]:

여성 근로자의 “외모” 따위로만 설명할 수 있는 회사 이미지란.. 참.. 하찮다.. 예쁜 승무원이 아닌 안전한 비행, 편안한 서비스.. 이런게 이미지가 되어야 옳지 이 양반들아[…]

Sura ya kibiashara ya kampuni hii ni finyu namna gani kama inaweza kuelezewa kwa mwonekano wa waajiriwa wa kike. Wanapaswa kujali zaidi usalama wa safari zao za anga na kutoa huduma zinazoridhisha, badala ya wahudumu warembo.

@Astralpink anaonya [ko] kwamba kuweka msisitizo wote kwa mwonekano wa wahudumu wa kike kunaweza kuwakera watu na kuwafanya wafikiri kugomea ndege zao.

여성 승무원들에 대한 불필요하고 성차별적인 용모, 복장 규정에다가 바지 유니폼을 허용하지 않고 근무 시, 비상 시 불편한 치마 유니폼만 고집하는 아시아나 항공 @Flyasiana.승객 안전보다 승무원 용모를 중시하는 항공사라면 불매하게 될지도.

Sera ya shirika hilo la ndege kuweka msisitizo zaidi kwenye mwonekano wa wahudumu wa kike na sare haina maana kwamba ina ubaguzi wa jinsia. Kampuni inasisitiza wavae sketi pekee ingawa hiyo ni kero katika mazingira yao ya kazi na (mbaya zaidi zinapokuja) nyakati za dharura. Kama shirika hili linajali zaidi mwonekano wa wahudumu kuliko usalama wa abiria wake – watu wataligomea.

Lee Jung-hoon(@sm749alituma ujumbe huu [ko]:

m.hani.co.kr/arti/society/l…아시아나항공 승무원은 바지입으면 안된다네요. 시대착오적이고 인격체로 보지 않고 기업의 이익을 극대화 하기 위한 상품 (으로 보는) 복장 용모규정 70년 박정희 시대인가

Suruali haziruhusiwi kwa wahudumu wa shirika la ndege la Asiana. Sharti hili limepitwa na wakati na ni kuwatumikisha wanawake kama vifaa vya kuwanyonya ili kukuza faida ya kampuni, badala ya kuwachukulia kama binadamu. Inaonekana kama sera ya kampuni hii ni ya miaka ya sabini chini ya utawala wa (Rais wa zamani wa Korea Kusini) Park Jung-hee.

Mtandao wa uanaharakati wa bidhaa wa Korea Kusini uitwao  Network for Glocal Activism [ko]umefungua mashitaka  [ko] yaliyosomeka:

이와 같은 규정들은 항공사가 […] 여성 승무 노동자들을 ‘관리'의 대상으로 보고 있음을 보여주는 것이다.[…] 기업들의 이러한 행태는 여성 노동자들이 수행하는 업무의 전문성을 보이지 않는 영역으로 밀어내 버리고…

Sharti hili linaonyesha kwamba shirika hili la ndege linamtazama mwanamke kama kifaa kinachohitaji kutawaliwa/kudhibitiwa na […] mashirika. Mtazamo kama huu dhidi ya wanawake unashusha utendaji kazi wa waajiriwa wanawake.

Shitaka hilo limeongeza kwamba sharti kuhusu wahudumu wa kile lina kurasa tano, wahudumu wa kiume wanatarajiwa tu kuimarisha “mwonekano nadhifu na usafi”.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.