Hong Kong: Raia wasema ‘Hapana’ kwa uchaguzi wa meya usio wa kidemokrasi

Miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Kumchagua Mtendaji Mkuu wa Hong Kong wapatao 1,200, wajumbe 689 walimchagua Leung Chun-ying kuwa meya mpya mnamo tarehe 25 Machi kufuatia ushawishi mkubwa uliofanywa na Ofisi ya Ushawishi ya Serikali Kuu ya Watu [2] ya Hong Kong. Matokeo yalipotangazwa, maelfu ya waandamanaji walipinga uchezewaji huo wa mchakato wa uchaguzi. Waliendesha maandamano hayo nje ya ukumbi wa muda wa uchaguzi.
Kura ya maoni ya kiraia ya majaribio

Kabla ya uchaguzi, kati ya Machi 23 hadi 24, zaidi ya raia 220,000 wa Hong Kong walishiriki kwenye “kura ya maoni”<>[3]” ya majaribio iliyoandaliwa na Programu ya Maoni ya Umma ya Chuo Kikuu cha Hong Kong ili kuonyesha kutoridhishwa kwao na uchaguzi wa kikundi kidogo cha watu na kudai haki yao ya kumchagua meya wa jiji.

Licha ya mfumo wa kupiga kura kushambuliwa na ‘waiba taarifa za mtandaoni’[4], maelfu ya wapiga kura wenye kustahili (wakazi wa jiji walio na umri wa zaidi ya miaka 18) walisisitiza kutaka kupanga mstari nje ya vituo vya kupigia kura kusubiri zamu zao:

Polling station at Poly University on March 24. From Facebook Page: Civic Referendum

Kituo cha kupigia kura katika Chuo Kikuu ya Poly mnamo tarehe 24 Machi. Kutoka katika ukurasa wa Facebook: Civic Referendum

Mtumiaji wa Facebook Leung Chau Ming aliyekuwa kwenye mstari wa kusubiri zamu nje ya moja ya vituo vya kupigia kura[6] mnamo tarehe 23 Machi; alieleza[7] [zh] namna alivyoguswa na yale aliyoyaona kupitia ukurasa wa Facebook wa tukio la kura ya maoni:

當時我身在其中, 寒風中大家也很自律, 有老中青, 更有媽媽在邊排隊邊給小朋友餵飯。

深明今天所為, 從64至71到323 etc., 未會於 有生之年 見証 民主之成果; 但為下一代…下兩代…下下下N代,我們是有責任的, 亦是 每個香港人 此時此刻 應盡的義務!

Nilikuwa kwenye foleni. Tulizingatia utaratibu licha ya upepo mkali. (Walikuwepo) wazee, watu wazima na vijana. Hata kuna mama mmoja alimlisha mwanae huku akiwa kwenye foleni. Ninaelewa vema kuwa licha ya mapambano na mikutano yote ya hadhara mnamo tarehe 4 Juni[8] [siku ya mkesha wa kuwasha mshumaa], 1 Julai [9], na [mwaka huu] Machi 23 [maandamano ya kupinga uingiliaji wa Beijing kwenye uchaguzi], n.k. Pengine hatutaona matunda ya demokrasi katika kipindi cha uhai wetu, lakini kwa kizazi kifuatacho, kizazi kitakachofuata baada ya kizazi kijacho, … idadi N ya vizazi vijavyo. Tuna wajibu. Ni wajibu wa kila mkazi wa Hong Kong hapa, na sasa!

Thomas Pang naye alikuwa kwenye msululu wa kusubiri zamu, naye alieleza kwa nini alikuwa tayari kushiriki kwenye uchaguzi huo wa majaribio:

HIYO NDIYO HALI YA SASA, TUNACHOTAKA NI MABADILIKO. HATUTAKI TENA “SIASA ZA KICHINA ZA KWENYE KASRI”. NDIYO SABABU TUMEKUJA KUPIGA KURA. TUNAFANYA HIVI KWA SABABU HATUTAKI VIZAZI VYETU VIJAVYO KUPITIA HALI HII TENA. NATUMAINI LOSO ITAELEWA.

Hatimaye jumla ya watu 222,990 walishiriki kwenye uchaguzi huo wa majaribio, ambapo asilimia 54.6 walipiga kura bila kuandika chochote kwenye karatasi za kura. Leung Chun-ying alipata tu asilimia 17.8 ya kura zote, ambapo matokeo yalikuwa kinyume kabisa na uchaguzi wa kundi lile dogo la wateule, ambao uliendeshwa katika Kituo cha Mikutano na Maonyesho cha Hong Kong.

Maandamano nje ya ukumbi wa jiji tarehe 25 Machi

Mnamo tarehe 25 Machi, zaidi ya watu 2,000 waliandamana nje ya ukumbi wa muda wa uchaguzi. Huku wakiwa wamekasirishwa sana na ushindi wa Leung, walipambana na kusukumana na ukuta wa polisi. Hapa chini kuna baadhi ya picha zilizopigwa na waandishi wa habari za kiraia kama zilivyotumwa inmediahk.net kuhusiana na mwonekano wa maandamano hayo:

Protesters pushing the police barricades on March 25. Image by Flickr user inmediahk (CC BY-NC).

Waandamanaji wakisukumana na ukuta hai wa polisi mnamo tarehe 25 Machi. Picha na mtumiaji wa Flickr inmediahk (CC BY-NC).

 width=

Waandamanaji wakiwa wameketi nje ya ukumbi wa uchaguzi. Picha na mtumiaji wa Flickr inmediahk (CC BY-NC).

Waandamanaji wakiwa wameketi nje ya ukumbi wa uchaguzi. Picha na mtumiaji wa Flickr inmediahk (CC BY-NC).

Joshua Wong, ambaye ni mwanaharakati kijana, alifanya tafakari kuhusu maandamano na kuonyesha wazi huzuni yake [zh]hasa kwa kukosa utayari kwa watu katika kuchukua hatua:

還記得今天在會展外的馬路坐下時,忽然有人大叫:「梁振英當選!」,群眾們立即站立起哄,面上流露著驚訝的神情。我本身對梁振英當選也有心理準備,但也想不到他可在第一輪投票以689票立即當選。

回家時十分痛心,我痛心的不是梁振英當選,我痛心的是大家的那種犬儒和事不關已的心態,「邊個做特首都唔關我事,平平安安和和諧諧咪算」、「懶衝動只會搞到政局亂哂搞臭香港個名」、「抗爭完都無用架啦」、「呢個世界邊有真正民主」……

我很想告訴大家,梁振英當選並不可怕,可怕的是大家對強勢政治和硬推政策無動於衷,即使將來對遊行集會的打壓會越來越強,但我乃我始終如一地相信群眾運動的力量,特別很想告訴各位同學和朋友,嘗試第一次的社會行動,把握今年的七一遊行,讓大家以一個又一個足印,告訴中共政權,我們不要這個由小圈子選舉產生,只有18%認受性的梁振英特首。

Nakumbuka nilikuwa nimeketi kando ya barabara kwenye Kituo hicho, kisha kuna mtu alipaaza saudi akisema, ‘CY Leung ameshinda!’ Watu walisimama na kutoa mguno wa hasira. Wengi walipigwa na bumbuwazi. Nilitarajia kwamba angeshinda, lakini sikutegemea kuwa angefanya hivyo katika raundi ya kwanza tu tena kwa kura 689.

Nilivunjika moyo niliporejea nyumbani, siyo kwa sababu ya ushindi wa Leung, bali hisia za umimi na kujitenga: ‘Sijali, yeyote atakayekuwa Kiongozi Mkuu, hili si suala langu, ili mradi tu [jamii] iko salama na kila kitu ni shwari’, ‘Msukumo utasababisha fujo za kisiasa na kuharibu jina la Hong Kong.’, ‘Hayana maana, hata baada ya maandamano yenyewe’, ‘Hakuna demokrasi ya kweli popote duniani'…

Ningependa nikueleze yote hayo, Ushindi wa Leung si wa kutisha; hofu ipo katika kutokujali kwa watu kuhusu siasa za mkono wa chuma za baadae. Hata kama ukandamizaji wa haki ya kuandamana na kukusanyika utaongezeka, bado ninaamini katika nguvu ya umma. Hasa, ningependa kuwatia moyo wanafunzi na marafiki kujiunga na harakati hizi za umma, hasa kutumia vema nafasi ya maandamano ya tarehe 1 Julai. Hebu tutoe kishindo kitakachoueleza utawala wa Kikomunisti wa China kwamba hatumtaki Leung Chun-ying ambaye “anachaguliwa” na kikundi kidogo na tena chini ya asilimia 18 ya ridhaa ya umma, ili kuwa Kiongozi wetu Mkuu.

Maandamano mengine ya kupinga uingiliaji kati wa Beijing katika siasa za Hong Kong yatafanyika kesho tarehe 1 Aprili.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.