Baada ya Kony 2012, “What I Love About Africa” Yanyakua Mazungumzo

Hii ni mojawapo ya maandishi maalum yanayofuata Kony 2012.

Yeyote anayefuata habari kutoka kwa raia wa kawaida katika mtandao mwezi huu hakika ameona mjadala ulioenea duniani kuhusu kampeni lijulikanalo kama ‘Invisible Children’[en], ambalo limeenea duniani, na lina nia ya kumkomesha mhalifu na kiongozi wa jeshi la waasi, Joseph Kony.

Ilhali kampeni la Kony 2012[en] hakika limepata usikivu lililotaka, Waganda na Waafrika wengi wanaona kwamba ujumbe wake umekosa muktadha na maelezo sahihi kuhusu Joseph Kony. Zaidi ya hiyo, kampeni lenyewe lilijishughulisha na kuchanga pesa kwa shirikisho lililoanzisha kampeni lenyewe badala ya kuwawezesha watu walioathiriwa [en] na vita hivyo kujiendeleza.

Zaidi ya hayo, raia wengi wa Afrika wanaona kuwa habari kuhusu Bara la Afrika ambazo zinaonyesha mabaya zaendelea kuenezwa, badala ya wanahabari kuripoti kuhusu maendeleo mazuri ambayo yameenea barani Afrika hivi karibuni.

Ili kukabiliana na hali hii[en], watu wengi wameanza kuandika hadithi na kadalika katika Twitter kusema ni nini haswa wanapenda kuhusu Afrika, wakitumia maneno #WhatILoveAboutAfrica[en]. (Nini Nipendacho Kuhusu Afrika)

#WhatILoveAboutAfrica ilivyoenea duniani: Picha kwa hisani ya Semhar Araia – @Semhar

Hatua hii, iliyoongozwa na Semhar Araia [en], mwanablogu katika Diaspora African Women Network (Shirika la Wanawake Walio Ugenini),[en] ilianza kuenea duniani katika Twitter[en] tarehe 13 Machi 2012.

Upande mwingine wa hadithi

Ilhali hakuna anayepinga umuhimu wa kuonyesha uhalifu uliotendwa na Jeshi la Kony, lijulikanalo kama LRA[en], ripoti zifuatazo kutoka kwa raia wa kawaida zaeleza jinsi mjadala huu ni zaidi ya mawazo matupu yanayoenezwa kutumia mtandao, au meme[en] kwa Kiingereza, lakini ni vita vya kukomboa mawazo na mtazamo wa walimwengu kuhusu bara zima.

Wakati kundi la wenyeji wa Kaskazini mwa Uganda, ambao waliathiriwa zaidi na uhalifu wake Kony, walionyeshwa video ya Invisible Children katika onyesho la hadhara, hawakupendezwa na waliyoona katika video hilo, kama inavyoonekana katika video ya Al Jazeera English ifuatayo.

“Kama watu walio katika nchi hizo wanatujali, hawatavaa shati zilizo na picha za Joseph Kony kwa nia yoyote”, alisema mwanaume mmoja aliyehojiwa. “Huko ni kusherehekea kuteseka kwetu.”

“Kuna watu fulani, shirika fulani linalotaka kutafuta pesa kwa kutumia ghasia iliyofanyika Kaskazini mwa Uganda”, Mganda mwingine katika onyesho lingine alisema.

Kampeni la kuonyesha upande mzuri wa Afrika pia umeimarishwa katika mtandao. Mwanafunzi kutoka Amerika anayependa Afrika, Karen Killenberg, alikusanya vichapisho vichache alivyovipenda[en] kuhusu jinsi watu wanavyopenda Afrika, na pia anamanukuu mwanablogu Tatenda Muranda[en] katika Twitter kuhusu sababu zake za kuandika:

@IamQueenNzinga: It's about time we ushered in the era of afro-optimism through words and action
Wakati umefika kwetu kueneza enzi ya matumaini kupitia maneno na vitendo.

Mwanahabari Paula Rogo kutoka Kenya alikusanya na kuhariri “maandishi bora na mabaya” kuhusu mazungumzo ya vitu ambavyo watu wanapenda kuhusu Afrika, ama “WhatIloveAboutAfrica”. Yafuatayo ni maandishi kadhaa ambayo yalikusanywa:

@mwanabibi: #WhatILoveAboutAfrica The youth! Hopeful, optimistic and innovative
“Ninachopenda kuhusu Afrika ni vijana! Wana matumaini, matarajio na ni wabunifu pia”

@Sarenka222: #WhatILoveAboutAfrica resilient, perceptive, courageous, independent press, even in the face of intimidation (cc: @dailymonitor :)
“Ninachopenda kuhusu Afrika ni ustahimilivu, ushujaa, uhuru wa vyombo vya habari hata wakipata vitisho”

@RiseAfrica: RT @texasinafrica: Innovations like mobile money, crowdsourced crisis mapping. #WhatILoveAboutAfrica
“Jinsi walivyo wabunifu, kwa mfano kutuma pesa kwa kutumia simu za mkononi, kukusanya habari inayotumiwa kutengeneza ramani ya sehemu ambako kuna ghasia, hizo ndizo nizipendazo kuhusu Afrika

Map of Africa tagged by participants of Barcamp Africa in October 2008, from the Maneno Flickr photostream

Ramani ya Afrika iliyo na maandishi ya washiriki wa Barcamp Africa, mwezi wa Oktoba 2008, kutoka kwa picha za Maneno kwenye Flickr photostream

Vita vya kale kusimulia hadithi ya Afrika

Kunyakua jinsi hadithi na habari za Kiafrika zitakavyosimuliwa kupitia mikondo ya mtandao si jitihada mpya. Mwaka wa 2007, kampeni kama hii ilienea kupitia mikondo ya mtandao barani Afrika, wakati wanablogu mashuhuri waliwakaribisha wanablogu wenzao kutoa maoni yao kuhusu “Kwa Nini Naandika Blogu Kuhusu Afrika”.

Mwanablogu kutoka Cote d'Ivoire, Théophile Kouamouo aliuliza mnamo mwaka 2008 [fr]:

Bloguons nous pour la diaspora et le vaste monde, coupé de nos contemporains sur le continent ? Blogue-t-on sur l'Afrique comme on blogue sur l'Europe ou l'Asie ? La blogosphère afro-orientée a-t-elle quelque chose de spécifique à offrir au concert de l'universel version 2.0 ?

Je, tunaandika katika blogu zetu ili watu walio nchi za nje na maeneo yaliyo mbali zaidi wasome, tukijitenga na wenzetu katika bara la Afrika? Kuandikwa kwa blogu kuhusu Afrika kunafanywa kwa njia sambamba na kuandikwa kwa blogu kuhusu Uropa au Asia? Je, blogu zinazozingatia bara la Afrika zina kitu maalum cha kutolea dunia toleo la pili la dunia?

Mimu hii inashangaza kwa sababu ilisababisha watu kutoka maeneo tofauti, kuanzia Afrika Magharibi na kuenea hadi maeneo yote ya bara la Afrika, hadi eneo la Afrika linalozungumza kiingereza[en]. Kama ufafanuzi wa mimu wakati huo, Rombo, ambaye anaandika blogu liitwalo What an African Woman Thinks” alitoa jibu kuhusu nini anachopenda katika bara la Afrika[en]:

Africa is under my skin. Africa is the voices in my head. Africa is the itch on my back that I can’t quite reach.
[…] She’s beautiful and she’s strong and she’s got so much to give, she inspires me and I love her truly madly deeply.
She’s battered and bruised and sometimes broken and I love her even more.
She’s always on my mind and in my heart.
It’s not so much, then, that I choose to blog about Africa. It’s that I can’t not.
I really wish the world would see in her all that I see in her.
That’s another reason why I blog about Africa: To make this wish come true.

Afrika imo ngozini mwangu. Afrika ni sauti iliyo kichwani mwangu. Afrika ni hisia ya kujikuna mgongoni ambayo siwezi kufikia.
[…] Yeye ni mrembo na mwenye nguvu, ana mengi ya kupeana, ananipa busara, nami nampenda kwa undani na moyo wangu wote.
Yeye amepigwa na kuachwa na alama, wakati mwingine amevunjwa, hata hivyo nampenda zaidi.
Yeye yupo daima mawazoni mwangu na katika moyo wangu.
Hivyo basi, sichagui kuandika kuhusu Afrika, bali ni sababu siwezi kutoandika.
Naungependa dunia imuone, na ione kile ninachoona ndani yake.
Hiyo ni sababu nyingine kwangu kuandika kuhusu Afrika, ili azimio langu lipate kuwa kweli

Sokari, wa blogu liitwalo Black Looks aliongezea wakati huo:

… she makes me angry and frustrated, lets me down, goes on walkabouts and is influenced by some pretty horrible characters many from distant lands. But I cant help loving her deeply – she is alive, she is real and wise with so many wonderful meaningful stories of humanity and life. She is rich in stature and spirit. I love the way she moves, her facial expressions, the taste of her food and the smell and colours of the earth

…yeye hunitia hasira na hunichanganyisha, huniacha sakafuni na kuenda matembezini, na kushawishiwa na baadhi ya wahusika wanaotisha kutoka nchi za mbali. Hata hivyo, nampenda kwa undani – yeye yu hai, yeye ni halali, ana hekima na hadithi nyingi za ajabu kuhusu maana ya kuwa binadamu, na maisha. Yeye ni tajiri kwa kimo na kwa roho. Napenda jinsi anavyosonga, usemi wa uso wake, ladha ya vyakula vyake na harufu na rangi za ardhi

Mapambano kuhusu hadithi ya Afrika ni hadithi nzee sana. Binyavanga Wainaina ameandika insha maarufu ijulikanayo kama “‘Jinsi ya kuandika kuhusu Afrika’“[en] mwaka wa 2005. Insha hii ilitumiwa kutengeneza video inayoitwa “Jinsi ya kutoandika kuhisi Afrika” iliyosimuliwa na muigizaji Djimon Hounsou:

Tukitazama jitihada ya muda mrefu ya kuoyesha upande mzuri wa bara la Afrika, mtazamaji wa kawaida atashindwa ni kwa nini imekuwa changamoto kubwa kubadilisha jinsi walimwengu wanalitazama bara la Afrika, na kwa nini hii ni muhimu kwa watu wengi.

Kama jibu la kuonyesha umuhimu wa kuonyesha upande bora wa bara la Afrika ulionyeshwa katika Kongamano la TED Africa na Euvin Naidoo, mwenyekiti wa Chumba cha Biashara. Anasema kwamba uaminifu ni mojawapo ya sehemu za uwekezaji barani Afrika, na kuelewa mahitaji madogo madogo barani kunahitajika. Anasema:

George Kimble said, ‘The only thing dark about Africa is our ignorance of it.’ So let's start shedding light on this amazing eclectic continent that has so much to offer [..] The first myth to dispel is that Africa is not a country. It’s made up of 53 different countries. So to say ‘invest in Africa’ is a no-go. It's meaningless.

George Kimble alisema, “Kitu cha pekee ambacho kiko na giza barani Afrika kutojua kwetu. Sasa tuanze kumulika bara hili lnaloshangaza na lililo na mchanganyiko spesheli, ambao una mengi ya kutupa [..] Imani potofu la kwanza ambalo tutakatiza ni kwamba Afrika si nchi moja. Ni bara ambalo lina nchi 53 tofauti. Kwa hivyo, kusema ‘wekeza pesa au mali yako Afrika’ haina maana.

Chapisho hili ni moja ya maandishi maalum kuhusu Kony 2012.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.